Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Asalaam aleykum wana Jf.
Leo Mkuu wa Majeshi, General Mkunda amegusia kuwa kuna baadhi ya wakimbizi wameshikilia nafasi nyeti serikalini kulingana na taarifa za kiintelijensia.
Sasa lengo la uzi huu ni kuwarahisishia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili kuwabaini wakimbizi wote ambao wameteuliwa kwenye nafasi za maamuzi.

Hii itasaidia kudumisha ulinzi na usalama wa Taifa letu kwani ni hatari sana kukabidhi nafasi nyeti kwa wageni/wakimbizi kwa sababu kuna wale ambao hata kama wameishi miaka 1000 sehemu nyingine, huendelea kuwa wazalendo kwa Taifa lao la asili. Mfano hai ni Mh. PK, Rais wa nchi mojawapo jirani, ambaye ni kama tu alizaliwa na kukulia Uganda, lakini bado kilichotokea wote tunakifahamu.

Kwa wasiofahamu tu ni kwamba huyu Mh. PK alishikilia nafasi nyeti sana katika nchi ya Uganda ikiwemo Mkuu wa kitengo cha Intelijensia Jeshini, lakini bado tu roho yake na akili yake ilikuwa katika nchi yake ya asili!

Chonde chonde kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, siyo kwamba hawa watu hawajulikani, wanafahamika vyema ila kwa sababu ya rushwa na mambo mengine, basi kunakuwa na ile hali ya kufumbia macho.

Naomba kuwasilisha.

View attachment 2879699

Marehemu ndio kapenyeza wote hao
 
Kuna mtu alikuwa ni mfungwa akatumikia kifungo jela kikaisha eti na yeye leo ni Askari kwenye moja ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tena hivi vikubwa vikubwa . Aibu hii [emoji706]
Tishio kubwa kwa Nchi hii ni CCM.
 
Tulitoa taarifa uhamiaji tena kwa viongozi wakubwa wenye dhamana ya uwwpo wa wahamiaji haramu na mahali walipo, wakatoa gari tukawapeleka kwenye hizo nyumba hakuna hatua yeyote walio chukua, tunahofia usalama wetu maana wale wahamiaji wameshatujua, mwingine alipigwa PI kipindi mwigulu akiwa waziri na Sasa yupo nchini tumetoa taarifa uhamiaji wakatucheka.

Kuna mengi yaaaani ........
 
Kuna yanki alikuja majuzi na Rais wa Ujerumani, yule jamaa ni waziri kule ila asili yake ni Tz , Uingereza kulikuwepo hadi waziri mkuu mponjolo kule America Obama aliongoza Taifa, huyo Mkimbizi ni nani? Wabongo waachage ubaguzi
Hata kama huyo mkimbizi kateuliwa na anafanya kazi yake vema kwanini asipewe uraia ili atamblike kisheria kama anatufaa? Kwanini mkimbizi abaguliwe? Mkimbizi sio mtu? Watoto wa lema waliokimbilia canada hawastahili teuzi kisa wamezaliwa bongo?
 
Kuna wazee wengi walikujaga
Na wakafikia na walikaa sana kwenye kambi ya Nyarugusu wamezaa mitoto

Na watoto wamekulia hapo na wakatoka hapo wengine wafanyabiashara, wanasiasa nk

Ova
NYARUGUSU ipi hiyo mkuu?
maana ninavyojuwa Bukoba kuna nyarugusu na mkoa wa Geita pia kuna kijiji kinaitwa nyarugusu.
 
Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi Gen Jacob John Mkunda amemueleza Rais kuwa Kuna wakimbizi wapo Hadi Serikalini na wamepewa nafsi za juu kabisa za kimaamuzi

Hili inashangza na kufikirisha Sana inakuwaje Hadi mkuu wa majeshi anawajua wakimbizi na wameteuliwa na wala hajawasiliana na mamlaka za uteuzi kuzuia uteuzi wao yeye amekaa kimya Hadi leo ndio Kuja kumueleza Rais by suprise.

Mimi najiuliza hivi Rais leo atapata usingizi Kweli? Atakuwa anajiuliza ni Nani huyu nimemteua ambae Ni mkimbizi?

Lazima Rais atapitia mafail yake kwa upya mnk kwa taarifa ya leo wa kamanda wake CDF kusema wasiwasi kuwa unawateua hadi wakimbizi inamaana kwamba wasaidizi wake wanamuingiza Chaka.

Anyway Kama Kuna kiongozi au afsa tunamuhisi siyo mtanzania mwenzetu Basi tumtaje hapa hajui kuwa siyo mwenzetu.

- Mtikila: Kagame amepenyeza Wanyarwanda 35,000 Tanzania, Burigi, katika Wilaya ya Muleba

Pitieni huu uzi

huu ni mtego 2025 kuna mtu anatafutwa.
 
Tulitoa taarifa uhamiaji tena kwa viongozi wakubwa wenye dhamana ya uwwpo wa wahamiaji haramu na mahali walipo, wakatoa gari tukawapeleka kwenye hizo nyumba hakuna hatua yeyote walio chukua, tunahofia usalama wetu maana wale wahamiaji wameshatujua, mwingine alipigwa PI kipindi mwigulu akiwa waziri na Sasa yupo nchini tumetoa taarifa uhamiaji wakatucheka.

Kuna mengi yaaaani ........
Ni wapi huko mkuu?

Unaweza kuelezea kwa urefu kidogo?
 
Back
Top Bottom