Wala Hujanikwaza mkuu sema ni vile hujajua undani wa issue yenyewe
Kwa kifupi kuna mzigo umepotea, wenyewe wenye mzigo (Kampuni) wanadai kulikuwa na Computer ya hizi gari kubwa (Lori) pamoja na Stater,
Wale jamaa wanadai thamani ya ule mzigo wao ni milioni 10, (sasa sijui ni ya kweli au kukomoa) Binafsi kwenye akiba yangu nilikuwa na 4 milioni tu,
Kawaida issue kama hii ikitokea Kampuni huwa Ina solve then badae mnamalizana ila kwa bahati mbaya wiki mbili nyumba ilitokea msala kama huu Caryn akamalizana nao bila hata kunidai chochote, lilivyotokea na hili alichokifanya alinipa tu milioni moja, zingine nijitafute
Tatizo sio akiba tatizo ni changamoto imekuja Wakati ambao akiba yote uliyoweka umeifanyia matumizi ya kimalengo, kwa madeni niliyonayo sasa hivi hata hiyo elfu 78 naiona ni kubwa sana yani sana, nimekuja kuamini kwamba hakunaga pesa ndogo
Caryn mwenyewe hana kitu sasa hivi, Kuna maswala yake anafuatilia yamemlia pesa ndefu sana, hata hiyo milioni moja aliyonipa kafanya kumuomba Mama yake
Halafu pia watu wanaokuzunguka sio wote wanaweza kukusaidia, wale usiowategemea ndio wanakutoa kimaso maso, mf kwenye hili swala Accountant alikuwa mtu wa mwisho kumuwazia, lakini ndio amenipa milioni 1 ila kasema mambo ya kikaa swala nimrudishie nusu ya hicho kiasi (laki 5)
Kwa ufupi nikimalizana na hao jamaa (Kampuni) natakiwa nitafute milioni 3 ilipo nianze kulipa watu niliowakopa.