Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Kuna ambaye siyo fisadi ndani ya CCM?Tatizo la Kisena ni Ufisadi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna ambaye siyo fisadi ndani ya CCM?Tatizo la Kisena ni Ufisadi
Wamvaa au wamuomba?View attachment 3159803
===
CHAMA Cha Wamiliki wa Malori wa Kati na Wadogo(TAMSTOA), kimeonesha nia yake ya kutaka kuwekeza katika mradi wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi huku ikiomba kufupishwa kwa masuala ya michakato katika kuingia ubia huo.
Tamstoa imeonyesha nia hiyo leo Ijumaa Novemba 22,2024 walipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Tanzania, David Kafulila, ambapo pamoja na mambo mengine walitaka kujua taratibu gani za kufuata ili kufanikisha hilo.
Wafanyabishara hao wanakuja na ombi hilo, wakati kukiwa na malalamiko ya uchache wa mabasi hayo jambo linalowafanya abiria kusubiri kwa muda mrefu vituoni.
Kwa upande wake Kafulila, amewaondoa hofu wafanyabiashara hao kuhusu michakato katika kuwekeza katika mradi huo kwa kile alichoeleza kumefanywa marekebisho ya sheria katika masuala ya ubia.
Huyu huyu 2mbili!!Nadhani wamegundua Kafulila ni kijana mzalendo ndio maana wameanza kuamini Serikali
Labda mtuambie Sasa tatizo la Kisena ni nini?Ufisadi ni nini?Nafikiri ifike wakati tujifunze kuhusu Biashara na tuelewe biashara ili hizi kauli za kufikiri kwamba Umaskini na Uzalendo na Utajiri ni Ufisadi tuachane nazo.
Kwanza tuelewe kwamba Kuataka Faida katika Biashara sio Ufisadi na kutaka kutajarika na kunufaika sio Ufisadi.Ni kiwango kikubw akabisa cha Uzalendo.Tunahitaji matajiri ili watengenee ajira kwa jaili ya waru.Tunahitaji matajiri ili walipe kodi za kutosha.Tunahitaji matajiri ili wachangamshe pesa katika uchumi wetu ili Pesa iweze kutembea na iweze kuwa na thamani.Tunahitaji Matajiri wazawa wazalendo.
Kisena anaweza kuwa na changamoto zake katika uendeshaji na Usimamizi na anaweza kuwa sio mtu BORA ila angekuwa FISADI kweli asingekuwa JELA,Asingeshatakiwa na wala Asingeguswa.Hii ni kwa sababu katika hali ya kawaida kabisa tunafahamu kwamba VINARA wa UFISADI ni viongozi wa kisiasa ambao kwa wanfikiri kwamba KILA tajiri anapaswa kuwagawia kidogo utajiri wao na ambao wanapenda kutumia mamlaka na nfasin zao kujineemesha pmaoja na familia ZAO.
Ifikie wakati tuache FIKRA za kimaskini kama TAIFA na tujivunie na kuwaunga mkono matajiri wazawa kwa faida za taifa letu sasa hivi na kwa miaka ijayo.Taifa letu litajengwa na sisi wenyewe.
Mimi nafahamu Kafulila ni mwadilifu sanaHuyu huyu 2mbili!!
Ukisikia wamvaa jua " Wamwendea kwa wingi"Wamvaa au wamuomba?
Uandishi wa ovyo huu.
Kisena alikuwa na Mipango Mizuri sana kama HiiLabda mtuambie Sasa tatizo la Kisena ni nini?
Tumwombee atoke itapendeza zaidiKisena alikuwa na Mipango Mizuri sana kama Hii
![]()
Uda eyes over Sh200bn in listing at DSE
>Dar es Salaam commuter transport company Uda, plans to raise at least Sh200 billion when it lists on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).www.thecitizen.co.tz
Hili taifa letu wachawi wetu ni wanasiasa ambao wanataka wananchi wawaamini ila wao hawajiamini wa la kuwaamini wananchi wao.Wankuwa na kale ka mtazamo ka FANIKIWA lakin USIFANIKIWE KUNIZIDI.Tumwombee atoke itapendeza zaidi
Basi utakuwa humjui 2mbili wewe, unajua kwanini anaitwa 2mbili? Au pia hilo hulijui?Mimi nafahamu Kafulila ni mwadilifu sana
Daah nchi inavituko sana hiiAisee Mtanzania haaminiki.
