Habari Wakuu.
Inafika hatua naanza kujiuliza hawa watu wanaondoka katika mazingira ya kawaida tu au kuna system inawaondoa kwa kutumia mbinu zilizoenda shule?
Yaani Bwana Yule na watu wake wa karibu wanaondoka mmoja baada ya mwingine huku yule mwingine akiponea chupu chupu baada ya Covid kumlaza kitandani na kulazimika kutumia mtungi kuokoa maisha yake ingawa leo kapanda cheo.
Ni hii Covid ndio inatumika kuwaondoa maana kwa Bongo imekuwa ni too much katika kuondoa vigogo( anyway, labda ni kwasababu wanaipuuza).
Yaani kwa sasa picha zao za pamoja, zinaonyesha jinsi walivyopukutika mmoja baada ya mwingine.
Kwa mtazamo wangu, hali hii sio ya kawaida wakuu unless ni hisia zangu tu.