Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
- Thread starter
- #81
Japo unalenga kuvuruga mjadala muhimu wa hoja mahususi mezani, lakini sio vibaya kujadili mambo haya muhimu pia japo sio muafaka....Ndugu yangu ipo namna hii.
Serikali inayoteka nyara, kutesa na kuua raia wake haina moral authority kujichunguza kwa matukio inayoyatekeleza. Kwani nani hajui luwa Wambura ni mahiri sana kushughulikia na hata kudhuru maisha ya watu kimya kimya? Unadhani tumesahau wale watoto walioljwa wanachukuliwa na vikosi kazi vya polisi kisa panya road na wanakutwa montuary?
Mimi namfahamu Wambura kuliko mnavyojifanya kututaka tumuamini na jeshi lake.
Hapa mzee, tumeshaanza kupiga hodi vyombo vya kimataifa ili serikali hii ichunguze na kikundi chake cha kigaidi ndani ya polisi
gentleman,
binafsi ningependelea zaidi kujizuia kuzumzia jambo ambalo liko mikononi mwa vyombo vya kisheria vya kiuchunguzi na vya kiulinzi na kiusalama, kwasabb ya nafasi na wajibu mzito na muhimu sana nilio nao kwa umma na kwa maslahi mapana ya Taifa na waTanzania wote...
nakusihi sana pia kujiepusha, kua mstahimilivu na mwenye subra kuzungumzia jambo muhimu la kiuchunguzi kama hili...
nakushauri kushirikiana na vyombo husika ikiwa unazo taarifa za kutosha na za uhakika kuhusu uhalifu huo ili kurahisisha unchunguzi na wathirika wapate haki zao huku wahusika sheria zikifuata mkondo wake....
Aidha,
nikuhakikishie tu kwamba,
kamwe mambo ya ndani ya Tanzania, hayata ingiliwa na Taifa lolote la kigeni kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
hakuna jumuiya ya kikanda au hata umoja wa mataifa inaweza kuthubutu kuingilia mambo madogo madogo ya Tanzania 🐒