Hawa wateja wanaoukuja kila mara dukani na kutuhangaisha muda mrefu bila kununua kitu tunadili nao vipi?

Tatizo na nyie wauzaji hamueleweki mnapandisha bei kiholela mno. Kuna sehemu nilienda zaidi ya mara tatu naulizia kitu kimoja nakuta bei tofauti huku muuzaji ni yule yule.
 
Huyu kiboko.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mbavu zangu
 
muhindi ndiyo anawapiga bao hapo waswahili kwenye biashara.

Muhindi ukienda dukani kwake yeye ndo anajihangaisha kukuonyesha bidhaa zaidi ya zile unazoziulizia.

Hebu ifike mahali waswahili mjifunze cross-selling and up-selling.
Muhindi yupi mbona wa Kariakoo wanatuma mbongo Juma onyesha hiyo

Yeye kakaa nyuma ya kabati
 
Akitoka hapo hutomuona,
Kwangu hii ni mara 4,
kwa mfanyakazi ndio hazihesabiki..
Akija siku nyingine mwambie akupe laki moja kwanza kabla kuanza kuuliza anachokitaka. Akiuliza kwa nini unamwambia ni gharama za malipo ya stoo kwa ajili ya mizigo minne tuliyoifunga tukisubiri uje kuinunua ukitoka kwenye banda la mpira.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Ila ulimkosea huyo mzee, hivi hajarudi tena? au tuseme leo si kuna mpira wa simba vs yanga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Ila ulimkosea huyo mzee, hivi hajarudi tena? au tuseme leo si kuna mpira wa simba vs yanga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi sijamkosea chochote mkuu,
Ni Sifa zake ndio zinamtesa, namsubiri kesho na kitambi chake
 
Makiseo na Carleen mnaombwa mkaripoti kituo chochote cha polisi kilicho karibu yenu sababu mmeharibu uzi wa jamaa kwa stori
Haha..
Huu ni uthibitisho kuwa umeelewa tulichokuwa tunafanya na Makiseo na hii ni namna yako ya kipekee ya kutuunga mkono ili tuendelee kuharibu vizuri uzi wa watu na mimi kwa moyo mkunjufu kabisa nakukaribisha sana..!!
 
Muhindi ndiyo anawapiga bao hapo waswahili kwenye biashara.

Muhindi ukienda dukani kwake yeye ndi anajihangaisha kukuonyesha bidhaa zaidi ya zile unazoziulizia.

Hebu ifike mahali waswahili mjifunze cross-selling and up-selling.


Muhindi maisha yake magumu sana huwezi kumfananisha na sisi.
 
Shabiki wa simba [emoji250][emoji250][emoji23][emoji23]
 
Hahahah sasa sindio biashara babu, watu wote wangekuwa hivyo si Mlimani City pangebakia duka la pipi tu na walinzi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Mwenyewe juzi nimeingia SONY Store nimeenda kuuliza OLED TV ambayo bei yake ni ghali kuliko gari nayotembelea πŸ˜‚ ila very confidently nikawaahidi nitarudi after Xmas. Kwahio ni swala tu la kuheshimu wateja jamani. Hii dunia ni yetu sote kuuliza bure kuchukua na hela 😝
 
Nafikir matatizo ya customer service hua yanaanzia hapa, ndugu wafanyabiashara hebu punguzen makasiriko kidogo. Uko hapo dukani sio kwa kutoa bidhaa kwa shelfu na kumfungia mteja na kupokea hela na kurudisha change. Kuulizwa bei za bidhaa, kuonyesha bidhaa ulizonazo kwa mteja, na hata wakat mwingne kutoa ushauri ni sehemu ya biashara uifanyayo. Usijenge chuki kwa mteja wa namna hiyo anaweza kua mnunuzi wako mzuri kwa kesho, who knows?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…