Hawa wote hawalipi KODI hapa Tanzania

Hapo kwenye listi ongezea wamiliki wa nyumba za kupanga...
 
Kodi gani?
Namba 18 (wamiliki wa daladala) sio kweli, hadi unaiona daladala barabarani tayari inalipa tozo kibao aisee...!


Kuna Kodi nyingi sana kweli
Lakini mmiliki akishapewa mgao wake analipa income tax?Mgao wa dereva je nae nae analipa?Tozo za gari acha..za mafuta hata gari binafsi zinalipa...

Hata housegirl wako anatakiwa kulipa kodi.
Ukiwa na fremu ..Yule muuzaji anatakiwa unapomlipa mshahara na yeye alipe kodi..

Hii elimu ya Kodi bado sana kwa watu wengi
 
Umesahau na malaya
 
Suluhisho ya haya yote ni KATIBA MPYA.shiriki kupaza sauti kijana ili itakapopatikana tuwabane viongoz walipe kodi
 
Hao ulioandika wakianza kulipa Kodi tutapiga hatua, kwanini wao wasitoe kodi
Ulipaji wa kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ila kama kuna baadhi ya watu kama wabunge hawalipi kodi inaumiza sana na inavunja moyo wa kulipa kodi kwa sisi wananchi.
 
Inasikitisha sana, tunapoteza mabilioni ya fedha...
 
Ulipaji wa kodi ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ila kama kuna baadhi ya watu kama wabunge hawalipi kodi inaumiza sana na inavunja moyo wa kulipa kodi kwa sisi wananchi.
Kila mtu lazima alipe Kodi hata mama ntilie, madereva Toyo, bajaji hao wakilipa kikamilifu mbona serikali haitahangaika na kuongeza matozo ya simu yanayoenda kuua kazi za maelfu ya mawakala, na kuathiri kampuni na Kodi maana watu watasusa
 
halafu ndio wanasimama kuwataka wananchi walipe kodi, kwa nchi zilizoendelea kulipa kodi ni moja ya sifa ya kugombea uongozi ndio maana unasikia Trump wanamshutumu kwa kukwepa kodi na ikithibitika tayari anapoteza sifa ya uongozi.
 
Mafundi simu, saa, nyumba, pikipiki,nk. Mama wauza matunda, mboga, na kila mwenye biashara yoyote. Na waliopanga kwenye ardhi za uma bila kulipia kama mabarabarani nk. