1. Wote wana magari
2. Wote wana majumba yenye majina ya kizungu ie contemporary house, bungalow, crib, mansion na kadhalika.
3. Magari waliyo nayo ni ya gharama kubwa, hamna mwenye vits wala IST.
4. Elimu zao ni kubwa kama nyumba zao na magari yao.
5. Wote ni maboss
6. Wote ni wafanyabiashara wakubwa.
7. Wote ni watu wa safari sana, zile safari za nje ya bara letu.
8. Wote walizipeleka familia zao vacation
9. Wote wamesoma shule nzuri za kimataifa
10. Wote walikuwa wakali sana darasani.
11. Wote wana wenza wenye hela nyingi na wazuri sana.
12. Wote familia zao ni bora sana na zina upendo wa hali ya juu sana.
13. Wote wanatumia simu kali na za juu. Techno na infinix wanawapa walinzi wao
Wote wana access na mkuu wa nchi muda wowote watakao.
Usiwaamini mtu hapa jukwaani, watu wamechoka balaa.
Watu hawana ajira, wanapost kuwa wao ndio wana uwezo wa kuajiri.
Watu hawana mitaji lakini hapa wanajiita wafanyabiashara wakubwa.
Hawana pesa ya kulipa pango la nyumba, wanaishi kama digidigi kwa kuwakimbia wenye nyumba walizopanga, lakini wakiwa hapa jukwaani wanajiita Land lord.
Kuwa macho ndugu yako