Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Baada ya mafunzo watarudi Tanzania kueneza ujuzi huo Kwa wenzao Kwa Kuanzisha mashamba darasa.
=====
DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Israel wameendelea na jitihada za kukuza ujuzi kwa vijana kwenye sekta ya kilimo, ambapo takribani vijana 260 wanapelekwa nchini Israel kupata mafunzo ya kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanaotarajiwa kwenda nchini Israel kuhudhuria mafunzo ya kilimo cha kisasa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Profesa Jamal Katundu amesema vijana hao watakuwa na mafunzo ya darasani lakini pia mafunzo kwa vitendo.
Amesema fursa hiyo imepatikana kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Israel ambao wamekuwa wakizungumzia suala hilo kwa ajili ya kujenga uwezo wa vijana kwenye sekta ya kilimo
Prof. Katundu amewasihi vijana hao kuitumia elimu wanayoipata nchini humo, ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuwa chachu katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Imeandaliwa na Lovin Keffa-Habari Leo
=====
My Take
Bado Rais Samia anaendelea Kuonesha dira na njia ya Vijana kupita.
Vijana msipotoka awamu hii ya Rais Samia kwenye Kilimo hamtatoboa tena.