Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Hawa ni Viongozi waliotumbuliwa na hayati Magufuli kimakosa kwa sababu za kisiasa au chuki binafsi

Hapa bado hujaweka ''ZENGWE'' alilofanyiwa CAG,Professor Assad!
 
Huu uchambuzi wako umechambua kwa kuongozwa na hisia za chuki dhidi ya Hayati JPM

Unaanzaje kusema kuwa ana chuki na familia ya Malecela ilhali baada ya kumtengua mke wa Malecela kutoka uRC baadae alimteua kuwa mbunge viti maalumu!?
Tena ubunge ndio post isiyo na stress na mshahara wake upo juu kuliko uRC

Pili, Dr Mwele alifanya kosa la kimamlaka ambalo lilipelekea yeye kuondolewa ktk hio nafasi yake. Kama alifanya uchunguzi na kubaini Zinca ipo nchini basi kimamlaka alitakiwa aliripoti hilo swala kwa mabosi zake Wizara ya Afya kisha Wizara ndio ingejua namna gani ya kuliwasilisha hilo mbele ya umma lakini badala yake yeye akakimbilia kwenda kuliripoti kwenye media,,,, akasahau kuwa yeye nae ana mabosi wake

Ni kama vile mkurugenzi usalama wa Taifa akigundua kuna hatari ya ugaidi nchini mwetu basi hakimbilii mbele ya media kuutangazia umma bali hupeleka taarifa kwa mabosi wake kwanza

Kwahyo utenguzi wake huyu DG NIMR ulikuwa sahihi kabisa
Umeandika kishabaki Ila hujui kilichokuwa kinaendelea na wala hujui Job Description ya DG NIMR.

Yaliyompata Dr Mwele mwendelezo wake ulikuja kwenye COVID 19. Kwa sababu zake za kishamba Mwendazake anadhani nchi ikikubali kuwa ina mlipuko wa ugonjwa fulani basi nchi hiyo itadhalilika na uchumi wake utadorora kwa sabubu watalii hawatakuja.

Kudharau kwake milipuko ya magonjwa ndiyo kumepelekea kifo chake pia ambacho amekufa kwa COVID19 hiyo hiyo.
 
Si kweli. Wewe ndiyo u a chukina Watanzania baada ya tubdulissu wako kukosa kurasasa kabuki na wadaiwa sugu kana sugu na wewe.

Mkurugenzi hajiamini, labda ndiyo hizi kazi za kupeana. Kware na mananasi na papai yalipimwa yakaonekana positive. Mkurugenzi mwadilifu angejieleza, au angepata statement hutoja Taasisi ya Mifugo Ukiriguru ielezw iweje kware apate covid. Vipimo hivyo hivyo vilikataliwa Italy na Ujerumani utasema hawampendi tundulissu?

Mwele ni mpumbavu. Tangu atangaze ugonjwa wa ebola, tangu afukuzwe, hajapatikana mgonjwa hata mmoja- yaani tulikuwa na mgonjwa mmoja tu wa nwele. Mwele alitumiwa na mabeberu kutetea utalii wa Kenya kwamba Serengeti kuna ebola. Hakuwa na madaraka hayo na sheria iko wazi. Hawa tukiwaacha mabeberu watangaze wanachotaka hatutabaki salama. Pale pale wakampa cheo wakamalizia rushwa waliyomwaahidi. Malecela ni shujaa wa nchi hii wala usimwingize kwenye uozo huu.

Semakafu aliteleza labda angeomba msahama. Anajua regulations yeye ndiye msimamizi wake, iweje asahau kwamba sera ilishapita? Yes, kulikuwa na uchaguzi na walimu ni taasisi nyeti, kwa nini usiwajibike kwa kupotosha?
Machines ziko calibrated kupima vimelea vya binadamu. Ukipeleka chembe chembe zingine ambazo siyo vimelea vya binadamu kama mapapai na oil itakupa majibu yeyote na siyo majibu sahihi.

