Ni wakati muafaka sasa kwa CCM kufanya wajibu wake muhimu sana, dhidi ya wenye kiburi, waongo, wabishi na wenye tamaa waliobakiza mioyo yao ccm, lakini akili zao zikiwa kwa walio watuma.
Wakati kamati ya maadili ya bunge ikiendelea na majadiliano, kufanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha mbivu na mbichi juu ya nyaraka na vielelezo alivyo wasilisha Mh. Luhaga Mpina kwa spika, dhidi ya tuhuma anazomtuhumu waziri wa kilimo, mwenye bidii sana, mchapakazi hodari waziri Mh. Hussein Bashe.
CCM ijiandae kumchukilia Mh. Luhaga Mpina hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya kumdharau spika, kulidharau bunge, kumzushia Mh. waziri waziri Bashe kinachofanyiwa kazi na kamati ya bunge, na kuituhumu bila hakika serikali yote sikivu ya CCM kwa ujumla.
Hii si sawa kwa taasisi imara na makini kama CCM, kuendelea kuwavumilia wanachama wake wasio zingatia misingi ya nidhamu, kanuni na katiba ya chama na kukengeuka kwa chuki isiyo na sababu.
Na baada ya kumchukilia hatua za kawaida za kinidhamu kwa mujibu wa katiba ya CCM, iwe pia ni wakati muafaka chama kiende mbali zaidi, kwa kumvua uanachama wa CCM Mh. Luhaga Mpina kwa kukiuka na kwenda kinyume na kanuni, taratibu, mila, desturi na utamaduni wa CCM, wa kufanya kazi kwa kuheshimiana na kwa umoja ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Mh Luhaga Mpina abanduliwe CCM haraka iwezekanavyo kwa kutatiza mara kwa mara kupinga, na kijaribu kidhoofisha na kwa kupotosha kwa makusudi nia, mipango mikakati na malengo ya chama na serikali sikivu ya ccm katika kuwaletea wananchi maendeleo, na kuchochea mageuzi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kwenye maisha ya waTanzania wote.
Mh. Luhaga Mpina apokonywe uanachama wa CCM, ili akapate fursa na wasaa mzuri zaidi wa kuendeleza tuhuma zake na gubu binafsi alizonazo, dhidi ya baadhi ya waandamizi serikalini, ambao anahisi ndio waliosababisha na kuchochea, yeye Mh. Luhaga Mpina kutoswa kwanye baraza la mawaziri alilokua akihuduma kama waziri wa uvuvi, hapo awali.
Mh. Luhaga Mpina avuliwe uanachama ili kwa uhuru zaidi, akaungane na wenzie wa upande wa pili, wanaomtetea na waliopoteza uelekeo, walio kosa hoja, sera na wasiojua hata wana dai nini wala wanatetea nini, yaani wapo wapo tu.
Ni matumaini yangu, mpaka sasa kwa hali ilipofikia, pasina shaka yoyote, kupitia vyombo maalumu vya chama, CCM itakua imejiridhisha pasina shaka yoyote kwamba Mh. Luhaga Mpina kwa kiburi, jeuri na utovu wa nidhamu hana sifa wala vigezo tena vya kua mwananchama, mkereketwa wala shabiki wa CCM na anastahili kufubgashiwa virago vyake CCM.
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili