Una uhakika miezi sita ijayo hali itaendelea kuwa hivyo?
I wish I had a crystal ball I’d look into and tell me what will happen 6 months from now. But I don’t.
Hivyo, sijui.
Na kuna tahadhari yoyote unayoweza kuchukua leo ili miezi sita baadaye hali isije kuwa kama sehemu ambazo igonjwa huu umeua watu sana?
Ndiyo.
Kujiandaa kwa majanga ndo tahadhari yenyewe.
Ukijua leo kwamba wewe utakuwa mmoja ya watu watakaofariki kwa ugonjwa huu katika miezi sita ijayo, ingawa ugonjwa hauui sana, bado utasema ugonjwa huu si wa kutisha?
Hahaaaa. Kama kuna mtu mwenye uwezo huo [wa kujua kwamba yeye atafariki katika miezi sita ijayo basi namwonea wivu. Maana kujua wakati wako wa kufa si sifa ndogo].
Kesho yenyewe tu kujua kitachokutokea, ni mbinde. Seuze miezi sita mbele!!?
Kwa nini miezi sita? Hiyo ndo incubation period ya coronavirus?
Inavyosemekana ni kwamba huu ugonjwa ulianza mwishoni mwa mwaka jana. Kati ya Novemba na Disemba. Mida hiyo watu walishaanza kuripoti dalili zake.
Nikihesabu miezi tokea muda huo, napata miezi 8/9.
Huo ni muda wa kutosha kabisa.
Ya nini sasa kusubiri hadi miezi sita tokea sasa?
Hujasikia habari za vaccine trials toka sehemu mbalimbali ikiwemo ile ya chuo kikuu cha Oxford?
Miezi sita ijayo huenda tayari kukawepo na chanjo kadhaa dhidi ya hivyo virusi.
Kama Tanzania pamoja na kutojali mask,pamoja na uchaguzi, hakutakuwa na mfumuko wa Covid-19 kiasi cha watu ku notice, then, kwa muktadha wa huko,ugonjwa huu unaweza kuwa hatari, lakini si sana. Mseme "C'est la vie", mambo yaendelee.
Karibu miezi miwili sasa au hata zaidi, watu walishaacha kuishi kwa hofu kubwa na kuchukua tahadhari kali lakini hakuna lolote baya na lililo kubwa ambalo limetokea.
Kwani ile makala uliyoileta hapa jana ni ya lini? Siyo hivi karibuni?
Mwandishi mwenyewe kafanya ka-uchunguzi kake na kaishia kwenda kula pilau tu 🤣.
Tumewaona wazee akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Lipumba, Lowassa, Membe, Maalim, na wengineo wakijichanganya bila hizo tahadhari.
Inavyosemekana, median age ya COVID related deaths ni mid 70s.
Hivyo hao wazee wapo kwenye very high risk group. Muda wote huu wamekuwa wakionekana hadharani bila hata barakoa wala social distancing [ukiachilia labda pale mwanzoni mwanzoni ambapo kila mtu alikuwa kwenye taharuki]. Lakini wazee hao mpaka sasa bado wapo na wanaonekana wenye afya nzuri tu.
Anyway, muda utazungumza tu. Ila ndo sijui itakuwa lini maana kirusi kaanza kuwepo kitambo.
Mi mwenyewe nahisi nilikuwa naye mwezi wa Februari kipindi cha Valentine’s lakini nilipona.
Na muda wote huu nimekuwa natoka nje, nasafiri, sivai barakoa, gym naenda, na hata totoz bado nafukuzia 😄.
Huku kwetu tulipo sasa tumeona uneua watu wengi sana na tumeuheahimu kama ugonjwa hatari.
Mazee uko muoga sana. Au labda kama una compromised immune system.
Hivi bado tu umejifungia ndani?