Hatimaye wazawa wamvaa Kafulila kuendesha mradi wa UDART

Hatimaye wazawa wamvaa Kafulila kuendesha mradi wa UDART

View attachment 3159803

===
CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA), kimeonesha nia yake ya kutaka kuwekeza katika mradi wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi huku ikiomba kufupishwa kwa masuala ya michakato katika kuingia ubia huo.

Tamstoa imeonyesha nia hiyo leo Ijumaa Novemba 22,2024 walipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Tanzania, David Kafulila, ambapo pamoja na mambo mengine walitaka kujua taratibu gani za kufuata ili kufanikisha hilo.

Wafanyabishara hao wanakuja na ombi hilo, wakati kukiwa na malalamiko ya uchache wa mabasi hayo jambo linalowafanya abiria kusubiri kwa muda mrefu vituoni.

Kwa upande wake Kafulila, amewaondoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu michakato katika kuwekeza katika mradi huo kwa kile alichoeleza kumefanywa marekebisho ya sheria katika masuala ya ubia.

Bega/sikio halizidi kichwa..🚶🚶
 
Kwanza wazawa wajue ubia maana yake waje na hela na mpango kuimarisha mradi. Sio kufikiri watapewa kama hisani. Tunaopinga wawekezaji wa nje hasa hawa wahindi na waarabu ni ujanjaujanja na kupora mali za taifa wakati kihalisia hawawekezi kitu. Wanakuja na gea za kuhonga vigogo na kisha kupora shirika au mamlaka za umma kujifanya wataendesha kwa faida. Maana ya ubia ni kuwekeza sio ujanja ujanja kama ule wa simon group. Simon group miongoni mwa mambo ya hovyo sana ni kutaka kupora UDA bila kulipa hata senti moja huku wakija na uongo eti wamelipa. Ni bora serikali yenyewe kupitia mashirika yake kuweka usimamizi thabiti jambo ambalo linawezekana kuliko kuruhusu kuporwa na wageni mashirika ya umma kama Udart au yale yenye kuendesha huduma kama viwanja vya ndege na shirika la ndege lenyewe.
 
Hivi mnaobeza wawekezaji wazawa mnafahamu hasara za wawekezaji wa nje kweli? Mliwahi kijiulizq Kwa Nini Shilling yetu Kila siku inashuka, unajua profit export na capitalflight ni kubwa kiasi gani Kwa wawekezaji wa nje.

Tuwape moyo na tuwape miradi ila tuweke mazingita wezeshi kwako iwe win win situation
 
🙋‍♂️🎯👍👌👊👏🤝🙏🗼
 
Elimu nzuri sana hii
 
Hivi mnaobeza wawekezaji wazawa mnafahamu hasara za wawekezaji wa nje kweli? Mliwahi kijiulizq Kwa Nini Shilling yetu Kila siku inashuka, unajua profit export na capitalflight ni kubwa kiasi gani Kwa wawekezaji wa nje.

Tuwape moyo na tuwape miradi ila tuweke mazingita wezeshi kwako iwe win win situation
Uko sahihi kabisa hawa watu tuwatie moyo
 
Kwa upande wake Kafulila, amewaondoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu michakato katika kuwekeza katika mradi huo kwa kile alichoeleza kumefanywa marekebisho ya sheria katika masuala ya ubia.

David Kafulila anajua fika hawa CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA) uwezo wao ni kuwa wamiliki wa lori za fuso za kubeba matenga ya nyanya kabichi, canter na matiper ya mchanga tani 7 ndiyo waweze kuingia Mwendokasi BRT si wataleta daladala aina canter, Isuzu n.k za abiria 40.

Halafu Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA) wakishindwa, David Kafulila atasema si mnaona hawana ubavu hivyo tuingie ubia na makampuni ya nje.

Kumbe kampuni serious za wenye kufanya ugavi na usafirishaji kwa kutumia Scania Volvo, Benz na brand za uhakika kwa mamia ya malori waTanzania wapo lakini wanatumia CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA) kufanya usanii kampuni za uhakika kubwa hazikupewa nafasi.
 
