Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Hapa bado hujaweka ''ZENGWE'' alilofanyiwa CAG,Professor Assad!
 
Umeandika kishabaki Ila hujui kilichokuwa kinaendelea na wala hujui Job Description ya DG NIMR.

Yaliyompata Dr Mwele mwendelezo wake ulikuja kwenye COVID 19. Kwa sababu zake za kishamba Mwendazake anadhani nchi ikikubali kuwa ina mlipuko wa ugonjwa fulani basi nchi hiyo itadhalilika na uchumi wake utadorora kwa sabubu watalii hawatakuja.

Kudharau kwake milipuko ya magonjwa ndiyo kumepelekea kifo chake pia ambacho amekufa kwa COVID19 hiyo hiyo.
 
Machines ziko calibrated kupima vimelea vya binadamu. Ukipeleka chembe chembe zingine ambazo siyo vimelea vya binadamu kama mapapai na oil itakupa majibu yeyote na siyo majibu sahihi.

Sawa na mashine ya kusaga mahindi, inapaswa kukupa unga. Ila ukiweka mapapai usitegemee kupata unga, Ila unaweza kupata juice au takataka
 
Huyo wa kwanza alitumbuliwa au alisimamishwa? anyway itapendeza akirudishwa kazini kama bado yupo nchini, hao wataalamu wapo wachache wanatakiwa kuwatumikia watanzania.
Na pesa zao nani alkura?
 
Kwan risasi mlizompga Lissu mlitaka akae kmya?
 

Mkuu Tanzania kuna Zica? Na ilikwenda wapi?
 
Ilikuwa siyo Ebola. Ni ugonjwa wa Usonji.Kiiglish chake sijui. Ila walipata watoto kadhaa.
Chuki ni Mwele akigombea Urais. Watu wote waliogombea 2015 aliwafanya maadui. Kumbuka Membe, January, Mwigulu, Mwele, Mwandosia n.k
Na yule mzenji Dr. Amina aliyeingia nae top 3, yaani baada ya kura za maoni mpaka leo hajulikani yupo wapi. Halafu cha kufurahisha, Mwendazake akawa anamwambia Hussein Mwinyi asiwasahau wale wenzie 11 aliochuana nao kura za maoni. Mambo ya nyani haoni kundule
 
Ilikuwa siyo Ebola. Ni ugonjwa wa Usonji.Kiiglish chake sijui. Ila walipata watoto kadhaa.
Chuki ni Mwele akigombea Urais. Watu wote waliogombea 2015 aliwafanya maadui. Kumbuka Membe, January, Mwigulu, Mwele, Mwandosia n.k

Acha uongo ilikuwa ni Zica...punguzeni uongo wana Jf
 
huyo naibu katibu mkuu huyo mwenye pua hapo chini, ambaye zamani alikuwa TGNP, nilikuwa simkubali tangu zamani sana, na nilifurahi kufumuliwa kwake. huyo wa gender aende huko akapiganie mambo ya gender, hakuwa mtu wa kufanya kazi kwenye utumishi wa umma kabisa, ni wale feminists wanaoamini wanaume ni adui zao bila kujua kwamba wao ndio wametuzaa, wengine hao ni kweli walifumuliwa kimakosa.
 
Dr Mwele aliponzwa na ukiukaji wake wa itifaki. Alipaswa kwanza kuwajulisha waajiri wake (mamlaka) kuhusu matokeo ya 'utafiti' anaoufanya.

Mamlaka ndiyo inayoyotoa hadharani matokeo rasmi, ama inatoa ruhusu kwa taasisi kutangaza, huku mazingira yakiwa yameshaandaliwa ya kukabiliana na matokeo hayo, ili kudhibiti taharuki katika jamii. Na hivyo ndiyo inavyokuwa hata kwa 'walioendelea'. Taasisi ya utafiti hazikurupuki tu kutangaza matokeo ya utafiti nyeti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…