Hawa vijana ambao walikuwa "Team Mbowe" kwa kweli wanahuzunisha

Hawa vijana ambao walikuwa "Team Mbowe" kwa kweli wanahuzunisha

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Nawazungumzia watu kama Godlisten Malisa ambaye ajira yake ya kwanza aliipata ndani ya ofisi ya KUB baada ya Chadema kushinda kura nyingi na kuwa chama kikuu cha upinzani kwa mara ya kwanza. Anasahau kuwa fadhila hazikutoka kwa Mbowe bali zilitoka kwetu sisi tulioipigia kura Chadema na tukaondoka kuendelea na majukumu mengine huku Malisa akifaidi matunda. Leo Lissu amekuwa mwenyekiti anajifanya haioni tena Chadema. Huo ni utovu mkubwa wa nidhamu.

Kina Yericko, Kileo, Mrema ambao walifaidi matunda ya Chadema baada ya sisi kujitoa kupiga kura kwa chama hatimaye wakapata ajira makao makuu ya chama. Leo Lissu yupo wanatamani ashindwe. Huo ni uhuni. Tulishasema Lissu alihitajika zaidi kuliko Mbowe zama hizi na tulimchagua kwa ajili hiyo. Tumeendelea kumpa support yetu kwa gharama zetu. Vipi nyie wenzetu? Mnadhani ruzuku ilitokana Mbowe bila sisi?

Kina Boniface Jacob, Asenga ambao wamekuwa viongozi baada ya sisi kujitoa kwa hali na mali kuitetea Chadema kwenye chaguzi mbalimbali. Nao wanajifanya hawana habari kabisa.

Kiukweli mnajichoresha na mnazidi kuonekana kwenye jamii nyie ni watu wa aina gani. Malisa usisahau una foundation yako ambayo sisi ndiyo wadau wakubwa. Itafika mahali tutakukataa.
 
FB_IMG_17389459365742792.jpg
Tuwape hii kitu wanyonye pumbavu zao....ndio walikuwa wanatuchelewesha kwenye safari ya mabadiliko
 
Wacheni wapone maumivu.

Siku zote mtu hawezi pona kwa siku Moja.
 
Kwamba kuna watu tayari ndani ya CDM wameshaanza kumfanyia Lisu sabotage kuhakikisha kwamba anashindwa au?
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Back
Top Bottom