Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umenena vyema ila kiukweli hao Burundi, DRC na Rwanda wana roho mbaya. Hakuna nchi watakayoenda wasisumbuliwe. Hapo Zambia wananyanyasika sana wakati kuna watanzania wengi hata vibali hawana lakini wanaishi fresh bila usumbufu.
Hizo nchi ulizotaja utawazuwia vipi wasiingie Tanzania?

Au wapo kwa vizazi vingapi hivi sasa?

Kweli mzungu ni mashetani, aliyekuja kuweka hii mipaka ya kijinga kabisa. Kakaa berlin huko juu ya meza akajichorea tu. Tutabaguwana mpaka tuuwane, mipango ya Berlin ya kututawala.
 
Kwa mara yakl kwanza Mrembo Faiza nakubaliana na wewe. Labda kama Rais ameamua kulitumia jeshi kisiasa kuwatisha watu wanaompa changamoto kwenye nafasi yake. Vinginevyo ni upoyoyo wa kiwango Cha juu kabisa
Huwa namkubali sana FaizaFoxy lakini katika hili ameniangusha sana. Kimsingi Mtu kama CDF kuzungumza vile ni dhahiri yeye na Boss wake(Rais) + System wanajua wanachokifanya. Pia ninaamini taarifa inayosomwa kwa Rais huwa inafanyiwa clearance na hata mwenyewe kuipata kabla na sio kwamba pale ndio anaipata.

Hivyo na wewe jaribu kufikiri nje ya Box
 
Duuh hatari sana aangalie MaRC wapo na MaDC yule bwanaa kwao RC sehemu nina wasiwasi nae apitie hata yule mama ana title ya Balozi anaanziwa na herufi L na ukoo wake unaanzia na M. daah hapo kuna kazi kwa ufupi apitie upya teuzi zote zilizopita na alizoteua,pale BOT napo pale foreign currency, Pale Costech, Madini, pale kwenye mahela na bajeti Hongera CDF
 
Watanzania tupo warahisi sana kuchezewa akili zenu. Lakini acha tu tuchezewe kwani huwa hatutaki kutafakari. Hivi jambo kama ni hili ni la utekelezaji au ni la kusemea kwenye majukwaa! Tuna idara za usalama, upelelezi na ulinzi.

Kama wamegundua kuna watu wa aina hii kwa nini wasiondolewa kwanza? Rais kila siku ni lazima apewe briefing kuhusu masuala mbali mbali ya nchi, ina maana hawakumwambia huko kwenye vikao?

Kwangu mimi hili ni suala la utekelezaji zaidi na siyo suala la kusemea jukwaani. Otherwise, kuna jambo fishy linataka kufanywa na huu ni mwanzo tu wa kulihalalisha.
Chama dhaifu huzalisha serikali dhaifu

Sent from my Infinix X657C using JamiiForums mobile app
 
Mipaka iliwekwa, na wakoroni, jamii moja ikajikuta IPO Nchi mbili,mfsno Jaluo,Kenya na tz,mmsai Kenya na tz, sio dhambi,ukisema kama raia yoyote anayefanana na watu wa Nchi nyingine, aondoke, huo ni ujinga na upumbavu, vice president wa USA, baba mjamaika, mama Indian, kazaliwa USA!
Obama, Mama mzungu, baba M Kenya!
Trump, Biden wana asili ya Ireland, Biden alienda mpaka kijiji alichotoka babu yake, sie mi afrika bado, tunapalulana na kuchukiana kisa mie naitwa mkama, na Uganda wapo wanaoitwa mkama, au Mimi naitwa onyango,cha cha na Kenya wapo kina onyango, ni akili za kijinga Sana,
Dunia inategnenza uwezekano wa kwenda kuishi mwezini, sie tunabaguana kwa makabila!
We mgeni, Malengo , Sasa kama wako kwa malengo tofauti ndo mana tumewashtukia, ila wangekuwa wanaipambania nchi Wala tusingeshtuka
 
Suala siyo asili ya mtu. Bali kuwa na wahamiaji haramu wanaotaka kupoka mamlaka ya nchi. Hatujui dhamira zao.

Hao akina Obama walikuwa wazi, na hawakuwahi kuwa na doa lolote katika kuvunja shetia za nchi. Obama ni raia wa kuzaliwa wa USA, na kwa taratibu za nchi alilazimika kufanya mambo machache tu ya kisheria ili kuukamilisha uraia wake.


Sisi hawa wa kwetu ni shida. Maana kwanza ni waongo. Ukimwuliza Biteko kabila gani, atakuambia ni msukuma!! Wakati siyo kweli. Kama una dhamira njema, kwa nini usikamilishe taratibu zote za kishetia, kama vile kuukana uraia wa wazazi wako, kufanyiwa assessment na jamii juu ya uzalendo wako kwa Tanzania, halafu uwe raia kamili wa Watanzania?

Kwa nini uwadanganye watu kuwa wewe ni msukuma. Halafu umepata cheo, unatumia hicho cheo kuwanufaisha watu wa huko iliko asili yako huku ukiwapora watanzania asilia maeneo yao ya leseni za uchimbaji dhahabu na kuwapa hao watu wa kwenu? Watu wa namna hii hata wakiomba uraia wanatakiwa kinyimwa kwa sababu wameonesha wazi kuwa hawaipendi Tanzania wala watu wake.
Jiwe nae hakuwa mtanzania
 
Usimsahau Nyerere na Mkapa, walishaandikwa sana zamani kuwa ni wageni ardhi hii.

Ukimaliza hapo, tuambie kwenu wapi?
Unajuwa Prof janabi babu yake alitokea Sudan, akaja akalikita dodoma,ndipo akazaliwa mohamed
Janabi refa wa zamani wa mpira tz
Ndipo akatokea Prof janabi
Tukisema hapa tanzania tuchunguzane umetoka wapi nchi hatobakia mtu

Ova
 
Hizo nchi ulizotaja ugtawazuwia vipi wasiingie Tanzania?

Au wapo kwa vizazi vingapi hivi sasa?

Kweli mzungu ni mashetani, aliyekuja kuweka hii mipaka ya kijinga kabisa. Kakaa berlin huko juu ya meza akajichorea tu. Tutabaguwana mpaka tuuwane, mipango ya Berlin ya kututawala.
Hahahaah wazungu.ni mashetanj ulitaka tuwe taifa moja kma marekani siyo
 
Mimi naamini bigezo na masharti yamefatwa.

Ikiwa tutaanza kukokoa vizazi vya watu vya tatu na na nyuma vya Watanzania basi tutajikuta nusu nzima au zaidi siyo wenye asili ya Tanzania.


Mradi sheria na kanuni za uhamiaji zimefatwa na vetting za kiusalama wamepita hao ni raia tu.

Leo Rishi Sunak ni waziri mkuu w Uingereza, wakifatilia kizazi chake cha tatu nyuma, tutamkuta ana Utanzania.
Wewe sio mtz ,tunaweza kukutimua Sasa ivi
 
Back
Top Bottom