Hawa ndio wana JamiiForums niliokutana nao

Japokuwa Kwenye suala la Pesa ni kwl tunadanganyana mno ila kwakweli kwa usomi watu ni wasomi humu ndani wengi elimu yao aghalabu ni ya ngazi ya chuo....ukikuta mdada huku naye anajielewa msomi, huwezi fananisha jamii forums na Facebook au insta....Wasomi hapa wako......
 
 
Sidhani kama ni haki sana kumrushia mawe na kumsimanga Bujibuji Simba Nyamaume , katoa yake ya moyoni kwa namna alivyochambua jinsi tunavyoji-mwambafy hapa JF. Thread zetu nyngi zimejaa majigambo na majisifu, matokeo yake tunakosa hata dili kwa sababu ya kujinyanyua sana kuliko tulivyo. Na hizi pseudonyms tunazotumia humu ndio zinaficha mengi. Yanaandikwa mengi ya ukweli na uongo, ni juhudi zetu kuchagua lipi ni lipi. Binafsi natoa ushuhuda huu kwa wana JF niliokutana nao!
  1. Nimepata marafiki wazuri na wabaya. Wazuri ninaendelea nao mpaka leo na wabaya tumepotezeana.
  2. Nimefanya biashara na wana JF kadhaa kunako 2015-2022, wengine bila kuonana sura, ni kuaminiana tu, mambo yameenda vizuri sana, nawashukuru wao kwa kuniunga mkono.
  3. Kupitia majukwaa mbalimbali, nimechota ujuzi mwingi sana, hasa lile jukwaa la ujasiriamali, kuna elimu nyingi sana mle. Nimewafuata wahusika PM mara kadhaa kuomba ufafanuzi na wamenisaidia sana.
  4. Nimalizie kwa kusema kwamba sometimes tunakosa mambo mengi ya manufaa kwa kuandika mambo feki na kuweka sifa zetu feki. Kama huna kazi sema huna kazi usaidiwe, kama huna kipato sema huna kipato upewe ideas za kutengeneza kipato nk. Otherwise JF ni jukwaa la muhimu sana kwa upande wangu najifunza mengi mno.
 
Mwambie huyo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…