Cha kushangaza hapa siwasikii wajaluo, wamasai, na watu wa kusini. Kwanini always Kigoma na Kagera. Kuna Siri gani. Kwanini mnawaogopa the so called wahamiaji haramu wa mkoa wa kigoma na Kagera na si wa mara, Arusha, Ruvuma au Mtwara.
Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi tu wanmesoma hadi shule kenya, wana ndugu zao kenya na Tanzania, ila hawana shida. ukienda Mtwara, wamakonde na wayao wapo pande zote mbili za msumbiji na Tanzania, ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na wazambia na wamalawi,wameoleana mno, in fact wafanyabiashara wazuri wengi wa Lusaka kwa wale waliofika kule, ni wakinga na wanyakusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule zambia. ukienda kwa ndugu zangu wachagga, na wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili, kama wameru ndio hadi kenya kuna eneo na kabila la wameru, ukienda Tanga ndio usiseme wanaingiliana na makabila, hivyo ukienda kigoma, bukoba na Rukwa, usishangae kuona kuna wanyarwanda, warundi na wacongo wengi tu ila ni watanzania. mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote.shida nadhani ni PK na sio makabila ya nchi hizo, watu hawampendi PK, kitu ambacho hata mimi huwa simkubali kabisa kabisa kwa ukatili wake. asingekuwepo PK hao wote wangeishi bongo kwa amani tu na suala hili lisingejitokeza.
hata hivyo, serikali ina mkono mrefu, kama wapo wanaoishi hapa kiitellijensia hao hawana nia nzuri, serikali ikamate mmoja mmoja kimya kimya uone kama wote wenye nia mbaya hawajakimbia kimya kimya. wataambizana kwamba mwenzetu kakamatwa na watasepa, ila wale wema hawana haja ya kufukuzwa. wengine ni wake za watu na waume za watu wanaprovide kwa dada zenu hapahapa tz.