Wanatongozana nje ya kanisa FL1 na siyo kanisani! Sasa mtu umeshika misale ya waumini au tenzi za rohoni utatongoza vipi?
Kwa PM sijawahi! Hivi inawezekana ukamtogoza mtu ambaye hujawahi kumuona? Nauliza tu!!!
Au ndiyo unaanza kwa kujitambulisha:
"...Hi FL1, Mimi naitwa BE, nina urefu wa mita moja, nina nyumba kumi mikocheni, na magari mia moja, naishi Barbados.. Kila wikiendi huwa naenda mapumziko mafupi Newyork na Gulf Stream yangu.. hujambo? Naomba tukutane New Africa Hotel siku ya Ijumaa au Mikadi kule kigamboni, nimevutiwa sana na avatar yako mpaka nakosa usingizi usiku... Kodi hammer hapo CMC kwa ajili ya kutumia wikiendi, bill nita-settle, au ukipenda nitakutumia VISA card details kwa ajili ya shopping ndogo ndogo... Mwaaaaah See Ya - I love you honey..."[/I]
Halafu unabonyeza "Submit this message" button
Kha!