Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Iko hivi, nikipokea mzigo Zanzibar kuanzia hapo mzigo unakua mikononi mwangu, so nikikabidhiwa huwa nahakikisha kwenye Parking list kama mizigo yote ipo kwa kuangalia Box namba

Na huo mzigo niliuona kwakweli, kwakifupi mzigo umepotelea kati ya Zanzibar (Wakati inapandishwa kwenye meli) au Bandarini Dar (Wakati nakaguliwa),

Hadi nafika kwenye Ile Kampuni nawakabidhi mizigo yao, (kwasababu ilikuwa sio mizigo ya kwenda ofisini) kwenye ule mchakato wa kukabidhiana na kuhakiki box zote kama zipo ndipo walipogundua kama Kuna Box linamiss, huku mm nikidhani nimefikisha mizigo yote

Nilirudi hadi Zanzibar Airport but sikuambulia kitu chochote, na kama ingekuwa hilo box sikuliona pengine ningesema yule jamaa wa china kajichanganya, maana sometimes unaweza tumiwa Parking list ya mizigo yote inayokuja halafu isipakiwe yote, Sasa kama hutahakiki pale pale Wakati unakabidhiwa mzigo na watu wa Airport unaweza kuuva msala kwa uzembe, (lakini hii pia ni ngumu pia kutokea kwasababu ya Airway bill)

lakini kwa hili kuna wajanja tu watakuwa wameniotea kwasababu mzigo niliutiki
Dah Bm jamani pole sana tena sana ,, kuna namna ya ziada ya kufanya mana kama ndo hatua hizi utaingizwa hasara zaidi kwani inakulazimu ukifika tena bandarini dar uikague mizigo yote ili kama kuna ulomiss unadeal nao kabisa hapo hapo ulowakabadhi kwenye boti
 
TSH 2000/- x watu(member) 100 = 200000/- hembu tuweke hata 2000, 3000, nk.

Natuma yang u ila utupe feedback.

Ushair wangu pia baada ya hapo story uiweke kwenye WhatsApp group, kama ni Asante yako kwetu wachangiaji was tsh 78500/- tuipatie huko.

Vilwvile itawajua waliokisaidia miendelezo iwe hukohuko.
 
Tatizo vitu vyote hivi huwezi ukafanya mwenyewe, Kuna kusaidiana, sasa ikitokea shida kama hii Kila mtu anajitoa kwenye kosa mwisho wa siku mwenye dhamana ndio anawajibika
 
TSH 2000/- x watu(member) 100 = 200000/- hembu tuweke hata 2000, 3000, nk.

Natuma yang u ila utupe feedback.

Ushair wangu pia baada ya hapo story uiweke kwenye WhatsApp group, kama ni Asante yako kwetu wachangiaji was tsh 78500/- tuipatie huko.

Vilwvile itawajua waliokisaidia miendelezo iwe hukohuko.
Feedback muhimu mkuu, hadi sasa hivi nimepokea pesa ya member mmoja tu ambaye ni Mlendamboga Tsh elfu ishirini (20,000)
 
Feedback muhimu mkuu, hadi sasa hivi nimepokea pesa ya member mmoja tu ambaye ni Mlendamboga Tsh elfu ishirini (20,000)
Labda ungeanzisha thread ya kuomba msaada. Kwasababu ulishawambia watu waje hapa mei mosi, Kwahiyo kutembelea hii thread ni watu wachache sana
 
Labda ungeanzisha thread ya kuomba msaada. Kwasababu ulishawambia watu waje hapa mei mosi, Kwahiyo kutembelea hii thread ni watu wachache sana
Sio wazo baya, ila acha tu watu watakutana nayo hapa hapa
 
Labda ungeanzisha thread ya kuomba msaada. Kwasababu ulishawambia watu waje hapa mei mosi, Kwahiyo kutembelea hii thread ni watu wachache sana
Ukianzisha thread kma hii inafutwa bora aombe humu humu wenye uwezo watamsaidia
 
Wala Hujanikwaza mkuu sema ni vile hujajua undani wa issue yenyewe

Kwa kifupi kuna mzigo umepotea, wenyewe wenye mzigo (Kampuni) wanadai kulikuwa na Computer ya hizi gari kubwa (Lori) pamoja na Stater,

Wale jamaa wanadai thamani ya ule mzigo wao ni milioni 10, (sasa sijui ni ya kweli au kukomoa) Binafsi kwenye akiba yangu nilikuwa na 4 milioni tu,

Kawaida issue kama hii ikitokea Kampuni huwa Ina solve then badae mnamalizana ila kwa bahati mbaya wiki mbili nyumba ilitokea msala kama huu Caryn akamalizana nao bila hata kunidai chochote, lilivyotokea na hili alichokifanya alinipa tu milioni moja, zingine nijitafute

Tatizo sio akiba tatizo ni changamoto imekuja Wakati ambao akiba yote uliyoweka umeifanyia matumizi ya kimalengo, kwa madeni niliyonayo sasa hivi hata hiyo elfu 78 naiona ni kubwa sana yani sana, nimekuja kuamini kwamba hakunaga pesa ndogo

Caryn mwenyewe hana kitu sasa hivi, Kuna maswala yake anafuatilia yamemlia pesa ndefu sana, hata hiyo milioni moja aliyonipa kafanya kumuomba Mama yake

Halafu pia watu wanaokuzunguka sio wote wanaweza kukusaidia, wale usiowategemea ndio wanakutoa kimaso maso, mf kwenye hili swala Accountant alikuwa mtu wa mwisho kumuwazia, lakini ndio amenipa milioni 1 ila kasema mambo ya kikaa swala nimrudishie nusu ya hicho kiasi (laki 5)

Kwa ufupi nikimalizana na hao jamaa (Kampuni) natakiwa nitafute milioni 3 ilipo nianze kulipa watu niliowakopa.
Daah pole mkuu
 
Back
Top Bottom