Alexprosper
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 3,286
- 6,110
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahiyo hizi kazi inabidi uwe umezisomea?
Jibu swali kijana acho kukwepaNawewe nenda mbinguni uanzishe wako.
Mbona povu kama la foma?Kuna kitu kinaitwa world view kama ulisoma level ya chuo kikuu utakuwa unakijua kama wewe ni gumbalu basi endelea na maswali yako ya kishamba.
HongeraNi vizuri kushukuru neema za Mwenyezi Mungu na kuhadithia ni Moja Kati ya njia za kushukuru ilimradi wengi nao wasikate tamaa kama mimi nimepata nilijiwekea maisha yangu niishie kulima korosho chitoholi lakini sasa nimehamasika kuingia USA kupitia uzi wake.
Mkuu nakumbuka mapambano yako humu aseeUmekomaa asee
Mimi imenichukua miaka 5 toka nia hadi kutua Canada
Cha msingi Mungu atukumbuke
Kazi zipo za kutosha, nina wiki 3 sasa, nimepata kazi 4 zote full time job. Mpaka nashangaa
Cha msingi Usije jaribu kukiuka vigezo na masharti mzee hasa ya 20hrs per week kwa mwanafunzi kufanya kazi
Jibu swali kijana acho kukwepa
Mavumbi ndio mbingu ya duniani, utasema na hiyo ni ya kusadikika utadhani ulijiumbaNenda na wewe mbinguni uanzishe Uzi wako.
Pili, sio Kila mtu anataka kwenda huko mbinguni au anaamini hizo story. Wengine mbingu zao ni hapa hapa hawasubiri mbingu za kusadikika.
Fanya vizuri kwanza ukigraduate makampuni mengi yanajitokeza kutafuta wafanyakazi nautaajiriwa kwa kile ulichosomea na kwa grades nzuri ulizopata .Hivi kwa Marekani ukitaka kubaki baada ya shule kuna process gani za Immigrarion
Mavumbi ndio mbingu ya duniani, utasema na hiyo ni ya kusadikika utadhani ulijiumba
Hiyo nchi me ilinishinda nitakuja kuleta uzi siku moja jinsi nilivyoshindwa kuishi amerika nikakimbilia CanadaAwali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kukamilisha ndoto zangu.
Pili napenda kuwashukuru wadau wakubwa humu jukwaani kwa support kubwa ya mawazo tangu nilipoweka nia ya kuondoka nchini kwetu, Mungu awabariki sana (wote mnaotambua uwepo wake na utendaji kazi wake).
Kwa kutaja baadhi, Bufa Kiranga Matola Smart911 na wengine wengi.
Hakika USA ni nchi ya ajabu sana, ni nzuri kwa namna ambayo siyo rahisi kusimulia kwa maneno, miundombinu mizuri sana kila kitu ni kizuri sana tofauti na kwetu, wameendelea sana (sidharau nasema uhalisia).
Nilianza safari yangu, kutoka Dar hadi Schiphol airport - Netherlands kwa KLM, kisha Amsterdam - JFK Airport New York kwa Delta.
Kutoka hapo, nikachua bus (42nd at Port Authority, gate 66, Greyhound, kuelekea Pittsburgh - Pennsylvania. Kutoka hapo nikabadilisha gari hadi Columbus Ohio.
Namshukuru Mungu nimefika salama, nimepokewa vizuri, nina furaha, kwa wajuzi na wenyeji huku naombeni mnipe mawazo ili iwe rahisi kwangu kupata michongo na kutimiza adhma ya moyo wangu.
Natamani kubaki huku baada ya kumaliza course yangu ya miaka 3, nitafurahi ikiwa mtanisaidia njia zaidi ndugu zangu.
Niwasisitize vijana wenzangu tupambane tu haijalishi kipindi gani tunapitia, ikiwa umeweka nia thabiti Mungu hawezi kukuacha, juhudi na maombi huleta fanaka.
Ahsante sana.View attachment 2358268View attachment 2358267
Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudiAt least wana uhakika na waendako badala ya nadharia.
Ahsante sana MkuuKila la kheri kaka. Huku bongo uje kutembea tu baki huko huko