Hatma ya ndoa yangu leo usiku imekuwa hatari kwa maisha yangu

Kuna ndoa zipo imara huku wanandoa wakiwa dini tofauti kuliko wenyendoa wa dini moja!..usifanye maamuzi ya hovyo na ukajutia baadae....kila la kheri.
 
Salama, nakupa hongera na sio pole maana uliamua kuoa MTU wa imani tofauti nawe. Binadamu hazaliwi na dini wala imani, hivi tunavikuta duniani. We we Mkristo ukampenda mwislam na mkaishi kipagani bila ndoa na bila dini. Nasema bila dini maana hakuna dini inayoruhusu maisha ya ndoa bila ndoa. Ulianza kuisaliti imani yako nawe ukamuingiza huko. Kwasasa maisha yaendelee tu ila kama kamrudia Mungu wake inamaana ataolewa na muislam mwenziwe. Lakini kama no ibada tu na swala na ndoa inaendelea hakuna tatizo. Ushauri kwako in kuongeza Upendo kwake Mara dufu, usivunje ndoa, atatubu tena nakuirudia imani yako. Hayo in Maputo tu, kuwa mtulivu na mvumilivu,
 
Nadhani ni ubinafsi mkubwa sana kumbadilisha mtu dini/kabila/imani yake akufuate wewe kwa ajili ya kuoana, ni sawa sawa na kufuta utambulisho wake, mila na desturi. Ikiwa kama mnaweza kuishi na tofauti zenu za kidini hiyo ni bora zaidi kwa kila mtu anakuwa huru.

Fikiria umeishi maisha yote ukiwa na mwendo fulani wa maisha halafu ukubwani ubadilishe ili ku "fit-in". Nadhani sasa atakuwa huru na mwenye furaha zaidi.
 
Allah Akbar,Mwenyezi Mungu nimuweza na kwa neema zake amemrudisha mja aliepotoka.
Allah amsimamie asiyumbishwe tena kimsimamo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Soma 1kor 7:12-15
 
Soma 1 Wakoritho 7:12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kukimbilia baraza la jf, kuna wasimamizi wenu, zaidizaidi kapate ushauri toka wachungaji wako, na kama ni mkatoliki kimbia kwa paroko haraka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nichukue maamuzi gani mwuungwana nipo na hali mbaya sana hapa
Mwache aendelee na imani yake. Biblia inaruhusu. Soma 1Wakorintho sura ya saba.

12 To the rest I say this (I, not the Lord): If any brother has a wife who is not a believer and she is willing to live with him, he must not divorce her. 13 And if a woman has a husband who is not a believer and he is willing to live with her, she must not divorce him. 14 For the unbelieving husband has been sanctified through his wife, and the unbelieving wife has been sanctified through her believing husband. Otherwise your children would be unclean, but as it is, they are holy.
 
Pole mkuu ila jaribu kuchunguza kwa makini sana huko ulikokuwa umempeleka huenda amepata mwanaume wa kumrubuni mwenye kipato zaid yako na ni wadini yake so anaona ht akikwambia alivokwambia ni sawa tu.
Anaona ht ukiamua kumuacha hakuna atakachokuwa amepoteza.
Chamsingi fuatilia kwanza chanzo n nn why aamue kukwabia hayo ndo uchukue uamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isitoshe mwisho wa siku sote tunakufa hivyo fanya liwezekanalo ambalo lipo ndani ya uwezo wako. Acha kujipa stress mzee rahisisha maisha

.
 
Huo ndio ukweli kua Dini ya kweli niuislamu, muache arudi kwenye dini ya kweli na pia nawewe nakushauri uende kwenye dini ya kweli ili mfunge ndoa ya kiislamu maisha yaendelee na kama hutaki mwache aende zake atapata muislamu wakumuoa kwa sababu hakuna ndia ya mwanamke muislamu na Mwanaume mkristo, akibaki na wewe atakua anazini tu hapo na anapata dhambi kwa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Allah Akbar,Mwenyezi Mungu nimuweza na kwa neema zake amemrudisha mja aliepotoka.
Allah amsimamie asiyumbishwe tena kimsimamo


Sent from my iPhone using JamiiForums
Alikuwa ameolewa mwenzenu, hujasema kama unataka avunje ndoa yake na huyo aliyempoteza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…