Gramma...
Inaelekea hujui sababu za matatizo yote haya ya elimu kuanzia kuvunjwa kwa EAMWS, kufukuzwa kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, kuundwa kwa BAKWATA kuzuiwa kwa OIC kujenga Chuo Kikuu, kuzuiwa OIC kujenga Chuo Kikuu, kuzuiwa kwa Waislam kuwa na taasisi huru nje ya BAKWATA, mgogoro wa Seminari za Kiislam, kufuzwa kwa Sheikh Mohamed Ali BAKWATA, kufukuzwa kwa Sheikh Malik Tanzania, yaliyokuwa yanatendeka katika Wizara ya Elimu, kupigwa marufuku kitabu cha Hamza Njozi, NECTA na maandamano ya Waislam kupinga NECTA.
Ndugu yangu huna moja uyajuayo katika haya.
Kuna uvunjaji wa mabucha ya nguruwe na maandamano ya kwanza mwaka wa 1993 na maandamano mengine yaliyofuatia.
Matatizo ya ugaidi na mengine mengi sana.
Mimi ninachojaribu hapa ni kukuelezeni yale ambayo hamkuwa mnayajua ili myajue kwani kujua kwenu ukweli kutasaidia maelewano katika jamii.
View attachment 2867888
VIONGOZI WA NECTA TANGIA KUANZISHWA KWAKE 21/11/73
1
1973 - 1977
P. MSELEWA
MKRISTO
2
1977 – 1980
I.M KADUMA
MKRISTO
3
1980 - 1988
N. A KUHANGA
MKRISTO
4
1988 - 1992
G. R. N.MMARI (prof)
MKRISTO
5
1992 - 1999
M.L LUHANGA
MKRISTO
6
1999 – 2004
G.R.V MMARI (prof)
MKRISTO
7
2004 - 2007
E. MWAIKONDO (PROF)
MKRISTO
8
2007 - 2018
R.S MKANDALA (PROF)
MKRISTO
9
2018 – to date
W.A.L. ANANGISYE (PROF)
MKRISTO
10
SECONDARY KUTOKA (DED)
EMANUEL BARIDI
MKRISTO
11
PRIMARY KUTOKA (DED)
ESTHER THOMAS
MKRISTO
12
UALIMU NA UTAALAM KUTOKA (DED)
JOSEPH KAMILI
MKRISTO
Picha hiyo hapo juu ni moja ya mabango yaliyobebwa na waandamanaji Waislam dhidi ya dhulma ndani ya NECTA.
Maandamano haya yaliyoongozwa na Sheikh Ponda Issa Ponda 2012.
Uchunguzi ulifanywa na ukweli ukajulikana.
Wanafunzi wa Kiislamu wakapata haki yao.