Wewe unaielewa vizuri historia.
Hizi propaganda za kisiasa zinatia sana watu upofu wa historia.
Kila anayesimulia mambo ya vita vya Gaza na historia ya wayahudi, huwa anaanzia kati kati ya miaka ya hivi karibuni.
Nimemsikiliza msomi Tundu Lisu juzi nikashangaa sana alivyokuwa akieleza historia hiyo, naye akijikita katika propaganda hizo hizo.
Kila msimuliaji wa historia hasa ya Wayahudi, lazima aipotoshe, sielewi ni kwa manufaa ya nani.
Inaonekana kama vile Wayahudi waliokotwa maeneo mbali mbali duniani na kuja kupachikwa Israel na kuanzisha taifa lao bila ya kuwa na asili ya eneo hilo.
Ndiyo propaganda hizo za uongo zinavyopikwa kuonesha kuwa, wayahudi waliokotezwa maeneo mbali mbali ya Ulaya na kuja kupachikwa eneo walipo leo bila ya kuwa na uasili wa eneo hilo, very pathetic!