Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Labda kwa kuanza tu niwasalim wote na nawaomba muwe miongoni mwa mtakaookoa nafsi yangu iliyojaa MAUMIVU YASIYO NA KIFANI

NILIANZA KUISHI NA MKE WANGU HUYU 2008 KABLA YA NDOA NA TUKABAHATIKA KUPATA WATOTO WAWILI NA MWAKA 2018 JANUARY TUKAAMUA KUBARIKI NDOA

NA KILICHOKUWA KINACHELEWESHA NDOA ILIKUWA DINI TOFAUTI MIMI NI MKRISTO YEYE NI MWISLAM ILA MWISHO ALIAMUA KUBADILI DINI MWANZONI MWA MWAKA 2009 NA TUKAWA TUNAHUDHURIA IBADA PAMOJA NA WANETU MPAKA January HII NA TUPO MKOA MMOJA LAKINI WILAYA TOFAUTI

POINT YA USHAURI HII HAPA NAOHITAJI KWENU WAUNGWANA
LEO USIKU HUU KANIAMBIA ANARUDIA IMANI YAKE KWA KINA NA ANAHUDHURIA IBADA NA MAADILI YOTE YA IMANI YAKE (Islamic) NA HAKUNA WA KUMRUDISHA NYUMA TENA

ILA PIA ANAKIRI KURUDI KWENYE IMANI YAKE HANA MAANA KWAMBA HANIPENDI ANANIPENDA NA ATAENDELEA KUNIHESHIMU KAMA MUME WAKE NA PIA HATAACHANA NA MIMI LABDA MIMI NITAKAPOAMUA KUMUACHA

NA PIA NAENDELEA KUNIAMBIA AMESHAOMBA TOBA KWA MWENYEZI MUNGU AMSAMEHE MADHAMBI YAKE YOTE ALIYOTENDA KWA KIPINDI CHOTE ALICHIMCHANGANA NABII ISSA NA MUNGU

HAKUCHOKA WALA KUISHIA HAPO ALIENDELEA KUNIAMBIA NIMSAMEHE KWA MAAMUZI HAYO NA MAISHA YAENDELEA KAMA KAWAIDA NA PIA ALIFANYA NDOA KUWEZA KUTURIDHISHA MIMI NA NDUGU ZANGU

JAPO ANASEMA JAMBO HILO ANAAMINI HALIWEZI VUNJA UHUSIANO WETU NA HATA AKIBAKI KATIKA IMANI HII ATAENDELEA KUPRETEND AMBAVYO YEYE HATAKI KUPRITEND NA NILIOGOPA KUKUAMBIA MDA ILA LEO NIMEAMUA KUKUAMBIA TU

NA HAYA YOTE YANATOKEA BAADA YA KUMPELEKA KWENYE SHULE KURISIT MTIHANI WAKE WA KIDATO 4 KATIKA SHULE ZA KISLAM

SASA NAOMBA MNISHAURI NIFANYE NINI KWA KUWA NAONA KAMA MOYO UNATOBOKA SIJAPATA USINGIZI TOKA NILIVYOJARIBU KULALA SAA 2 YA LEO

PILI KIIMANI IKOJE TENA HII NDOA BAADA YA MWENZANGU KUAMUA HIVYO

Je kuna umuhimu wa kuendelea na mipango ya maisha ya pamoja mfano tulikuwa tumenunua viwanja vitatu na kimoja nimeandika jina langu viwili majina ya watoto na pia kiwanja kimojawapo tumeshaanza ujenzi na nilipanga kumalizia nyumba yetu mwezi Wa nne je kuna umuhimu wa kufanya hivyo ??

NB SIKUWEZA KUAMINI YALIYOTOKEA KWA KUWA YEYE ALIBADILI NA KUWA MKISTO BILA KUSHAWISHIWA NA MTU YEYOTE NA KWA KWELI TULIPENDANA NA NAWAPENDA SANA YEYE NA WANANGU
kwanza binafsi nampongeza huyo mwanamke kwa huo msimamo wake kwanza aliamua kudhihirisha upendo wake kwa kubadili dini halafu akakuonyesha ukomavu wa fikra kwa kurudi kwenye dini ya haq km umempenda badili dini usilimu huwezi muache mtoto wa watu usiwe chanzo cha yeye kutoiona pepo
Km karudi kwenye dini yake nawe rudi kwenye dini yako
 
Hapo hakuna busara zaidi ya kutua mzigo tu katika Sheria ya Kiislam hakuna ndoa kama hiyo na huyo binti ajielewi tafuta mkristo mwenzio maana mkiendelea kuishi pamoja itakuwa mnazini tu

Ila ukiamua kusilimu itakuwa bora zaidi maana Sheria ya kiislam hairuhusu Mwanaume wa Kikristo kuowa Muislam lakini kinyume chake inakubalika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliitaka ndoa na akaipata. Inawezekana kuna mtu kamuahidi hata akiachika atamuoa mke wa pili. Muache ukiweza au msikilize uishi bila amani from there.
 
Kwangu, sijaona tatizo. Ulimpenda akiwa kwenye dini tofauti na wewe. Mkaungana, mkaishi vizuri. Yeye kurudia dini Yake sidhani kama ni tatizo, ila hakuonyesha msimamo tokea mwanzo.
Japo, binafsi, napenda sana wote tuwe dini moja.
 