Watashirikiana na baadhi ya watumishi wa UDART kuchepusha mifumo ya ukataji tickets ili wapige pesa chafu huku serikali ikitiwa hasara
Wasi wasi wa KijingaScrutiny ifanyike:
-Kuna uwezekano mipanga imeshapangwa behind the scenes hichi kinachofanyika ikawa ni danganya toto.
-Kuna uwezekano hii ikawa ni kiini macho tu kwamba anayeweka pesa ni mtu wa nje ya nchi au mwanasiasa ambaye hataki maswali ya kwamba pesa amezipata wapi.
Kama kikao chao ni sincere:
-Kuwa wafanyabiara(transporters) wamiliki wa vyombo(malori) vya usafiri ina maana wanakopesheka hivyo mtaji(cash) si lazima wawe nao bali kinahitajika wawe na clean records kwenye mabenki wakopeshwe wamwage hata mabasi 1,000 if need be.
Usafiri ukisimamiwa na private entity utaendeshwa kwa umakini bora serikali ihakikishe ina-regulate nauli kwani itakuwa ni wao(wawekezaji) literally without competitors.
Na wewe ni Kafulila? Maana hapa kila mtu anaitwa KafulilaWasi wasi wa Kijinga
Uwekezaji sio jambo baya hata hivyoAdani PPP kaingia hadi kwenye Mifuko wa Bima ya Afya SHA
Ilibaki kidogo aimiliki Kenya yote 😀
Kwanini unawadharau hata kabla hawajaanza?hahaha wahuni hao, Malori ya mchanga na UDART ni vitu viwili tofauti.
Pili Kuendesha mradi kuna qualification za kitaaluma siyo PESA kama wanavyodhani wao, mwishi ni wapigaji hatuwataki.
Tender itangazwe tutapata applicant wenye uwezo na uzoefu waache janja janja zao, wabaki kwenye malori yao.
Wadanganyika tunajuana.Kwanini unawadharau hata kabla hawajaanza?
sokoine alivunja UDA na kuruhusu wazawa kuendesha huduma ya kubeba abiria mijini, tulianza na chai maharage, kwa miaka zaidi 30 hakuna mzawa hii biashara ilimtoa, hakuna maboresho yeyote, ndio kwanza huduma hii imekuwa shughuli za mateja, ni juzi wakati wa msabaha akapiga marufuku matumizi ya chai maharage na hiace vinginevyo tungekuwa bado tuna pinda mgongo kwenye hiace.hahaha wahuni hao, Malori ya mchanga na UDART ni vitu viwili tofauti.
Pili Kuendesha mradi kuna qualification za kitaaluma siyo PESA kama wanavyodhani wao, mwishi ni wapigaji hatuwataki.
Tender itangazwe tutapata applicant wenye uwezo na uzoefu waache janja janja zao, wabaki kwenye malori yao.
Haya mambo ya WAZAWA ni Upigaji tu, hakuna lolote, kila siku tunaona wanavyotupiga na wanaondolewa bila kushitakiwa wala kutikiswa, na pesa zetu wamekula. Sitaki kusikia MZAWA watangaze tender ndani na nje tupate mtu sahihi aendeshe UDART. Walimpa Kampuni ya UDA Kisena, wakatupigia mipicha ya buses alizoleta, akala mabilioni, wakamnyang'anya mradi, wakapiga picha mbili tatu kuonyesha wanmpeleka mahakamani, watanzania tukasahau yuko wapi.sokoine alivunja UDA na kuruhusu wazawa kuendesha huduma ya kubeba abiria mijini, tulianza na chai maharage, kwa miaka zaidi 30 hakuna mzawa hii biashara ilimtoa, hakuna maboresho yeyote, ndio kwanza huduma hii imekuwa shughuli za mateja, ni juzi wakati wa msabaha akapiga marufuku matumizi ya chai maharage na hiace vinginevyo tungekuwa bado tuna pinda mgongo kwenye hiace.
hii biashara kichaa ya wazawa nani asiyejua ni chanzo cha manyanyaso ya wanafunzi wazee na wamama, imekuwa kazi ya mateja ifike sehemu tukubali hii kazi hatuwezi,
tuache watu wenye ujuzi na weledi wafanye kazi zao.
Hawana pesa hao sanasana watatafuta mbia tena huko nje!Pesa wanayo ndio maana wamekwenda PPPC ngoja tuwape muda