Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Hivi ni ujinga [kwa maana halisi ya neno ‘ujinga’]?
Uoga?
Kuwa na ajenda ya siri?
Kuwekewa masharti ya mahojiano?
Kutokujiandaa kikamilifu?
Au ni nini hasa?
Nimeyaangalia mazungumzo ya Tundu Lissu na Clouds Media 360.
Moja ya maswali ambayo nilitegemea wangemuuliza, hawakumuuliza.
Ni swali kuhusu uzushi ambao aliusema wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Straight Talk Africa, kinachorushwa na Voice of America.
Lissu alizusha kuwa mmoja wa walinzi wa Rais Magufuli naye alikufa kwa corona, kama alivyokufa Magufuli, kwa mujibu wake [yeye Lissu].
Akatoa kabisa na maelezo ya kimuonekano ya huyo mlinzi.
Kwa mtu yeyote mwenye hata chembe ya akili kidogo tu, angejua Lissu alikuwa anamzungumzia nani.
Niliwahi kuandika kuhusu huo uzushi wake hapo kitambo kidogo.
www.jamiiforums.com
Katika kumbukumbu zangu zote, sijawahi kuona popote pale ambapo Lissu aliulizwa kuhusu huo uzushi.
Na nasema ni uzushi kwa sababu huyo jamaa aliyedaiwa kufa, hakuwa amekufa. Alishiriki kikamilifu hadi mwisho wa mazishi ya Magufuli.
Kwa nini waandishi wa Tanzania hawamuulizi maswali kama hayo yanayohusu hizo kauli zake tatanishi?

Tundu Lissu amzushia kifo mlinzi huyu wa Rais Magufuli?
Nami nimeyatazama mahojiano ya Tundu Lissu na Shaka Ssali kwenye kipindi cha Straight Talk Africa kirushwacho na runinga ya Voice of America. Bw. Lissu kaongea mambo mengi. Na kama kawaida yake kila apatapo wasaa au fursa ya kufanya hivyo, kwenye mahojiano haya na Shaka, katema nyongo yake...