Sawa na mashine ya kusaga mahindi, inapaswa kukupa unga. Ila ukiweka mapapai usitegemee kupata unga, Ila unaweza kupata juice au takataka
 
Huyo wa kwanza alitumbuliwa au alisimamishwa? anyway itapendeza akirudishwa kazini kama bado yupo nchini, hao wataalamu wapo wachache wanatakiwa kuwatumikia watanzania.
Na pesa zao nani alkura?
 
Si kweli. Wewe ndiyo u a chukina Watanzania baada ya tubdulissu wako kukosa kurasasa kabuki na wadaiwa sugu kana sugu na wewe.

Mkurugenzi hajiamini, labda ndiyo hizi kazi za kupeana. Kware na mananasi na papai yalipimwa yakaonekana positive. Mkurugenzi mwadilifu angejieleza, au angepata statement hutoja Taasisi ya Mifugo Ukiriguru ielezw iweje kware apate covid. Vipimo hivyo hivyo vilikataliwa Italy na Ujerumani utasema hawampendi tundulissu?

Mwele ni mpumbavu. Tangu atangaze ugonjwa wa ebola, tangu afukuzwe, hajapatikana mgonjwa hata mmoja- yaani tulikuwa na mgonjwa mmoja tu wa nwele. Mwele alitumiwa na mabeberu kutetea utalii wa Kenya kwamba Serengeti kuna ebola. Hakuwa na madaraka hayo na sheria iko wazi. Hawa tukiwaacha mabeberu watangaze wanachotaka hatutabaki salama. Pale pale wakampa cheo wakamalizia rushwa waliyomwaahidi. Malecela ni shujaa wa nchi hii wala usimwingize kwenye uozo huu.

Semakafu aliteleza labda angeomba msahama. Anajua regulations yeye ndiye msimamizi wake, iweje asahau kwamba sera ilishapita? Yes, kulikuwa na uchaguzi na walimu ni taasisi nyeti, kwa nini usiwajibike kwa kupotosha?
Kwan risasi mlizompga Lissu mlitaka akae kmya?
 
1. Dr. Nyambura Moremi
View attachment 1755243

Alikuwa ndiye mkurugenzi wa maabara ya taifa na fya ya jamii.

Alitumbuliwa kipindi janga la corona limepamba moto kwa kisingizio kwamba alipima sampuli ya ndege aina ya kware, mbuzi na mapapai vikakutwa na virusi vya corona.

Kimsingi, Dr Nyambura hakuwa na kosa bali alitimiza wajibu wake wa msingi kwa uweledi kulingana na taaluma yake kwa kuripoti majibu kadri ya kipimo kilivyoonyesha.

Itakumbukwa ni katika kipindi hicho hayati magufuli alitaka kuaminisha dunia kwamba nchi yetu haina ugonjwa korona kwahiyo hakuwa tayari kusikia taarifa yoyote juu ya uwepo wa ugonjwa huo. Hata hivyo baadae iligundulika vipimo vilivyotumika kupima sampuli vilikuwa na kasoro, hivyo Dr Nyambura alitumbuliwa kimakosa.

2. Dr Mwele Ntuli Malecela
View attachment 1755245

Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR).

Kipindi kumeibuka na ugonjwa usiojulikana uliohusishwa na ugonjwa wa homa ya dengue jijini Dar es Salaam, Dr mwele chini ya taasisi aliyoiongoza(NIMR) walifanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika ndipo akatangazia umma ili watu wachukue tahadhari ya kujikinga na kujilinda dhidi ya ugonjwa huo. Lakini kitendo hicho kilionekana kuwa chukizo kwa hayati magufuli akaamua kumfukuza kazi huku akimtuhumu kwamba anatumiwa na mataifa ya nje (mabeberu kama alivyopendelea kuwaita) bila ushahidi wowote wa kuthibitisha kauli yake hiyo.

