Hapa kwenye biashara yangu kwa nyuma kuna banda la mpira, Sasa kuna mzee mmoja huyo ni shabiki wa simba, basi kila kukiwa kuna mpira wa simba ndio unamuona.
Kabla hajaingia lazima apitie Dukani kuangalia na kuulizia bidhaa na ana oda bidhaa nyingi kama humjui waweza useme leo Nimeula, Anapenda sana kubagain bei, unakua mpole kumshushia sababu unaona anataka mzigo mkubwa.
Hio ndio kawaida yake, Niwepo mimi au mfanya kazi, halafu akimaliza anasema Usifunge duka nifungie mzigo wangu Nikitoka kuangalia mpira nakuja kuchukua si tushapatana bei, basi unalazimika kuchelewa kufunga kwa sababu yake.
Akitoka hapo hutomuona,
Kwangu hii ni mara 4,
kwa mfanyakazi ndio hazihesabiki..
Jana kama kawaida, Kipindi cha kwanza kilivyoisha nikamwambia Mzee vipi njoo uchukue maana leo sitasubiri mpira uishee,
Akasema "kijana usijali mimi nikisema nimesema huwa sina uswahili"
Daaa kimoyo moyo nikajisemea hivi huyu anaelewa anachokisema kweli?
Au nimemfananisha???
Kipindi cha pili kimeanza tuu nikaona ujinga huu, nikafunga nikasepa halafu nikamwabia jirani huyo mzee akija hapo hata akisimama kwenye grili mzuge nakuja halafu niambie nichukue boda fasta.
Jamaa baadae anani text...
"Oya mzee wako leo kapitia nyuma ya banda"
Hata Kama mteja ni mfalme, Mfalme huyu ngoja tu nimkose.
Sasa si ujinga huu, mtu mzima kama yule anajitesa kwa uswahili mpaka unapitia uwani kwa watu...?
Ukidumbukia kwenye shimo la choo utasemaje???