Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Kwa hiyo Mdee na Bulaya wameendaje bila katibu kupeleka majina? Nyie watu mtaongopewa hadi lini?? Mnyika anajua anachofanya na hao kina Mdee
Nimemsikia Halima akitoa hotuba fupi baada ya kuapishwa akikishukru chama na Mwenyekiti wake Mbowe. Kwamba chama na Chairman wametoa baraka zao zote kwa Wabunge 19 wa kuteuliwa kwenda kula kiapo!

Nina amini CHADEMA uongozi wa juu kwa maana ya CC na watakuwa wamekaa na kuzungumxia hii habari. Naamini Tundu Lissu atakuwa amehusishwa na kufikia mwafaka l

Mimi napenda kuwapongeza CHADEMA kwa uamzi huu wa kishujaa. Nitaeleza :
  1. Wamepeleka Wabunge wanawake ambao ni MAJEMBE kwa kuchangia hoja, kujenga hoja,kupangua na kuchambua hoja. Sina shaka na Halima, Esther, Pareso na wengine ni Wabunge makini sana,
  2. CHADEMA wameona mbali. Kwa vile JIWE alikuwa na nia ya kuua na kufuta UPINZANI Bungeni hasa KUB kwa move hii JIWE atakwama. Tayari CHADEMA ina Wabunge 20 ndani ya Bunge watakaou ngana na wale wa ACT Wazalendo na yule 1 wa CUF.
  3. Napendekeza Mhe. Halima Mdee awe Kiongoxi wa KUB ili apambane na mafisi wa CCM Bungeni.
  4. Hii itakuwa ni FURSA YA CHADEMA, ACT na CUF kupaza sauti zao kuelexa MADUDU NA MAOVU YOTE YA WIZI WA KURA ULIOFANYWA NA CCM wakti wa Uchaguzi Mkuu wa 2020.
  5. CHADEMA pia watakuwa wameepuka kufutika katika siasa za Upinzani kwa kuendelea KUPATA RUZUKU ITAKAYO KISAIDIA CHAMA KUJIENDESHA. Tusidanganyane chama bila fedha iwe ya Michango ya Wanachama au RUZUKU hakiwezi ku-survive.

Hivo wabunge 19 mlioteuliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA Bungeni kapigeni kazi kuonesha uhai na uwepo wa CHADEMA Chama chenye nguvu Tanzania. MUNGU IBARIKI CHADEMA.

 
Erythrocyte unaitwa huku? Njoo ujibu imekuwaje wakati jana na kibaraka wako mliitangazia dunia kuwa hamtashiri bunge. Au hawa wamenunuliwa?
 
Naona tunatafutiana ban tu sasa. Akili yako jaribu kuichakata ili unaposoma sarcatic comment uielewe bila kutumia torch
 
Esau aliuza uzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake Yakobo, simply alikuwa na njaa na hakuna na mbadala wa kutulinza njaa wakati huo.

It's hard to negotiate at point of weakness.

Ila inabidi maisha yaendelee na muda utasaidia watu ku-heal kutoka kwenye maumivu na kuna watu inabidi wajifunze kutokuwaamini sana watu wenye "maslahi ya kudumu"
 
Kakaaa usicheze na njaa kaka.Wengine waliacha nyumba zipo kwenye Linta.
 
Nonsense, halafu useme uchaguzi haukuwa huru na haki?
 
Hii inaleta taswira gani?

Chama hakina msimamo? Njaa? au ubinafsi wa viongozi?

Kwaiyo mlivyotaka tuandamane tuvunjwe miguu, afu baadae mkae meza ya maridhiano mkubaliane sio?
Aseee akili za kuambiwa changanya na zako, wa Tz wenzangu tuwe makini na wasaka tonge usimwamin mwana siasa yeyote yule, Familia yako ni bora kuliko chama.
 
Kumbe ulikuwa unawaamini? Watu wanatafuta kula hamna lolote
Kutafuta kula ni dhambi? Mbona kuna watu wanatafuta kula kwa njia haramu kama kuuza mwili, itakua hawa ambao katiba inawatambua?!
 
Hawa ndio mlitaka muwape nchi[emoji23][emoji23][emoji23]

This time i hope watakua kimyaa sana.
 
Leo naenda kuchoma kadi yangu ya CHADEMA na kujiunga rasmi na ACT-Wazalendo!
Siasa haiitaji hasira. Chadema hawakuwa na jinsi ya kukwepa huo mtego. Kukataa kupeleka hao wabunge ilkua ndio kujiua kisiasa kbsa. Wangepotea kwenye akili za watu
 
Leo naenda kuchoma kadi yangu ya CHADEMA na kujiunga rasmi na ACT-Wazalendo!
Hahaa, na wao wakijiunga na Sirikali ya Pamoja/Umoja wa Kitaifa Zanzibar kufuata maridhiano utafanyaje, utajiunga na Mzee wa Ubeche?
 
Tunaowajua chadema hatushangazwi,tulijua tu huwa wanabweka mitandaoni,
Chadema hawana ubavu wa kuacha ruzuku,kelele zote za kuibiwa kura zimekuwa null and void!
Salary Slip na vikaragosi wenzako,mtaweka wapi sura zenu,uchaguzi umekwisha rasmi
 
Hebu tutafute ukweli wa hili jambo ndo tuanze kulaumu unaweza kuta ni habari gushi pia wabunge wanaapa bungeni mbona hill eneo si bungeni hawa wanatuchezea akili zetu
 
Umeandika pumba tupu futa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…