Mimi ni mtanzania halisi, vizazi na vizazi. lakini wakati mwingine ninaamini hii dunia sio ya mtu mmoja, ni ya wote, hata Tanzania sio ya kwako peke yako ni ya wote, ni wakoloni tu walitutenganisha hasa sisi waafrika. sasa mtu kama mkimbizi aliyekimbia Rwanda au Burundi miaka ya 60, amekuja hapa akiwa mtu mzima, amezaa watoto, na watoto wamezaa watoto. wamesoma hapa, wamekulia kila kitu hapa, hawajui kwengine kwa kwenda ila hapa, mnataka waende wapi? warudi Rwanda, Burundi au Congo ambako hawajawahi hata kufika na hata wakienda wanafikia hotelini? wangekuwa wanawajua ndugu zao huko labda, au kama wanazipenda hizo nchi labda, ila huko kwenye asili yao hawakujui, hawajawahi kwenda, wengine hata baba zao hawajawahi kwenda, mnataka wafanye nini? wamekua wakijua hapa ndio kwao hawana kwao kwengine wanakokujua, na wamepapenda.
watusi kwa mfano, walianza kukimbilia Tanzania hata kabla ya uhuru kwenye first Hutu Revolution ya mwaka 1952 ambapo wahutu wali rise up against tutsi ambao ndio walikuwa kabila la kifalme Rwanda, kwasababu hiyo watusi wengi sana walikimbilia congo (ndio wale banyamulenge), na wengi walikimbilia Tanzania. ukienda mikoa kama ya kigoma, Tabora, Mwanza hadi Rukwa, kuna watu wenye sura za kitusi kabisa ila babu zao walikuja hapa kabla ya uhuru wa Tanzania, na wameishi wakibaguliwa tangu miaka hiyo hadi leo. mnataka waende wapi? nchi yenyewe hii ya Tanzania mnaishi mnakufa na kuiacha hapahapa, mtu kama haleti madhara, mwacheni. Kina Obama hao mbona baba zao ni wakenya ila wamekuwa marais wa Marekani? mnachotakiwa kufanya ni kuweka vizuri mifumo ya intelijensia ili mtu awe na asili ya moja kwa moja ya hapa Tanzania au la, asilete madhara, kwasababu hakuna guarantee kwamba hao mnaowaona kama ni asili ya wakimbizi ndio wataidhuru nchi, kuna uwezekano threat kubwa ikatoka miongoni mwetu sisi wenyewe tunaojiita wazalendo. dunia hii mmeikuta na mtaiacha, hamjaiumba kwanza ni mali ya Mungu hapa ametuweka kama mifugo tu tuishi, achaeni ubinafsi na ubaguzi.