Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Wakati Pele anacheza soka hakukua hata na sheria ya Offside,alikua anatupia tu kambani,

MESSI ndio mfalme wa soka hata makocha wakubwa wanatambua hilo,

Ila ruksa kwako kuamini kua Pele ndio King.
Mzee unatudanganya makusudi..sheria ya offside ipo toka 1863 huko tena ilikuwa ngumu zaidi kipindi cha kina pele, imeenda inapunguzwa makali 1990 hadi leo kina messi wameikuta ni mdebwedo. Siku hizi ili uwe onside inabidi uwe level na defense line wakati zamani ilikuwa lazima mbele yako wawepo wapinzani watatu kisha ikapunguzwa kuwa wawili.
 
Ebuuu Mleta uzi chokoza mada watu watuletee List ya Wanasayansi bora dunian, Maana nishashindwa kumlinganisha Newton na Washkaj zake wa enzi hizo.
Uzi huo upo hapa JF..Mabishano Ni makali Kati ya Einstein.. Newton na Tesla Nani mkali
 
I see..!
Waache ubishi..PELE ni zaidi
 
Mkuu mbona niliandika katika thread kuwa pamoj na ubora wake lkn kuna baadhi ya mapambano ambayo alipigwa, au haukusome thread yote vizuri?
Na pia nnachokumbuka Tyson alipigwa na Holyfield mwaka 1996. Tyson alikuwa bora na ataendelea kuwa na heshima hiyo hata baada ya kifo chake, lkn hii haiondoi ukweli kwamba Mohammad Ali ndio king haswa wa mchezo huo.
 
Tyson alikuwa vizuri kwenye kutupa ngumi, yani akikupiga ngumi lazima uhisi kitu kizito mithili ya gunia la kilo 100 kimekuangukia kichwani. Pia sifa za ukorofi na hasira za hapa na pale alikuwa nazo sana. Hii ni kutokana na maisha aliyokulia, Mike amekulia mitaani kwahiyo zile tabia bado alikuwa nazo mpaka ukubwani.

Kwa upande wa Ali yeye alikuwa mwamba wa kukwepa masumbwi. Ali alikuwa na uwezo wa kumchezesha adui yake ulingoni round nzima bila kupigwa ngumi hata 1 (kama unavyoona hapo pichan), yani anamsogezea sura adui lkn adui akirusha kombora hola. Ali akishaona adui amechoka sasa ndo anaanza kumuadhibu kwa namna anavyotaka yeye. Wengine alikuwa anawaonea hata huruma anawanyanyua baada ya kuwaangusha kwa KO.
Kuhusu tabia Ali alikuwa ni mtu mwenye kiburi, mwenye kujiamini na asiependa dharau wala kushikiwa akili na mtu yoyote. Ndo maana serikali ilichemsha kumpeleka Vietnam kupigana.
Licha ya hivyo Ali alikuwa mwenye upendo kwa watu wote bila kujali rangi zao, lkn pia alikuwa anapenda kufanya u comedy kwa watu mbali mbali.
 

Attachments

  • images (35).jpeg
    19.2 KB · Views: 11
  • images (36).jpeg
    19.8 KB · Views: 10
  • images (34).jpeg
    26.8 KB · Views: 10
Asante mkuu kwa kuweka comment bora yenye mafunzo kwa wale wasioelewa tasnia ya soka na sheria zake kwa ujumla. Huyu anamzungumzia Mesi ambae asingeweza kufanya lolote mbele ya wakongwe kina Zidane, Ronaldo de Lima, Ronaldinho nk.
Mesi angekutana na ukuta kama ule wa Robert Carlos asingeweza kupenya kwa namna yoyote ile. Enzi hizo ulitakiwa uwe na nguvu, akili, maarifa na mpira na mbio. Sasa Mesi anakimbia na mpira na kuanguka mwenyewe unafikiri angewezaje game lile.
 
Vya kale dhahabu,hata Marcelo kafanya yote aliyofanya Carlos lakini tuzo ufalme WA namba 3 ni WA Roberto carlos
Shukran mkuu, jamaa nimemfafanulia vizuri kwahiyo post ya hapo juu kabla ya hii kwamba Mesi mbele ya Carlos asingeweza kuthubutu kutia mguu. Ule ukuta wa Carlos ulikuwa ni wa chuma mkuu, Mesi asingeweza kupiga chenga hata 1.
 
Acheni unazi bila facts. Messi kaanza kucheza Barca wakati hao wote uliowataja bado wanacheza. Sijui hizo info zenu huwa mnazitoa wapi?
 
Acheni unazi bila facts. Messi kaanza kucheza Barca wakati hao wote uliowataja bado wanacheza. Sijui hizo info zenu huwa mnazitoa wapi?
Je ni kipi cha maana alichofanya wakati huo?
 
Pambano la pili 2005 . Alipomn'gata skio Holyfield
 
Well said br
 
Hapo wacko jacko, bob marley na bruce lee nimewajua nikiwa mtoto tu wengine nilikuja kuwajulia ukubwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…