Nakuambia amehudhuria kanisani miaka kumi na kubatizwa kabatizwa sasa nashindwa elewa na nimemwuliza uko serious akaniambia hawazi kurudi nyuma coz amepretendi mda mrefu dini ya kweli in uislam pekee hakuna nyinginee
Du! Pole. Kuwa na msimamo wa wazi toka mwanzo ni muhimu sana.
 
Kama wewe kweli ni Mkristo tafakari maneno haya kutoka 1 Kor 7 : 1-16

Maagizo kuhusu Ndoa
1Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.

2Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

3Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

4Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.

5Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

6Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.

7Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.

8Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

9Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

11lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

12Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.

13Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.

15Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.

16Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
Mstari wa 15 unaweza kumfanya jamaa aondoke.

Alichofanya huyo mwanamke ni kosa kubwa.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Nazani kwanza tuelewe ndoa ni nini kwanza tukielewa hilo nazani hayo mambo ya dini tutayaweka kando na kuweza kuoana kwa namna yeyote tunayotaka.
Ndoa ni ridhaa ya mwanamke kukubali kuolewa na mtu fulani baada ya mwanamume kuamua kutaka kuoa. Kwahiyo kitendo cha mwanamke kuridhia kuolewa hiyo ni kitendo tosha na kimekubalika kwa Mungu, hiyo ya kufunga ndoa kwa namna gani ni mbwembwe zetu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe kweli ni Mkristo tafakari maneno haya kutoka 1 Kor 7 : 1-16

Maagizo kuhusu Ndoa
1Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.

2Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

3Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

4Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.

5Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

6Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri.

7Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.

8Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

9Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

11lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

12Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.

13Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.

15Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.

16Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?
Mkuu naomba ufafanuzi mstari wa 15 kama hutoji kuhusu kuamini.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
tumeshaanza ujenzi na nilipanga kumalizia nyumba yetu mwezi Wa nne je kuna umuhimu wa kufanya hivyo ?? <<<< HAKUNA UMUHIMU WA KUMALIZIA NYUMBA LETE HIZO PESA HUKU TUNYWE BIA MAANA NAONA HUJAJITAMBUA
 
Alishawishiwa na ndoa iliyokuea mbele yake. Akafanya maamuzi kuwaridhisha. Baada ya ndoa akarudi kwenye imani yake. Huo ni msalaba wako. Hajakukataa na amesema anakupenda. Endelea na ndoa na maisha yenu. Endeleeni na biashara kama kawaida. Yeye ni mtu mzima. Kwa sheria ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kufanya maamuzi ya dini ipi aifuate. Kwa wengine ambao hamjaingia katika maisha ya ndoa nawashauri msioe au kuolewa na mtu wa dini nyingine. Si busara. Hata Mungu alikataa watu wake wasichangamane au kuoa na kuolewa na watu wengine/wageni/wasioamini/wasiomjua jehova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ni shida kwelikweli, hivi wanaonshauri wanadhani mkiwa kwenye dini moja ndio hakuna changamoto? Walio wengi tuko kwenye hizi dini “ by default “ kila mmoja anaamini alichorithi kwa wazazi. Inatakiwa kutoka kwenye hili obwe la udini na kuishi kwa kukubaliana na utofauti ambao tunao. Mungu angelitaka angetufanya tuwe na dini moja. We need to embrace diversity and be tolerant to each other. Hapo ndio tutakuwa wamoja. Mbona familia nyingi zina ndugu wakristo na waislamu, je tumeshawahi kutengana kwa ajili ya dini? Mbona tunaishi nao kwa amani kabisa na kushirikiana. Jamaa afikirie mara mbili kabla ya maamuzi.

We need more Tanzanians na Africans like you ili tuishi in harmony. I hate hizi dini zinatuchanganya akili na kubaguana wakati hazina maana yeyote kwetu. Mungu hana dini.
 
Waafrica tumekua brain washed na hz dini ili tuweze kutawaliwa nakunyonywa vzr na wakoloni ukiendekeza dini sana katika maisha haya hutaweza kuishi kabsa kila ktu utaona hakko sawa yan dini hz hz ndo chanzo cha umaskin Africa

Sent using Jamii Forums mobile app

Thank God umeona hili. Utakuta mtu kajikariria Qur'an kichwani na kuvaa maturubai juu ya kichwa huku kapaka hina ndevu zake kujifananisha na mwarab na hata kiswahili anaongea kwa kujifanya yeye ni mwarab, cha kushangaza hajuwi chochote kuhusu historia ya hiyo dini, yeye kakariri tu.
 
Pole sana mkuu, ila usipate mawazo sana, huyo kuna mtu anamdanganya tu huko mitaani, na amini usiamini leo achana naye lakini kesho atarudi kwako na machozi kibao huku anakupigia magoti
 
Hapo hakuna busara zaidi ya kutua mzigo tu katika Sheria ya Kiislam hakuna ndoa kama hiyo na huyo binti ajielewi tafuta mkristo mwenzio maana mkiendelea kuishi pamoja itakuwa mnazini tu

Ila ukiamua kusilimu itakuwa bora zaidi maana Sheria ya kiislam hairuhusu Mwanaume wa Kikristo kuowa Muislam lakini kinyume chake inakubalika

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sababu ya msingi ya mwanamke wa kiislamu kutoolewa na mwanaume mkristo, mpaka leo kuna mashehe wanapinga. Ni watu tu wamekaa na kutunga misimamo yao. Ndio maana kuna wanazuoni wanafungisha hizi ndoa mseto.
 
Back
Top Bottom