Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Mie huwa nashangaa sana kuona watu wanataka kuvunja ndoa kwa tofauti ya dini hasa ukitilia maanani mke hana tatizo kwa watoto kufuata dini ya Baba yao.

BAK, Inawezekana ukaliona kuwa ni jambo dogo sana, lakini mimi najaribu fikiria jinsi ambavyo wazazi kwa sababu zenu mnawasumbua watoto, yaani wewe unakwena kanisani halafu mke anakwenda msikitini, kumbuka watoto wanatamani kuongozana na mama yao ili kufurahia malezi yao
 
N
Sijaelewa bado ndugu

DINI HAZINA MAANA YOYOTE ILE ILI MRADI TU UTENDE YALIYO MEMA NA KUWASAIDIA WENYE UHITAJI HUKU UKIMTUMAINIA MUNGU.

UKIFANYA HAYO HATA USIPOENDA KANISANI AU MSIKITINI PEPO KAMA IPO UTAIONA TU.

HILO JAMBO LISIKUSUMBUE KICHWA,ENDELEA NA UPENDO KWA MWENZAKO NA ENDELEA NA MAISHA
 
Pole kwa yaliyokukuta..Brother nnachokiona hapo mimi ni mke mwema anayelelea wanao na kukujali.. ni vizuri amekuwa muwazi kwako ili umjue zaidi.. hizi dini zimeletwa tuu.. wazungu wametuletea ukristo and waarabu wametuletea uislamu.. let her enjoy her life by loving you bila kuwa na vishinikizo .. sio lazima awe mkristo ndo ujue kwamba anakupenda and na wewe enjoy maisha kwa kupenda maisha yako.. religion is very complicated thing.. cha muhimu make sure watoto wako wako in your side ( means wawe wakristo) .. the rest ishi na mkeo kwa upendo.. miaka 10 ni mingi sana brother.. ukimuacha watoto watalelewa na nani .. mama wa kambo au utampa watoto? Why complicu things kwa issue ya dini tuu..hizi ni changamoto tuu and try kulisolve kwa kumsupport with her decision and make sure familia yako inaenjoy life.. Thats all..
 
Mkuu hatari ipo wapi hapo? Dini haina uhusiano na mwili huu, ndoa ni maungano ya kimwili tu, endelea kula mashine na lea wanao, jengeni nyumba muishi pamoja. Huyo mwanamke mzuri sana ana akili, ameona huko kwenye dini yako kuna wanafiki wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana wangu..wewe hukuoa DINI ulioa kwa kuongozwa na upendo. Kuna familia ina zaidi ya watoto kumi sasa inaishi kwa misingi ya upendo bila kuthamini IMANI zao. Mama ana IMANI tofauti na baba. Watoto wamechagua IMANI waliyoipenda hawakuzuiwa. Hizi IMANI/DINI za mapokeo zisitufarakanishe hata kkidogo. Ulimpenda MKEO sio IMANI yake mvumilie mwach aamini anachokiamini kikubwa kuwepo na nidhamu na upendo. Asante.
 
Tafadhali tafadhali sanaa nipeni mawazo yenu na uzoefu wenu
Kama unampenda muache aendelee na imani yake. Sio vzr kulazimisha mtu abadili dini. Au unaonaje ukaungana nae ukawa muislamu?
 
Nakuambia amehudhuria kanisani miaka kumi na kubatizwa kabatizwa sasa nashindwa elewa na nimemwuliza uko serious akaniambia hawazi kurudi nyuma coz amepretendi mda mrefu dini ya kweli in uislam pekee hakuna nyinginee
Ni Bora amekuambia ukweli.
 
Ulipata Raha sasa kabiliana na Karaha.
 
Mkuu,
Kama kigezo ni dini, mi sioni tatizo...

Labda kama ana marltatizo mengine ambayo yanakunyima furaha na ndoa yako....

Zaidi angalia km upo comfortable na ndoa yako, kama sivyo basi pima ukiwa haupo nae utakuwa vp....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushaur usichukulie juju juu hili suala fuatilia kwa umakini uislam unasemaje juu ya dini zingine ukiona unakufaa ingia katika dini ya ukweli na haki dini ya manabii kuanzia Baba yetu Adam mpaka nabii isa ambae ni yesu mwisho nabii Muhammad (Alw)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana hamna haja ya kuachana manake bado anaonekana anakupenda na yuko tayari kuendelea kuishi na wewe kila mtu asali kivyake.
 
Cha msingi hapo ni jinsi ya kulea watoto wenu ...na nyie kuendelea kupendana ndani ya mtindo mpya wa maisha...kumbuka dini zooote hizi zililetwa na wageni...jifikirieni nafsi zenu na za watoto wenu...
 

Ni kweli lakini kama imeshindikana kuwa dini moja na mshazaa na mnapendana unafanyaje?Utaamua kumuacha ili umtafute wa dini yako??? unafikiri kudumu kwa ndoa ni kuwa na dini zinazofanana? Nonsense and unpracticable!
 
wakati mwingine mnadhalau sana mfumo dume. hapa ilitakiwa mfumo dume ufanye kazi! hakuna kujimulia au kuvunja makubariano, marufuku ilitakiwa hapo mkuu! sema yawezekana, ulisha weka udhaifu, baby, baby nyingi, ndio maana mke anaamua kujiamulia na kupeleka familia sehemu anayo ijua yeye, wewe ni kichwa cha familia, ilitakiwa wewe ndio usimamie maswara yote katika familia, hakuna makubariano wewe ndio ukubari au ukatae! shauri yenu, hizo haki sawa, na kusikiliza kila kitu kwa wanawake ndio hayo yanatokea! kwa upande wangu, mfumo dume, unanisaidia sana, japo kuwa ni mfumo dume sahihi, mimi ndio najua familia yangu inafuata upepo upi? sio familia inamatabaka ya aina mbili, hapo tegemea watoto wakristo na wengine waislamu!
 
Cha msingi hapo ni jinsi ya kulea watoto wenu ...na nyie kuendelea kupendana ndani ya mtindo mpya wa maisha...kumbuka dini zooote hizi zililetwa na wageni...jifikirieni nafsi zenu na za watoto wenu...
Huo mtindo mpya ndo uweje boss
 
Wallah utakua Umepunguza dozi, dozi ingekua Kali kama miaka hio kabla ya kumzoea angekutubisha na kukupenda zaidi. Seems miaka Ile ilikua unapiga show za kibabe, hadi akatafuta ubatizo. Piga gemu Mwana, atarudi hewani mwenyewe, sio Dada yako huyo.
Nakuambia amehudhuria kanisani miaka kumi na kubatizwa kabatizwa sasa nashindwa elewa na nimemwuliza uko serious akaniambia hawazi kurudi nyuma coz amepretendi mda mrefu dini ya kweli in uislam pekee hakuna nyinginee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…