Nililiongea hili wakaona naleta uchuro, watu zaidi ya laki moja kila mtu anauliza majina yanatoka lini, haijalishi ni miujiza gani itatendeka lakini lazima wapo watakaokosa na hapo ndipo utajipa stress mwaka mzima, ni bora uendelee kufanya mambo mengine hizi ajira uweke kama probability, sasa wewe mda wote upo kitandani kwa wazazi wako mbavu sikichoka unaenda sebleni kuangalia TV wageni wakija unaenda nje kukaa nyuma ya nyumba, ugali ukiiva unakuwa wa kwanza kupakua nakugombania nyama na wadogo zako, ukishiba mnanyang'anyana remote ya TV na watoto sebleni, jua likizama unaweka sijui HUBA mara series za kihindi, ukichoka unaenda kujibwaga kitandani. Huchangamani na wenzako, kucha kutwa upo jamiiforum na kibando cha kuiba Mia tano ukitumwa sokoni unakata ya vocha mwisho wa siku umetumwa nyanya za Mia tano unaenda kuchukua za Mia nne, vitunguu vya Mia tatu wew unanunua vya 200, mafuta ya buku wewe unaomba upimiwe ya 800 ili upate jero ya vocha uweke bando uje utusumbue na vimeseji vyako vya kipumbavu mara mambo vp, maraa umepotea, mara nambie, mara sijui uko wapi nije, mara sisi Tupo, yani unakuwa kama tahila. Vijana tafuteni kazi hata yakumwagilia mboga za majani huwezi Kosa buku teni faida kwa siku, nchi yoyote Ile Dunia serikali huwa haiajiri mda wote, inaajiri kulingana na uhitaji wao kazi yao kubwa ni kutengeneza mazingira rafiki kwa sekta binafsi kufanya uwekezaji na hawa ndio wanaoajiri kwa viwango vikubwa kitu ambacho serikali imeshindwa kushawishi wawekezaji na ndio maana ajira zimekuwa ngumu.