Hawa watu sasa wamekubali kuwa Corona imeisha?

Hawa watu sasa wamekubali kuwa Corona imeisha?

Ukinieleza ya Uingereza, halafu ukataka kuyafananisha na ya Tanzania, nitakwambia uwazi kabisa kwamba unapotea.

Vifo vinavyotokea Uingereza vinafahamika vinasababishwa na/au husishwa na nini. Kumbukumbu hizo ni lazima ziwepo kisheria si kwa matakwa tu.

Sasa kama unazungumzia vipimo vya maenezi ya ugonjwa katika jamii, hilo litakuwa ni swala tofauti.

Tunajadili vipimo sio vifo, mbona unatoka kwenye hoja? Nimetaja vipimo kwa sababu msingi wa Tanzania kusitisha kutangaza maambukizi mapya ilikua ni vipimo.

Usahihi wa vipimo unauongeleaje?
 
Jitahidi kujua, at a minimaum, kama kuna ongezeko lolote la vifo katika huu muda ambao corona imeingia, hata kama hujapima waliokufa wamekufa kwa ugonjwa upi.
Hili nalo ni jambo zito kulifanya?

Lakini hamtaki kujua, msionekane mapambano yenu ambayo mnajivunia hayakufana!

Hicho ndio unachoshauri mtaalam?
 
Kwa sababu tumeongozwa na Magu kujitoa ufahamu.hata hivyo my point was hata Kama watu wanakufa bila serikali kutoa takwimu zinazokusanywa kutoka facilities za afya ni ngumu kwa mtu kujua wangapi wanakufa kwa corona na wamefia wapi mbaya zaidi imeruhusu tuzikane wenyewe ili tuambukizane vizuri
Ni kwamba hujui kwasababu vifo hivyo hakuna! Mbona hili suala mnashindwa kulikiri?
 
Ubalozi wa Marekani bado unawaonya watalii kuja Tz.Why?

Wenyewe wakati wa maandamano ya juzi walivaa barakoa na kuzingatia tahadhari zote za kujilinda na Covid? Si walikua lockdown wale? Mbona waliandamana barabarani kwa maelfu si hadi sasa hivi ingekua nusu ya nchi imeshaangamia?

Watalii wanashuka hivi tunavyoongea. Achana na Marekani kasema nini. Ana haki ya kuwalinda raia wake hilo hatuwezi kumzuia.
 
Wenyewe wskati wa maandamano ya juzi walivaa barakoa na kuzingatia tahadhari zote za kujilinda na Covid? Si walikua lockdown wale? Mbona waliandamana barabarani kwa maelfu si hadi sasa hivi ingekua nusu ya nchi imeshaangamia?

Watalii wanashuka hivi tunavyoongea. Achana na Marekani kasema nini. Ana haki ya kuwalinda raia wake hilo hatuwezi kumzuia.
Hoteli nyingi za kitalii bado zipo closed.
Na nakuhakikishia kuwa Kenya watatupiku kwa utalii vibaya sana
 
Tunajadili vipimo sio vifo, mbona unatoka kwenye hoja? Nimetaja vipimo kwa sababu msingi wa Tanzania kusitisha kutangaza maambukizi mapya ilikua ni vipimo.

Usahihi wa vipimo unauongeleaje?
Unao ushahidi wowote unaoonyesha kwamba vipimo sio sahihi,?

Kumbuka, usije ukachanganya hayo yanayohojiwa huko Uingereza na usahihi wa vipimo.

Nionyeshe sehemu walipodai kwamba vipimo havifanyi kazi na ndio sababu ya kusitisha kupima.
 
“When you are up there do not forget those who are below you because you may need them on your way down” Does this saying make sense as relates to Lowassa and Membe?. This should also apply to Bashite as he is living as semi -God!
 
Hoteli nyingi za kitalii bado zipo closed.
Na nakuhakikishia kuwa Kenya watatupiku kwa utalii vibaya sana

Watalii nchi zao bado zimefungwa, unategemea waje kwa wingi wakati huu?

Hilo la Kenya kutupita muda utaamua.
 
Umechoka!

Utaalam unaipachika wewe, mimi sijaandika popote kuwa ni mtaalam wa chochote.

Sijachoka ila kila nnapojaribu kujua unachokitaka tunazidi kuvuta mambo tu.
Kwakua tunachojadili ni Covid, nikaona sio mbaya kujua wewe unapendekeza mambo gani yafanyike kwa hii hatua tuliyonayo kuhusu Corona.
 
Unao ushahidi wowote unaoonyesha kwamba vipimo sio sahihi,?

Kumbuka, usije ukachanganya hayo yanayohojiwa huko Uingereza na usahihi wa vipimo.

Nionyeshe sehemu walipodai kwamba vipimo havifanyi kazi na ndio sababu ya kusitisha kupima.

Unakumbuka Vipimo vilivyorudishwa India kuwa na hitilafu?
Umeshawahi kusikia watengenezaji au wasambazaji wa vifaa vilivyodaiwa kutokutoa majibu sawa na JPM wakipinga au kukanusha zile tuhuma nzito?
 
