Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Hawa watu wanaondoka kawaida au kuna system inawaondoa kwa kutumia akili kubwa sana?

Mtu kama dikteta alijua fika yuko miongoni mwa makundi hatarishi yanayopaswa kujilinda dhidi ya UVIKO..

Ila he was careless kila mahali na kila kitu kwake alitumia minguvu pasipo ulazima kwahiyo ni uzembe wake kujiexpose ! Kwani umesahau last year alikua mtoro siku 50 alipokua amejifungia machakani kwao kule
 
ni kweli ni kazi walizochagua, lakini pia tambua kazi hizo zinahitaji kujitoa maana hata wao wangeweza kufanya kazi unayofanya, au wangeweza kutokuwa waaminifu na kila siku maadui wakavamia....usifikiri wale wanaokesha kwenye mashimo huko mipakani ni kazi na sio uzalendo pia kwa taifa lao.... usifikiri hao walio busy kufuatilia nyendo za watu na mwenendo wa mambo katika nchi usiku na mchana wanafanya kwa sababu ni kazi tu wameichagua bila chembe ya uzalendo..

Uhalifu upo kila mahala duniani, hata nchi zenye mifumo bora kabisa ya ulinzi duniani watu wanauwawa kila siku....ukizungumzia nchi zenye high crime rate duniani tanzania haiwezi kuingia hata kumi bora...kuokotwa watu kwenye viroba sio kweli ndio iwe sababu ya kuviona vyombo vya ulinzi na usalama havifanyi kazi maana wote tungekuwa kwenye viroba....

JF Kennedy aliuwawa ndani ya USA ikiwa na vyombo bora kabisa vya ulinzi, September 11 USA ilipigwa ikiwa na vyombo bora kabisa vya ulinzi, Big na tupac walipigwa risasi kweupe kabisa...bado daily shoot the mtaani usizozijua ambazo zinachukua maelfu ya watu, SA wako na vyombo bora mara 100 zaidi yetu lakini uhalifu na mauaji ya kila siku ni hatari...

Hapo uliposema kuwa watu kuokotwa kwenye viroba sio kweli nimejua huna jipya. Na hata hayo maelezo yako mengine yote nimeyapuuza.
 
Kupambana mitandaoni ni dalili ya uoga, mapambano ya kweli na watawala yako barabarani.....wote waliofanikisha mambo yao dhidi ya tawala dhalimu walitoka barabarani...

Concern yangu, wakati wa JPM hakuna aliyejaribu kusimama barabarani kumpinga au kupambana naye zaidi ya wachache huku mitandaoni ambao wasingeweza kumnyima usingizi....alipiga marufuku mikutano ya siasa na maandamo na hakuna aliyejaribu kutoka barabarani tena kwa mikwara mbuzi kabisa ya lina Moroto...
TL alipigwa risasi mchana kweupe, nani aliyetoka barabarani kudemand justice for TL, nani aliyetoka barabarani kudai uchunguzi huru dhidi ya shambulio ya TL.
Uchaguzi haukuwa huru na haki yakaitishwa maandamano, nani alitoka barabarani kunyanyua bango...

Naomba nikwambie, Watanzania bado hawajachoka au kuichoka CCM siku ikifika automatically tu utaiona response yao dhidi ya dola...najua na nimewashawahi kufika nchi za watu waliochoka na tawala zao, Tanzania bado watu wanashiba ugali...

Kwa taarifa yako maandamano ni hatua ya mwisho kabisa ya kuchokwa, dalili za dhahiri za kuchokwa utaona kwenye box la kura. Kwa jinsi ccm inavyotegemea vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti, ni mtu mwenye upeo mdogo tu atasema ccm haijachokwa. Akina Elbashir, Gaddaf nk walitawala nchi zao zaidi ya miaka 30, hawakuwa wanaamini wamechokwa mpaka watu walipoingia mtaani. Na huko kote watu walikuwa hawakohoi zaidi ya kuongea mitandaoni. Huyo Magufuli uliyekuwa unamuona jemadari tungemfurahisha maana tayari watu walishalipuuza box la kura.
 
