The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 21,281
- 49,313
Basi hutaki kuelewa ninachoandika kama huoni ninachokitaka katika maandiko yooote niliyoweka hapa, na siwezi kukulazimisha uyaone kuwa ni mapendekezo.
Nimekwishakueleza toka mwanzo, kosa la kwanza lililofanyika ni tabia ya kuficha ficha mambo, ukidhani hayatafahamika.
Mambo kama corona huwezi ukaficha, kuwa tu mkweli watu wajue.
Historia ya muda mfupi inatuonyesha kuwa hiyo ndio tabia yetu, ya kuficha ili "watalii" wasiogope kuja.
Binti Malicela na Zika yake humkumbuki? Huko ndiko tulikotokea hadi tukaingia kwa corona.
Nimekwishakueleza: sehemu mhimu ya kufanya jambo lolote ni kufuata taratibu zinazofahamika. Wataalamu watatoa ushauri, zingatia wanayosema na usiwatishe hata wengine kuwatumbua, kama yule waziri mdogo wa Afya.
Fanya maamuzi katika misingi ya taratibu.
Hili ni janga la dunia, sio la Tanzania pekee, kutumia tu hisia, eti kwa misingi ya hisia, na kuuita 'uthubutu' ni upotofu wa hali ya juu, pamoja na kwamba bahati yetu ndio hiyo imetuvusha wakati huu.
Sasa unataka nipendekeze nini, nikubali tu kwamba Corona haipo Tanzania sasa hivi?
Ngoja nimalize kwa kukupa pendekezo langu la mwisho:
Hii iwe ni fursa kwetu , kwa nchi yetu kuimarisha uwezo wetu wa kushughulikia majanga kama haya yanapojitokeza.
Kwa mfano. Hadi sasa hakuna anayefahamu bahati yetu imetokana na nini. Sizungumzii bahati ya Tanzania pekee, hata huko kwa majirani zetu wanakopima na kutangaza corona haikuathiri kama ilivyoathiri sehemu zingine duniani.
Kwa nini tusianzie hapa kuimarisha wataalamu wetu na sehemu zao za kazi kuanza kufanya tafiti za namna hii na nyinginezo. Kisingizio mara nyingi ni uwezo wa kipesa, lakini hili sio sahihi kiujumla. Uimara wa tafiti za mambo kama haya hutegemea mashirikiano na wadau mbalimbali duniani, ambao wanaweza kushiriki na tukawa imara kupitia njia hizo.
Huenda ni mimi nisiyejua. Hebu nipe mfano wa maabara zetu zinazojishughulisha na tafiti kama hizi.
Sitaki kuandika kitabu kwa mtu kama wewe uliyeshikilia msimao ulioushikilia kiasi kwamba unasoma umefumba macho.
Nasoma nimefumba macho?
Kwahiyo tunachotakiwa kufanya sasa hivi ni kupambana na utafiti kujua kwanini tumebahatika, hicho tu?