Hawa wateja wanaoukuja kila mara dukani na kutuhangaisha muda mrefu bila kununua kitu tunadili nao vipi?

Eti oya mzee wako leo lapita nyuma ya Banda 😂😂
 
Biashara ni uvumilivu mkuu , kwa Hua hajulikani nani ni mnunuzi na nani c mnunuzi cha msingi ni kuendelea kuvumilia na kua makini maana kuna wengine Hua ni wezi wanakulia timing uzubae wakupige ,

Kiuhalisia mtu akija zaidi Ya mara mbili kukusubua na ukamkariri inatakiwa tu umwambie ukwel kua haupo tayari kusumbuliwa
 
[emoji3][emoji3][emoji3]this is thimba...
 
Ndio maana ikitwa window shopping. Ukiona hutaki maswali ma usumbufu, weka bei kwenye bidhaa zako, mteja akija azunguke kutazama akimaliza aondoke...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hiyo ndio biashara Mimi hata niwe naongea na simu akiingia mteja awe ananunua awe hanunui simu naikata na nitasimama kwa heshima zote kumkaribisha anaweza asinunue lkn atapatangaza mnaongea vzr,huduma nzr na akakuletea wateja hata 100 nyuma yake...

Mimi huwa simpi pesa yangu MTU asiyeheshimu mteja yaan naingia dukani kwako uko bize na simu nakuuliza BEI unajibu huku unaendelea na simu hapo hela yangu huwezi kuipata asilan ndugu zangu wananiita mkoloni kwa.Tabia hiyo...hahaaa
 
Kikubwa uvumilivu tu mana hujui yupi mteja yupi mpitaji biashara ngumu mkuu wazee wa window shopping wanaua sana
 
Wengi hawajaelewa mada husika.. Huwezi kuja mara 3 kwa wiki halafu unauliza tu.. Mwingine unamuuliza una sh ngap kwani anakujibu nitarudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…