Ni kweli Yesu wa ndani ya Quran sio Yesu mnayemuabudu kanisani
Yesu wa ndani ya Quran ni binadamu aliyezaliwa na Mariam pia ni mtume aliyetumwa na Mungu Kwa Wana waisrael na aliwambia Wana waisrael kuwa Mungu ni mmoja tu
1) Yesu wa ndani ya Quran
Quran 5:72 -
Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
JE! WAPI YESU ALISEMA KUWA MUNGU NI MMOJA
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
And this is life eternal, that they might know thee the only true God, and Jesus Christ, whom thou hast sent.
Yohana 20:17
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
2) Yesu anayeabudiwa Kanisani hakuwahi kuwepo hapa Duniani ila ni galasa lililotengenezwa na Wazungu
Tito 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;