Vipo viwanda vinaanzishwa kila inayoitwa siku
Kwa trend hiyo vilikuwa vinajengwa kila mara, tunataka vile mlivyokuwa mnaleta propaganda mfu za Tanzania ya viwanda.
 
Kwani kufa ni kitu cha ajabu jamani[emoji23][emoji23][emoji23] nyie ukoo wenu hamfiii

Yaani wanavyoongea utafikiri wenyewe tayari wako peponi wanakula raha. Kumbe hukumu bado iko mbele yao.
🤣🤣🤣
 
Ripoti inaonyesha ktk kipindi cha January hadi Machi baadhi ya taasisi ikiwepo TANROADS NA BANDARI zililipa wakandarasi mara mbili kwa kazi ileile .

SIJUI Mfugale alikuwa ktk hali gani kwa hili.Kifo kina mengi.
 
Sasa tuichoke CCM nani mbadala ? Hawa wapinzani uchwara ndio tuwape nchi ? Ni CCM tu mpaka 2050
Kupambana mitandaoni ni dalili ya uoga, mapambano ya kweli na watawala yako barabarani.....wote waliofanikisha mambo yao dhidi ya tawala dhalimu walitoka barabarani...

Concern yangu, wakati wa JPM hakuna aliyejaribu kusimama barabarani kumpinga au kupambana naye zaidi ya wachache huku mitandaoni ambao wasingeweza kumnyima usingizi....alipiga marufuku mikutano ya siasa na maandamo na hakuna aliyejaribu kutoka barabarani tena kwa mikwara mbuzi kabisa ya lina Moroto...
TL alipigwa risasi mchana kweupe, nani aliyetoka barabarani kudemand justice for TL, nani aliyetoka barabarani kudai uchunguzi huru dhidi ya shambulio ya TL.
Uchaguzi haukuwa huru na haki yakaitishwa maandamano, nani alitoka barabarani kunyanyua bango...

Naomba nikwambie, Watanzania bado hawajachoka au kuichoka CCM siku ikifika automatically tu utaiona response yao dhidi ya dola...najua na nimewashawahi kufika nchi za watu waliochoka na tawala zao, Tanzania bado watu wanashiba ugali...
 
Habari Wakuu,

Inafika hatua naanza kujiuliza hawa watu wanaondoka katika mazingira ya kawaida tu au kuna system inawaondoa kwa kutumia mbinu zilizoenda shule?

Yaani Bwana yule na watu wake wa karibu wanaondoka mmoja baada ya mwingine huku yule mwingine akiponea chupuchupu baada ya kudaiwa kuugua Covid iliyomlaza kitandani na kulazimika kutumia mtungi kuokoa maisha yake ingawa leo kapanda cheo.

Naanza kujiuliza hii Covid ndio inatumika kuwaondoa maana kwa Bongo imekuwa ni too much katika kuondoa vigogo? Na kama ni Covid, mbona wanasita kuitaja? Au ndio wanatumia mwanya huu kuondoa ile inner circle yote ya Bwana Yule?

Yaani sasa napata mashaka kuwa huenda wanaishi na nyoka anaewagonga na kuwatemea sumu pasipo wao kujua. Nyoka huyo huenda asili yake ni humu humu ndani au katengenezwa kutoka huko nje ila kwa kushirikiana na wa ndani.

Hivi sasa hata ukiangalia baadhi ya picha zao za pamoja, utaona jinsi walivyopukutika mmoja baada ya mwingine mpaka unabaki kushangaa.

Kwa mtazamo wangu, hali hii sio ya kawaida wakuu unless ni hisia zangu tu.

Anyway, time will tell.
CC: UVIKO 19
 
Hakuna cha System wala Uvuko-19. Sababu ya kifo ni hii hapa

'Siku za mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni fupi sana tena zimejaa tabu'

Kifo kwa mtu maarufu kwenye jamii hutafutiwa sababu za kuungaunga wakati kila uchao mamia ya ndugu zetu wanapoteza maisha.

It was a regular death. Rest in peace Engineer Mfugale, Engineer Kijazi, HE JPM
 
Back
Top Bottom