Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Miaka yote hii tumepata nini?
Bora Manji achukue tuone atafanya nini cha kimaendeleo.
Ila miaka 10 ni mingi sana,labda kama katika mkataba wamekubaliana ujenzi wa kiwanja cha kisasa...
Otherwise angepewa miaka miwili ya majaribio.
 
Nahic yanga wanatapeliwa mchana kweupeeeeeeeee[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
Sisi kama wanachama tumetapeliwa nini? Miaka yote huko nyuma sijawahi kufaidika hata na kitu chini ya hao viongozi! Furaha/faida ya mwanachama yeyote wa klabu ni matokeo no matter timu inaendeshwa na nani! Watakao umia ni wale waliokuwa wanaishi kutegemea klabu najua watafungua sana kesi mwaka huu
 
Anaikosisha kwa sh ngp? I mean mtaji wake alioweka ni sh ngp?

Hyo asilimia 75, inathamani ya sh ngp? Isije kuwa manji anataka kuwauza yanga? Ikitokea tim ikashuka daraja je atafanyaje?

Yanga haja fikiria kwA umakini, kunahasara kuliko faida, hayo maamzi ya mwendo kasi yatakuja kuighalim yanga

Think
Mawazo mengine ya kitaahira kweli kweli, Yanga ishuke daraja imekuwa Simba?
 
Kandambili ovyo sana.. yaani klabu inakodishwa.!?
 
Wakuu,hebu nisaidieni mfano wa timu moja ya mpira iliyowahi kukodishwa ili tuseme yanga wameitumia kama kiolezo katika kufanya maamuzi yao..
 
Yanga bana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani mmekubali 75% achukue manji hahahahha
 
Am Young Dar African Sports Club,

Ila hapa naona tumeliwa mchana kweupeee, Unajua nini....?

Tunamkabidhi timu mtu for nothing..!!!, Hatujui anataka kuwekeza nini? Hatujui anataka kufanya biashara gani? Hakuna mkataba unaomfunga kwamba anatakiwa kujenga Uwanja wa Timu labda ndani ya kipindi hicho...!!!! Mkataba kwamba anatakiwa kununua angalau wachezaji wa kiwango fulani ndani ya kipindi husika hakuna...!!! Kwamba anatakiwa kuwekeza kiasi fulami kila mwaka ndani ya kipindi hicho hakuna....!!!!!!

Yaani mtu akienda huko kishumundu kutununulia kina Kibwanguso kama wachezaji wa Yanga, ni sawa tu....!!!! Hakuna cha kumbana..!!! Hapana.

Hapa tumeliwa kweupe hata jogoo hajawika!

Hii ni nafuu sana kwa watani zetu hapo ambao Mo amewaambia atawapa Bl 20. Na hata igusa hiyo wala faida yake ambayo itapatikana baada ya kukopeshwa hela hizo. Hii maana yake nini? Siku huyu mtu akiamua kuondoka Simba itakuwa imepata Bl20 na faida iliyopatikana baada ya kukopeshwa fedha hizo.

Huyu bwana ni mtu mjanja sana, Aliwekeza bure kabisa kwenye Club kwa kipindi cha karibu miaka sita sasa akilenga kupata hiki anachoomba leo, Ambacho binafsi ninaamini ni kikubwa kulinganisha na kile tutachopata kwa miaka hiyo kumi. Nembo tu ya Club inazaidi ya thamani ya trilioni moja...!!!!

Unajua nini......
Akimua kuuza maji tu yenye nembo ya club ya yanga angalau kwenye mechi moja tu ya club ya Yanga huku akifungia maji mengine kuuzwa kwenye mechi husika unajua fedha itakayopatikana? Achia mbali hilo akiamua kuuza tu Opener za soda zenye nembo ya club ya Yanga kwa miaka hiyo kumi unajua itapatikana bei gani?

Hapa sijazungumzia Jezi, Skafu, Soksi, Kofia, Miruza, Laba, Six........ Oooopssss

Ngoja niishie hapa mimi........!!!!!

BACK TANGANYIKA
kama yote haya ni rahisi (kuuza maji, opena, skafu, jezi na mafanano wake kwa nini? ndani ya miaka 70+ ya yanga haijawahi fanya ivi na kubaki kutegemea ufadhiri. wacha aichukue tu
 
Wakuu,hebu nisaidieni mfano wa timu moja ya mpira iliyowahi kukodishwa ili tuseme yanga wameitumia kama kiolezo katika kufanya maamuzi yao..
Shangazi yako aliwahi kukwambia kuwa Yanga inaendeshwa kwa mifano? Yaani tangu Jerry Muro aende likizo mna maswali ya kijingajinga kweli kweli.
 
Shangazi yako aliwahi kukwambia kuwa Yanga inaendeshwa kwa mifano? Yaani tangu Jerry Muro aende likizo mna maswali ya kijingajinga kweli kweli.
Punguza jazba mkuu,tulia..na kama hauna nilichouliza unaweza kupita tu waje wajibu wengine..
Au wewe ndio yanga??
 
Shukrani nyingi zimwendee Mr...Mo.....

amewatoa usingizi vyura....

SIMBA NGUVU....MOJA
Habari za hisa/kampuni zilianzishwa na akina Tarimba miaka kumi iliyopita .
Wamatopeni wamedesa bila kujua undani wenyewe. Mpeni Mo hiyo timu mje mlie vizuri baadaye. Mnadandia train kwa mbele.
 
Manji akizungumza hamna sauti nyingine yakukohoa,Hongera MANJI coz hamna mfanyabiashara anayetoa fedha bure.

Huu ni wakati wake wa kurudisha hasara ya mlivyokuwa mnachekelea kuingia bure uwanja wa taifa
 
Yanga buana...kama shamba la mihogo vile...unakodishwa tu
 
Back
Top Bottom