Hata hivyo inasadikika kuwa kutumbuliwa kwa Dr mwele ulikuwa ni mwendelezo wa chuki binafsi ya hayati magufuli na familia ya malecela kwani hapo kabla aliwahi kumfuta kazi ya ukuu wa mkoa mama yake mwele( anne kilango malecela) kipindi cha sakata la watumishi hewa.

3. Dr Ave Maria Semakafu
View attachment 1755246

Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Alitumbuliwa kwa kosa la kutaka kuboresha elimu ambapo awali alitangaza kufuta mafunzo na ualimu wa cheti jambo ambalo Hayati Magufuli aliita ni uamuzi wa kipumbavu na baadaye akamfuta kazi.

Hata hivyo, Dkt. Semakafu alitumbuliwa kimakosa kutokana na sababu za kisiasa kwani kwa wakati huo kampeni zilikuwa zimepamba moto hivyo hayati magufuli alifikia uamuzi wa kumfukuza Dkt. Semakafu kama njia ya kujitafutia kura kwa wananchi ila suala la kuboresha elimu ni miongoni mwa sera zilizoko kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi(CCM) 2020-2025 ambayo hayati mwenyewe alizunguka kuinadi nchi nzima.

Mkuu Tanzania kuna Zica? Na ilikwenda wapi?
 
Ilikuwa siyo Ebola. Ni ugonjwa wa Usonji.Kiiglish chake sijui. Ila walipata watoto kadhaa.
Chuki ni Mwele akigombea Urais. Watu wote waliogombea 2015 aliwafanya maadui. Kumbuka Membe, January, Mwigulu, Mwele, Mwandosia n.k
Na yule mzenji Dr. Amina aliyeingia nae top 3, yaani baada ya kura za maoni mpaka leo hajulikani yupo wapi. Halafu cha kufurahisha, Mwendazake akawa anamwambia Hussein Mwinyi asiwasahau wale wenzie 11 aliochuana nao kura za maoni. Mambo ya nyani haoni kundule
 
Ilikuwa siyo Ebola. Ni ugonjwa wa Usonji.Kiiglish chake sijui. Ila walipata watoto kadhaa.
Chuki ni Mwele akigombea Urais. Watu wote waliogombea 2015 aliwafanya maadui. Kumbuka Membe, January, Mwigulu, Mwele, Mwandosia n.k

Acha uongo ilikuwa ni Zica...punguzeni uongo wana Jf
 
huyo naibu katibu mkuu huyo mwenye pua hapo chini, ambaye zamani alikuwa TGNP, nilikuwa simkubali tangu zamani sana, na nilifurahi kufumuliwa kwake. huyo wa gender aende huko akapiganie mambo ya gender, hakuwa mtu wa kufanya kazi kwenye utumishi wa umma kabisa, ni wale feminists wanaoamini wanaume ni adui zao bila kujua kwamba wao ndio wametuzaa, wengine hao ni kweli walifumuliwa kimakosa.
 
Mkuu mbona kwenye post nimeeleza in and out ilivyokuwa au umesoma kwa juu juu tu ukakimbilia kukomenti?
Nimesema by that time kulikuwa na homa iliyosaidikiwa kuwa ni dengue lakini baada ya Nimr kufanya utafiti wakagundua ni ugonjwa wa zika kumbuka dalili za ugonjwa huu na homa ya dengue zinaelekeana
Dr Mwele aliponzwa na ukiukaji wake wa itifaki. Alipaswa kwanza kuwajulisha waajiri wake (mamlaka) kuhusu matokeo ya 'utafiti' anaoufanya.

Mamlaka ndiyo inayoyotoa hadharani matokeo rasmi, ama inatoa ruhusu kwa taasisi kutangaza, huku mazingira yakiwa yameshaandaliwa ya kukabiliana na matokeo hayo, ili kudhibiti taharuki katika jamii. Na hivyo ndiyo inavyokuwa hata kwa 'walioendelea'. Taasisi ya utafiti hazikurupuki tu kutangaza matokeo ya utafiti nyeti!
 
Back
Top Bottom