Hatimaye wazawa wamvaa Kafulila kuendesha mradi wa UDART

Hatimaye wazawa wamvaa Kafulila kuendesha mradi wa UDART

View attachment 3159803

===
CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA), kimeonesha nia yake ya kutaka kuwekeza katika mradi wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi huku ikiomba kufupishwa kwa masuala ya michakato katika kuingia ubia huo.

Tamstoa imeonyesha nia hiyo leo Ijumaa Novemba 22,2024 walipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Tanzania, David Kafulila, ambapo pamoja na mambo mengine walitaka kujua taratibu gani za kufuata ili kufanikisha hilo.

Wafanyabishara hao wanakuja na ombi hilo, wakati kukiwa na malalamiko ya uchache wa mabasi hayo jambo linalowafanya abiria kusubiri kwa muda mrefu vituoni.

Kwa upande wake Kafulila, amewaondoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu michakato katika kuwekeza katika mradi huo kwa kile alichoeleza kumefanywa marekebisho ya sheria katika masuala ya ubia.

Wamvaa au wamuomba?
Uandishi wa ovyo huu.
 
Ufisadi ni nini?Nafikiri ifike wakati tujifunze kuhusu Biashara na tuelewe biashara ili hizi kauli za kufikiri kwamba Umaskini na Uzalendo na Utajiri ni Ufisadi tuachane nazo.

Kwanza tuelewe kwamba Kuataka Faida katika Biashara sio Ufisadi na kutaka kutajarika na kunufaika sio Ufisadi.Ni kiwango kikubw akabisa cha Uzalendo.Tunahitaji matajiri ili watengenee ajira kwa jaili ya waru.Tunahitaji matajiri ili walipe kodi za kutosha.Tunahitaji matajiri ili wachangamshe pesa katika uchumi wetu ili Pesa iweze kutembea na iweze kuwa na thamani.Tunahitaji Matajiri wazawa wazalendo.

Kisena anaweza kuwa na changamoto zake katika uendeshaji na Usimamizi na anaweza kuwa sio mtu BORA ila angekuwa FISADI kweli asingekuwa JELA,Asingeshatakiwa na wala Asingeguswa.Hii ni kwa sababu katika hali ya kawaida kabisa tunafahamu kwamba VINARA wa UFISADI ni viongozi wa kisiasa ambao kwa wanfikiri kwamba KILA tajiri anapaswa kuwagawia kidogo utajiri wao na ambao wanapenda kutumia mamlaka na nfasin zao kujineemesha pmaoja na familia ZAO.

Ifikie wakati tuache FIKRA za kimaskini kama TAIFA na tujivunie na kuwaunga mkono matajiri wazawa kwa faida za taifa letu sasa hivi na kwa miaka ijayo.Taifa letu litajengwa na sisi wenyewe.
Labda mtuambie Sasa tatizo la Kisena ni nini?
 
Tumwombee atoke itapendeza zaidi
Hili taifa letu wachawi wetu ni wanasiasa ambao wanataka wananchi wawaamini ila wao hawajiamini wa la kuwaamini wananchi wao.Wankuwa na kale ka mtazamo ka FANIKIWA lakin USIFANIKIWE KUNIZIDI.
 
Scrutiny ifanyike:
-Kuna uwezekano mipanga imeshapangwa behind the scenes hichi kinachofanyika ikawa ni danganya toto.
-Kuna uwezekano hii ikawa ni kiini macho tu kwamba anayeweka pesa ni mtu wa nje ya nchi au mwanasiasa ambaye hataki maswali ya kwamba pesa amezipata wapi.
Kama kikao chao ni sincere:
-Kuwa wafanyabiara(transporters) wamiliki wa vyombo(malori) vya usafiri ina maana wanakopesheka hivyo mtaji(cash) si lazima wawe nao bali kinahitajika wawe na clean records kwenye mabenki wakopeshwe wamwage hata mabasi 1,000 if need be.
Usafiri ukisimamiwa na private entity utaendeshwa kwa umakini bora serikali ihakikishe ina-regulate nauli kwani itakuwa ni wao(wawekezaji) literally without competitors.
Wasi wasi wa Kijinga
 
hahaha wahuni hao, Malori ya mchanga na UDART ni vitu viwili tofauti.

Pili Kuendesha mradi kuna qualification za kitaaluma siyo PESA kama wanavyodhani wao, mwishi ni wapigaji hatuwataki.

Tender itangazwe tutapata applicant wenye uwezo na uzoefu waache janja janja zao, wabaki kwenye malori yao.
 
Kwanini unawadharau hata kabla hawajaanza?
 
Kwanini unawadharau hata kabla hawajaanza?
Wadanganyika tunajuana.

KISENA alipiganiwa na Serikali yote ya CCM wakati wanampa Kampuni ya UDA, leo hao hao wanatudanganya walimshitaki baada ya kupiga mabilioni na hakufanya chochote. Ni hao hao wanazunguka mlango wa pili wamevaa nguo tofauti wanajidai ni watu wapya, wakiisha tupiga. CCM tena wanatudanganya kuwapeleka mahakamani kama kawaida yao, tukisahau wanwatoa maisha yanasonga mbele.

Muwekezaji atafutwe kwa tender, itangazwe ndani na nje, tupate muwekezaje mwenye qualification siyo hawa mnaowaita wazawa.

CCM wataiua nchi hii, halafu wanamiliki pesa na mali zisizo na uhalisia manabaki kuwasifia na kuwaabudu.
Uwazi unahitajika, kwenye miradi mikubwa kama hii, hakuna/hatutaki UPENDELEO wa aina yoyote kwa kisingizio cha UZAWA.
HAWAPASWI hata KUANZA, yani waishie kupiga picha huko huko.
 
hahaha wahuni hao, Malori ya mchanga na UDART ni vitu viwili tofauti.

Pili Kuendesha mradi kuna qualification za kitaaluma siyo PESA kama wanavyodhani wao, mwishi ni wapigaji hatuwataki.

Tender itangazwe tutapata applicant wenye uwezo na uzoefu waache janja janja zao, wabaki kwenye malori yao.
sokoine alivunja UDA na kuruhusu wazawa kuendesha huduma ya kubeba abiria mijini, tulianza na chai maharage, kwa miaka zaidi 30 hakuna mzawa hii biashara ilimtoa, hakuna maboresho yeyote, ndio kwanza huduma hii imekuwa shughuli za mateja, ni juzi wakati wa msabaha akapiga marufuku matumizi ya chai maharage na hiace vinginevyo tungekuwa bado tuna pinda mgongo kwenye hiace.

hii biashara kichaa ya wazawa nani asiyejua ni chanzo cha manyanyaso ya wanafunzi wazee na wamama, imekuwa kazi ya mateja ifike sehemu tukubali hii kazi hatuwezi,

tuache watu wenye ujuzi na weledi wafanye kazi zao.
 
Haya mambo ya WAZAWA ni Upigaji tu, hakuna lolote, kila siku tunaona wanavyotupiga na wanaondolewa bila kushitakiwa wala kutikiswa, na pesa zetu wamekula. Sitaki kusikia MZAWA watangaze tender ndani na nje tupate mtu sahihi aendeshe UDART. Walimpa Kampuni ya UDA Kisena, wakatupigia mipicha ya buses alizoleta, akala mabilioni, wakamnyang'anya mradi, wakapiga picha mbili tatu kuonyesha wanmpeleka mahakamani, watanzania tukasahau yuko wapi.

Uzawa ni deals za watu wale wale tu, wanabadili mashart wanapiga picha wanatafuta kutuibia, Wabaki huko huko.
 
Back
Top Bottom