Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nilichojifunza baada ya kutembea nchi kadhaa hasa za watu wenye uelewa wa dunia, katika maisha unachotakiwa kujali ni namna gani unaingiza kipato chako na usalama wa familia yako na nchi yako tu, otherwise, unaweza kuishi popote na ukapaita nyumbani. ndio maana nashauri serikali iweke vizuri intelijensia yake ili kukamata waovu na wanaochunguza nchi, ila si kufukuza wageni. mgeni akiwa hapa kama hana matatizo, pesa yake ataspend hapa, though cha muhimu ajulikane yupo ili apewe masharti ya kuishi.
 
Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi tu wanmesoma hadi shule kenya, wana ndugu zao kenya na Tanzania, ila hawana shida. ukienda Mtwara, wamakonde na wayao wapo pande zote mbili za msumbiji na Tanzania, ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na wazambia na wamalawi,wameoleana mno, in fact wafanyabiashara wazuri wengi wa Lusaka kwa wale waliofika kule, ni wakinga na wanyakusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule zambia. ukienda kwa ndugu zangu wachagga, na wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili, kama wameru ndio hadi kenya kuna eneo na kabila la wameru, ukienda Tanga ndio usiseme wanaingiliana na makabila, hivyo ukienda kigoma, bukoba na Rukwa, usishangae kuona kuna wanyarwanda, warundi na wacongo wengi tu ila ni watanzania. mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote.shida nadhani ni PK na sio makabila ya nchi hizo, watu hawampendi PK, kitu ambacho hata mimi huwa simkubali kabisa kabisa kwa ukatili wake. asingekuwepo PK hao wote wangeishi bongo kwa amani tu na suala hili lisingejitokeza.

hata hivyo, serikali ina mkono mrefu, kama wapo wanaoishi hapa kiitellijensia hao hawana nia nzuri, serikali ikamate mmoja mmoja kimya kimya uone kama wote wenye nia mbaya hawajakimbia kimya kimya. wataambizana kwamba mwenzetu kakamatwa na watasepa, ila wale wema hawana haja ya kufukuzwa. wengine ni wake za watu na waume za watu wanaprovide kwa dada zenu hapahapa tz.
Hata mm naamini tz sio shida jamii yoyote kuwa hapo tatzo na tishio ni wale watu wa pua ndefu tu kutoka kigali
 
Mkunda jina la kinyamwezi,maana yake mburuzo uwe wa nyoka,mkia au chochote kile
hao wengi sana wapo Tabora, Shinyanga, na Katavi. na wengine wana sura za kitusi, wanaongea kirundi, na wanaitwa watanzania wa kabila la kihutu. nilishangaa sana nilipofika kuile. ila ni watanzania na wana haki zote na hawajawahi kuleta madhara yeyote.
 
Obviously itakuwa ni wasonjo ,maana unakuta baadhi ya maeneo sababu ya kuhonga fedha baadhi ya wakuu wa idara za serikali wanatunukiwa na nafasi za kioungozi katika ngazi za kijamii au vyama vya siasa more especially green party.
 
chief, hao wa Tabora, usije kuconnect dots na kamanda wa kinyamwezi. Tabora kama sikosei kuna wale wa Ulyakuru (nawakumbuka kwa kanda yao ya dini ya "katika viumbe vyote vilivyoumbwa binadamu kaumbika kuliko vyote"), hawa walijulikana kama wakimbizi na walikuja kabla hata ya ukoloni au soon after independence, more than 150k walipewaga uraia na sio wakimbizi kwasababu walizaliwa hapahapa na wamekulia hapa na wamezaa watoto walozaa wajukuu hapahapa.
 
Kuna wazee wengi walikujaga
Na wakafikia na walikaa sana kwenye kambi ya Nyarugusu wamezaa mitoto

Na watoto wamekulia hapo na wakatoka hapo wengine wafanyabiashara, wanasiasa nk

Ova

TZ lishakuwa shamba la bibi, kila mtu anajikatia pande.

Sasa sijui hiyo vetting wanaifanyia wapi?
Halafu, kambi ya wakimbizi si inakuwa na wawakilishi wa wizara ya mambo ya ndani ambaye ndiye mkuu wa kambi na wasaidizi wake, inakuwaje wanashindwa kudhibitiwa?
 
Wapo ambao wameoa na kuolewa na wamejipenyeza mpaka ndani kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna yanki alikuja majuzi na Rais wa Ujerumani, yule jamaa ni waziri kule ila asili yake ni Tz , Uingereza kulikuwepo hadi waziri mkuu mponjolo kule America Obama aliongoza Taifa, huyo Mkimbizi ni nani? Wabongo waachage ubaguzi
 
Back
Top Bottom