Hatuoni mwendelezo wa Maasai wa Ngorongoro kuhama

Hatuoni mwendelezo wa Maasai wa Ngorongoro kuhama

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Zipo kaya zaidi ya laki moja, wakazi zaidi ya 150,000, mifugo zaidi ya milioni moja, lkn tunachoona ni lori moja limebeba ng’ombe 20 na coaster 3 zimebeba wakazi wasiozidi 50, tunajiuliza mifugo yao mingine wameiacha wapi na wakazi wengine wapo njiani wanaelekea Msomera kwa miguu? haiwezekani wakazi wa vijiji zaidi ya 12 wabebwe kwenye coaster tatu tu, msafara mwingine ni lini, zoezi limestishwa au limefeli.

3AE47495-D318-4F07-99AD-43AB725FEDD7.jpeg
83A063A1-12A4-4CF8-AABA-C1F59DF2886F.jpeg


Mdau mmoja kaandika....,,

“Kwa akili ndogo tu. Unawahamisha wanainchi laki moja kuwapeleka katika kijiji ambacho kishakuwa na wakazi wake na kijiji chenyewe hakizidi kilomita 100 ya mraba halafu. Mnajenga nyumba moja mmasai ana wanawake 4+8 na watoto 20+35 sasa hapa jama tuangalie kama huu sio uonevu”?
 
Hili suala LA wamasaai naona mnapotosha sana. Acheni serikali ifanye kazi yake.....wamasaai wahame ili kupisha eneo LA hifadhi. Tusilete siasa za kikanda kwenye suala pana kama hili.
Nani kaizuia serikali kufanya kazi.
 
Gazeti la "wamachinga" linasema "wamasai" wametoa msimamo wao🐒🤸🤣
20220618_104054.jpg
 
Hili suala LA wamasaai naona mnapotosha sana. Acheni serikali ifanye kazi yake.....wamasaai wahame ili kupisha eneo LA hifadhi. Tusilete siasa za kikanda kwenye suala pana kama hili.
Mbona mtoa mada hajapinga kuhama? Kauliza zoezi linaendelea lini
 
Tatizo la wanaharakati na wapinzani ni kutafuta kiki. Ngorongoro yote itakuwa tupu na hakuna mtafanya
 
Back
Top Bottom