Uchaguzi 2020 Hawa wakienda kupiga kura Oktoba 28, CCM hatuna chetu!

Uchaguzi 2020 Hawa wakienda kupiga kura Oktoba 28, CCM hatuna chetu!

Kwa ngazi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Kama chama tawala kinachoomba ridhaa ya miaka mitano mingine, tukeshe tukiomba kuwa hawa wafuatao wasiende kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu. Wakienda na wakipiga kura, CCM hatutakuwa na chetu. Watapiga kura za uchungu na kuukataa uchungu zaidi. Zitakuwa kura za kuponya mioyo yao kwakuwa watakuwa wametoa maumivu yao kupitia kukataa.

Hawa wakienda kupiga kura, CCM lazima ije na mbinu mbadala kuliko daladala. Wataikataa CCM na wagombea wake mchana peupe. Wataikataa CCM na wagombea wake kwa kutumia kadi zao za kupigia kura, kwenda kwao kupiga kura. CCM itakataliwa kwa maumivu yaliyotokana na matendo na maneno ya Serikali iliyoundwa nao. Nawataja wa uchache watu hao ambao kama CCM tunapaswa kukesha tukiomba wasiende kupiga kura.

Waliobomolewa nyumba na biashara zao bila kulipwa fidia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofukuzwa kazi kwa sakata la vyeti bila kupewa hata sumni pamoja na kufanya kazi kwa miongo kadhaa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliopatwa na majanga ya asili bila kupata msaada wa kiserikali pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofungiwa biashara na shughuli zao za kiuchumi kwa njia za kibabe pamoja na wategemezi wao.

Na wote ambao wameoisoma namba kwa namna moja au nyingine!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)

Hizo ni KURA TOSHA KABISA za kuhitimisha Utawala Dhalimu wa CCM ya Dikteta Pombe ya Magufulication......!!!
 
Ukitaka kujua nan anashinda huu uchaguzi ni simple sana! mskilize mgombea mwenyewe kwa makini utajua nan anashinda


We are in 2020 General election, wewe unaleta mambo ya Lowassa wa 2015?

You are joking, right ?

Hata kama hutanii, Edward Lowassa in 2015 won the election massively in the BALLOT BOX....

Changamoto kubwa ya uchaguzi kama tulio nao hapa Tanzania ni KUSHINDA katika sanduku la kura na KUTANGAZWA....

If they do their home well to solve this problem, there's no doubt that the opposition will massively win this year's election....!!
 
We mzee kumbe unafanana sana matendo na nyumbu

Ok wapigakura ni ml28 je ukijumlisha hao wote unapata ngapi? ukitaka +na wafanyakazi wa serikali
wanachama wa ccm pekee wanatosha kumrudisha JPM madarakani
nyie endeleeni kupiga ramli tuu 😁😁😁
CCM wenyewe hawamtaki kwa vile ameinyang'anya CCM kutoka mikononi mwao na kuweka kwa watu wake wachache
 
Nyie mnaota!!
Waliobomolewa ni ngapi ya watanzania wote
Waliosoma NAMBA ni ngapi ya watanzani wote
Jobless ni wangapi ya watanzania wote
Ushindi WA CCM mwaka huu itakua ni Sawa na daladala za Mbagala Anashuka Mmoja Wana panda 5,
Tathiminj tunazo tayari Wana CCM!!
Na mwaka huu Goli la mkono hatutumii
Ushindi Upo palepale
 
We are in 2020 General election, wewe unaleta mambo ya Lowassa wa 2015?

You are joking, right ?

Hata kama hutanii, Edward Lowassa in 2015 won the election massively in the BALLOT BOX....

Changamoto kubwa ya uchaguzi kama tulio nao hapa Tanzania ni KUSHINDA katika sanduku la kura na KUTANGAZWA....

If they do their home well to solve this problem, there's no doubt that the opposition will massively win this year's election....!!

are you done assuming? hakuna chama tanzania hii kinaweza kuitoa ccm madarakani hata vyama vyote vikiungana
 
Watu wanapenda kutumia msemo wa "kuona mbali" kama kigezo cha kutetea kile wanacho kiamini au kuona ni sahihi kwa mtazamo wao.

(Huko mbali hivi huwa ni wapi?)
 
Ongezea basi na wanaodai mafao yao na hawalipwi hata kama wamefikisha miaka sitini.
Wanaodai mafao yao na hawalipwi kwa wakti,miezi na miezi wanasubiri utafikiri wanasubiri mkopo kumbe ni hela zao.
Walionunua drones ili wajiongeze na kujiajiri lakini leo wanatakiwa kusajili zaidi ya laki mbili kila mkoa.
Walioaanzisha blogspot na kulazimishwa kuzisajili utafikiri wameajiri kampuni ya mtaji wa bilioni Ishirini.
Napenda sana kufanya utani hasa niapokuwa nimevuta kile kitu chetu cha CHUGA a.k.a CHUGANISTANI
 
Ndiyo maana namomba Lisu akazie sana watu hapo juu uliowataja, hawa kila mmoja angalau awavute watu 10 wa kumpigia kura Lisu, basi kama ulivyosema mchezo umekwisha!
Unadhani ni kaxi rahisi kuwapata hao 10 wa uhakika?
 
Back
Top Bottom