Hawa NIDA kweli hawajui wafanyalo au watakalo?

Hawa NIDA kweli hawajui wafanyalo au watakalo?

Ukigoogle kama wanavyoelekeza badalala ya kuongozwa unapotezwa
Hahahahahh bongo noma
 
NIDA Tanzania kwa mfano mimi nilienda kufuatilia kitambulisho nikaambiwa utapata message kwenye simu, nikawaambia sina uhakika kama namba ya simu niliyosajilia kwenye nida kama bado niko nayo, ofisaa akaniambia we nenda utapata tu msg.
Yet wanasisitiza may mosi ndiyo mwisho kutumia namba ya nida. Mnatuchanganya wananchi. Na hapo wengine tulijiandikisha 2020 vitambulisho vimekuja mwaka jana, wengi hatupo maeneo tuoiyojiandikishia, wananchi tumevumilia miaka yooote hiyo kusubiri vitambulisho ninyi vimekuja muda mfupi tu mnasema mnavifuta, kwahiyo havina maana mtu anaweza tengeneza nida namba zaidi ya moja?
 
Ukiona wanatangaza unaweza jua wapo makini,

Warudishe ile "ONLINE COPY"
 
Hatimae imejulikana nani anatakiwa
KUFUNGA DOMO
😇😇😇🤣🤣🤣🤣

Mimi ni serikali, na serikali ni mimi

Wakijishau nitawakumbusha lakini fujo mmmmhhhh hapana
unajielewa kweli umesema wede ni serikali halafu bado unawakumbusha kina nani Sasa wakati wewe ni serikali
 
Wamesema mwisho wa matumizi ya namba may mosi, tunachakarika kuchukua vitambulisho na bado hawatupi, leo ni siku ya pili nashinda gongo la mboto kuanzia asubuhi mpaka jioni kitambulisho hakionekani

Kuna mwengine hapa anataka kumchukulia mdogo wake aliyehamia kanda ya ziwa anaambiwa hadi mwenyewe aje, hivi kweli mtu atoke kanda ya ziwa kufata kitambulisho ambacho ni haki yake na amemtuma kaka yake? Hiyo nauli mnamlipia?
Nenda kwa boss wao hapo uwashitaki
 
Inabidi NIDA wakajifunze Kwa wenzao wa UHAMIAJI wanavyofanya kazi nzuri.kuna siku nilienda kuchukua passport pale uhamiaji nilikuta watu wengi mamia Kwa mamia lakini watu wa UHAMIAJI walikuwa wanachakalika Kwa uharaka kuhakikisha watu wanapata huduma Bora.Nilihudumiwa vizuri nikapata passport yangu Kwa muda sahihi.Yule bosi anayewasimamia uhamiaji pale kurasini anastahili kupongezwa kwa kazi nzuri au ikiwezekana apewe kabisa promotion maana anajua wajibu wake.Nilitamani kama ningekuwa billionea ningempatia hata milioni miambili sema ufukara ndiyo shida
 
Oooh mpe hongera sana
 
Back
Top Bottom