Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

kwanza binafsi nampongeza huyo mwanamke kwa huo msimamo wake kwanza aliamua kudhihirisha upendo wake kwa kubadili dini halafu akakuonyesha ukomavu wa fikra kwa kurudi kwenye dini ya haq km umempenda badili dini usilimu huwezi muache mtoto wa watu usiwe chanzo cha yeye kutoiona pepo
Km karudi kwenye dini yake nawe rudi kwenye dini yako
 
Hapo hakuna busara zaidi ya kutua mzigo tu katika Sheria ya Kiislam hakuna ndoa kama hiyo na huyo binti ajielewi tafuta mkristo mwenzio maana mkiendelea kuishi pamoja itakuwa mnazini tu

Ila ukiamua kusilimu itakuwa bora zaidi maana Sheria ya kiislam hairuhusu Mwanaume wa Kikristo kuowa Muislam lakini kinyume chake inakubalika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliitaka ndoa na akaipata. Inawezekana kuna mtu kamuahidi hata akiachika atamuoa mke wa pili. Muache ukiweza au msikilize uishi bila amani from there.
 
Kwangu, sijaona tatizo. Ulimpenda akiwa kwenye dini tofauti na wewe. Mkaungana, mkaishi vizuri. Yeye kurudia dini Yake sidhani kama ni tatizo, ila hakuonyesha msimamo tokea mwanzo.
Japo, binafsi, napenda sana wote tuwe dini moja.
 
Nakuambia amehudhuria kanisani miaka kumi na kubatizwa kabatizwa sasa nashindwa elewa na nimemwuliza uko serious akaniambia hawazi kurudi nyuma coz amepretendi mda mrefu dini ya kweli in uislam pekee hakuna nyinginee
Du! Pole. Kuwa na msimamo wa wazi toka mwanzo ni muhimu sana.
 
Mstari wa 15 unaweza kumfanya jamaa aondoke.

Alichofanya huyo mwanamke ni kosa kubwa.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Nazani kwanza tuelewe ndoa ni nini kwanza tukielewa hilo nazani hayo mambo ya dini tutayaweka kando na kuweza kuoana kwa namna yeyote tunayotaka.
Ndoa ni ridhaa ya mwanamke kukubali kuolewa na mtu fulani baada ya mwanamume kuamua kutaka kuoa. Kwahiyo kitendo cha mwanamke kuridhia kuolewa hiyo ni kitendo tosha na kimekubalika kwa Mungu, hiyo ya kufunga ndoa kwa namna gani ni mbwembwe zetu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba ufafanuzi mstari wa 15 kama hutoji kuhusu kuamini.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
tumeshaanza ujenzi na nilipanga kumalizia nyumba yetu mwezi Wa nne je kuna umuhimu wa kufanya hivyo ?? <<<< HAKUNA UMUHIMU WA KUMALIZIA NYUMBA LETE HIZO PESA HUKU TUNYWE BIA MAANA NAONA HUJAJITAMBUA
 
Alishawishiwa na ndoa iliyokuea mbele yake. Akafanya maamuzi kuwaridhisha. Baada ya ndoa akarudi kwenye imani yake. Huo ni msalaba wako. Hajakukataa na amesema anakupenda. Endelea na ndoa na maisha yenu. Endeleeni na biashara kama kawaida. Yeye ni mtu mzima. Kwa sheria ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kufanya maamuzi ya dini ipi aifuate. Kwa wengine ambao hamjaingia katika maisha ya ndoa nawashauri msioe au kuolewa na mtu wa dini nyingine. Si busara. Hata Mungu alikataa watu wake wasichangamane au kuoa na kuolewa na watu wengine/wageni/wasioamini/wasiomjua jehova

Sent using Jamii Forums mobile app
 


We need more Tanzanians na Africans like you ili tuishi in harmony. I hate hizi dini zinatuchanganya akili na kubaguana wakati hazina maana yeyote kwetu. Mungu hana dini.
 


Thank God umeona hili. Utakuta mtu kajikariria Qur'an kichwani na kuvaa maturubai juu ya kichwa huku kapaka hina ndevu zake kujifananisha na mwarab na hata kiswahili anaongea kwa kujifanya yeye ni mwarab, cha kushangaza hajuwi chochote kuhusu historia ya hiyo dini, yeye kakariri tu.
 
Pole sana mkuu, ila usipate mawazo sana, huyo kuna mtu anamdanganya tu huko mitaani, na amini usiamini leo achana naye lakini kesho atarudi kwako na machozi kibao huku anakupigia magoti
 
Hakuna sababu ya msingi ya mwanamke wa kiislamu kutoolewa na mwanaume mkristo, mpaka leo kuna mashehe wanapinga. Ni watu tu wamekaa na kutunga misimamo yao. Ndio maana kuna wanazuoni wanafungisha hizi ndoa mseto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…