Hatua kwa hatua, Jinsi ya kuiba nyama kwenye hot pot

Hatua kwa hatua, Jinsi ya kuiba nyama kwenye hot pot

watu kibao

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
466
Reaction score
1,663
01.Ingia jikoni,angalia kushoto na kulia Kama Kuna mtu anakuja

02.Angalia mkao wa mwiko / kijiko umekaaje ili mda wakuondoka uache vile vile usigeuze, usifanye kosa kizembe
😂


03. Fungua hot pot pole pole ,usiache mfuniko upige kelele au uanguke(utashtukiwa)

04.Hesabu vipande vya nyama hakikisha vipo kuanzia vitano na kuendelea maana kama vipo chini ya vitano ni rahisi kugundua vipande vilivyopungua.

Sasa ni muda wa kuchukua mnofu anza kuutafuna
👌
..lakini Kama vipande viko chini ya vitano basi chukua kimoja kimoja na kung'ata robo afu kirudishe chukua kingine fanya hivyo hivyo kwa minofu yote(unang'ata kidogo unaacha)..

05.wakati unakula ,simamisha masikio yako vzr kusikia Kama Kuna mtu anakuja(atakufuma),Sasa fungua roho nyama ishuke,usiruhusu mchuzi ukudondokee kwenye nguo au kudondoka chini,na Kama mchuzi utakudondokea wahi haraka fua nguo..na ondoa ushahidi wowote jikoni

06.Baada ya kula nawa mikono kwa sabuni na uinuse mara 6 Kama unahisi harufu Bado ipo nawa tena na tena..

07.Weka viganja kwa kuziba mdomo afu pumua kusikia Kama harufu ya nyama inatoka kinywani
🙌
Usiwe na wasi wasi kuhusu Hilo, chukua tangawizi au au limao tafuna kuondoa harufu,

08.sasa toka jikoni Kama mtakatifu,maana uko salama
🙄
🙄
🙄
😀
😀
😀
😀
😷
😷
😷
😷


Kesho ntafundisha jinsi ya kumuiba mke wa mtu.
😒
😏
 
Dah!Tunaongezewa ujuzi uzeeni.Kudokoa nyama bila kuleta rabsha.
NB:Mimi nikiamka na kusikia njaa,naenda kupakua hizo nyama tena kwa mikwara mingi hadi Maza house asikie.Ninunue mwenyewe halafu mtu anipangie kuzitafuna? Haiwezekani hiyo.
Mada hii unaaweza cheka kutwa nzima usipoangalia isee! 😆😆😆
 
Back
Top Bottom