Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Habari Wakuu,

Inafika hatua naanza kujiuliza hawa watu wanaondoka katika mazingira ya kawaida tu au kuna system inawaondoa kwa kutumia mbinu zilizoenda shule?

Yaani Bwana yule na watu wake wa karibu, wanaondoka mmoja baada ya mwingine, huku yule mwingine akiponea chupuchupu baada ya kudaiwa kuugua Covid iliyomlaza kitandani na kulazimika kutumia mtungi kuokoa maisha yake ingawa leo kapanda cheo.

Naanza kujiuliza hii Covid ndio inatumika kuwaondoa maana kwa Bongo imekuwa ni too much katika kuondoa vigogo. Na kama ni Covid, mbona wanasita kuitaja? Au ndio wanatumia mwanya huu kuondoa ile inner circle yote ya Bwana Yule?

Yaani sasa napata mashaka kuwa huenda wanaishi na nyoka anaewagonga na kuwatemea sumu pasipo wao kujua. Nyoka huyo huenda asili yake ni humu humu ndani au katengenezwa kutoka huko nje ila kwa kushirikiana na wa ndani.

Hivi sasa hata ukiangalia baadhi ya picha zao za pamoja, utaona jinsi walivyopukutika mmoja baada ya mwingine mpaka unabaki kushangaa.

Kwa mtazamo wangu, hali hii sio ya kawaida wakuu unless ni hisia zangu tu.

Anyway, time will tell.
 
Corona ipo na ukiizingua inakuzingua.
hawa vigogo na magonjwa yao yasio na tiba, Corona inabambataa..!
tulikosea toka mwanzo tulipo zifuata legacy za Mwendawazimu .
na tunavyochelewa kupata chanjo,
Mashaka matupu. MaCCM hatutawasamehe.
 
Corona ipo na ukiizingua inakuzingua.
hawa vigogo na magonjwa yao yasio na tiba, Corona inabambataa..!
tulikosea toka mwanzo tulipo zifuata legacy za Mwendawazimu .
Mpaka kufika 2025, tunaweza kuwa na mkuu wa kaya/wakuu wa kaya wengine wa kurithi zaidi ya huyu wa sasa kama kweli Covid ndio inahusika na si vinginevyo.
 
Magufuli, Kijazi na Mfugale Hawa watu kwa miaka 20 iliyopita wamefanya kazi kwa karibu sana kati ya TANROADS na Ujenzi. Hao wameshirikiana sana kugawana rushwa itokanayo na mikataba ya Ujenzi.

Ndiyo kisa wakawa wanabatiza madaraja kwa majina yao. Siyo ajabu kuona wote wanaondoka kwa COVID19
 
Hawa virus washenzi kweli, siku hizi wanakula kimyakimya, ukianza kuhisi vibaya tu kwa heri, yule mama aliefariki ghafla akila futari hoteli gani sijui, ni uthibisho kuwa covid wako kazini na wanatafuna kimya kimya tu, siku hizi hukohoi wala kutoa mafua.

Kwa msiojua huu ugonjwa ni cardiovascular disease, sio Respiratory.
 
Back
Top Bottom