Sijachoka ila kila nnapojaribu kujua unachokitaka tunazidi kuvuta mambo tu.
Kwakua tunachojadili ni Covid, nikaona sio mbaya kujua wewe unapendekeza mambo gani yafanyike kwa hii hatua tuliyonayo kuhusu Corona.
Basi hutaki kuelewa ninachoandika kama huoni ninachokitaka katika maandiko yooote niliyoweka hapa, na siwezi kukulazimisha uyaone kuwa ni mapendekezo.

Nimekwishakueleza toka mwanzo, kosa la kwanza lililofanyika ni tabia ya kuficha ficha mambo, ukidhani hayatafahamika.

Mambo kama corona huwezi ukaficha, kuwa tu mkweli watu wajue.

Historia ya muda mfupi inatuonyesha kuwa hiyo ndio tabia yetu, ya kuficha ili "watalii" wasiogope kuja.

Binti Malicela na Zika yake humkumbuki? Huko ndiko tulikotokea hadi tukaingia kwa corona.

Nimekwishakueleza: sehemu mhimu ya kufanya jambo lolote ni kufuata taratibu zinazofahamika. Wataalamu watatoa ushauri, zingatia wanayosema na usiwatishe hata wengine kuwatumbua, kama yule waziri mdogo wa Afya.

Fanya maamuzi katika misingi ya taratibu.
Hili ni janga la dunia, sio la Tanzania pekee, kutumia tu hisia, eti kwa misingi ya hisia, na kuuita 'uthubutu' ni upotofu wa hali ya juu, pamoja na kwamba bahati yetu ndio hiyo imetuvusha wakati huu.

Sasa unataka nipendekeze nini, nikubali tu kwamba Corona haipo Tanzania sasa hivi?

Ngoja nimalize kwa kukupa pendekezo langu la mwisho:

Hii iwe ni fursa kwetu , kwa nchi yetu kuimarisha uwezo wetu wa kushughulikia majanga kama haya yanapojitokeza.

Kwa mfano. Hadi sasa hakuna anayefahamu bahati yetu imetokana na nini. Sizungumzii bahati ya Tanzania pekee, hata huko kwa majirani zetu wanakopima na kutangaza corona haikuathiri kama ilivyoathiri sehemu zingine duniani.

Kwa nini tusianzie hapa kuimarisha wataalamu wetu na sehemu zao za kazi kuanza kufanya tafiti za namna hii na nyinginezo. Kisingizio mara nyingi ni uwezo wa kipesa, lakini hili sio sahihi kiujumla. Uimara wa tafiti za mambo kama haya hutegemea mashirikiano na wadau mbalimbali duniani, ambao wanaweza kushiriki na tukawa imara kupitia njia hizo.

Huenda ni mimi nisiyejua. Hebu nipe mfano wa maabara zetu zinazojishughulisha na tafiti kama hizi.

Sitaki kuandika kitabu kwa mtu kama wewe uliyeshikilia msimao ulioushikilia kiasi kwamba unasoma umefumba macho.
 
Unakumbuka Vipimo vilivyorudishwa India kuwa na hitilafu?
Umeshawahi kusikia watengenezaji au wasambazaji wa vifaa vilivyodaiwa kutokutoa majibu sawa na JPM wakipinga au kukanusha zile tuhuma nzito?
Kwa hiyo hiyo ndiyo ikawa sababu ya kuacha kupima kabisa?

Mbona huko kwingine wanapima.

Ndio, nilisikia WHO wakikanusha kuhusu ubovu wa vipimo, sasa sijui kama ni hivyo unavyoandika hapo juu au hivyo nivingine.

Na kama una 'background' ya sayansi ya aina yoyote, huwezi kuchukulia ile njia iliyotumika kuashiria ubovu wa vipimo vile. Ile ilikuwa ni njia ya mtu asiye elewa chochote kuhusu tathmini ya ubora wa vipimo.
 
Kwenye Corona tulilishwa matango pori haswa. Sijui hata imepotelea wapi, tusingekuwa na mtu wa msimamo by now tungekuwa hoi kabisa kiuchumi.
 
Kitu cha muhimu ni kushukuru tu wasiwasi mbaya sana bp nje nje
 
Kwenye Corona tulilishwa matango pori haswa. Sijui hata imepotelea wapi, tusingekuwa na mtu wa msimamo by now tungekuwa hoi kabisa kiuchumi.
Hata vyama vya upinzani kimoyomoyo si ajabu wanaukubali msimamo wa Magufuli.

Maana kama wangekuwa hawamkubali, basi kwenye mikutano yao wangekuwa wanafanya tofauti.

Hebu ona hii shughuli ya Zuchu jana. Hakuna cha barakoa. Hakuna social distancing. Hakuna hofu ya korona.

Yaani COVID-19 ni ancient history 🤣🤣

 
Tungekuwa na Rais mwenye uthubutu wakati UKIMWI unaingia wala usingekuwepo Tanzania😁
 
Back
Top Bottom