2024-03-15

TAMSTOA WAKUTANA NA DP WORLD, WAAMBIWA KUNA SUALA LA UWEZO, MASHARTI VIGEZO KURIDHISHA WATEJA

news-8.jpg

Chama cha wamiliki wa malori wadogo na wakati Tanzania (TAMSTOA) Siku ya ijumaa walikutana na DP World kujadili sekta ya usafiriahaji nchini.

Mpango huu uliwakutanisha viongozi wote wa Tamstoa na Chief Commercial Officer kutoka DP World ili kujadiliana mambo mbalimbali na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya uchuuzi na usafirishaji mizigo kutoka bandarini.

Mkakati ulielezea zaidi katika kuboresha miundombinu na kutoa nadharia potofu kuhusu wasafirishaji wa mizigo kutoka bandarini.

Akiuliza swali ndugu Shabani Chuki ambaye ni mwenyekiti wa Tamstoa kuhusiana na je ni kweli wasafirishaji wadogo hawatakuwa na nafasi ya kutoa mzigo bandarini? DP World kupitia bwana Aaron George alijibu kuwa kila mwenye kampuni ya usafirishaji iwe ni ndogo au kubwa basi atakuwa na uwezo wa kutoa mizigo bandarini endapo watakuwa wamesajiliwa katika mfumo.

Pia DP World wamejipanga katika kuleta huduma bora ya utoaji mizigo bandarini na pia katika utoaji hudumu kupitia mfumo wa kiteknolojia
 
TAMSTOA ni genge la njaa tupu, hawana uwezo

TOKA MAKTABA :

2023 6 November

MGOMO MZITO WA MADEREVA WA TANZANIA WALIOPO CONGO, VIONGOZI WA TAMSTOA WAJA JUU WANAOHAMASISHA WAGOME...

View: https://m.youtube.com/watch?v=hJD60Z7xVKc

Madereva wa malori wa Tanzania waliopo nchini Congo DRC wako kwenye wakati mgumu baada ya kuhamasishwa kuwafanyia mgomo mabosi wao ili wawape posho iliyotajwa na kinara wa mgomo huo kama ‘Risk Allowance’ ambayo amesema hiyo ni posho ya kimataifa ulimwengu mzima hivyo nao wanahitaji wapewe.

Akizungumza na wanahabari kwenye Hotel ya Double View iliyopo Sinza jijini, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Malori nchini (TAMSTOA), Chuki Shabani aliyekuwa na kamati ya chama hicho amesema posho hiyo inayodaiwa kuwa ya kimataifa wao hawajawahi kuisikia.

Aliendelea kusema;“Kuna mtu mmoja tunasikia anaitwa Steve ambaye tumemfuatilia na kupata mpaka namba ya hati yake ya kusafiria ndiye kinara wa kuhamsisha mgomo huo kwa kuwataka madereva wote kupaki malori waliyokabidhiwa mpaka watumiwe posho hiyo na mabosi wao.“

Jambo analofanya ni huyu jamaa ni baya sana na mbaya zaidi imesemwa kwamba kama kuna dereva ataamua kukaidi mgomo huo wamepanga kumshambulia huyo dereva na hiyo gari anayoendesha”.

Kufutia hali hiyo mwenyekiti huyo ameiomba serikali kupitia kitengo cha kuzuia uhalifu wa mitandaoni ‘Cibercrime’ kumfuatilia na kumkamata mualifu huyo anayechochea mgomo kupitia mitandaoni na kumfungulia mashitaka.

Chuki Shaban amesema wao kama walipa kodi kufuatia mgomo huo serikali inapoteza mapato mbalimbali kama vile ushuru wa bandarini, ununuzi wa mafuta na mengineyo.

Hivyo serikali tunaomba itusaidie kumdhibiti mharifu huyo anayetoka hapa nchini ambaye anayetaka kutuvuruga. Alimaliza kusema Chuki Shabani na kuungwa mkono na Makamu wake Mwenyekiti Mgendela Thobias Gama
 
Back
Top Bottom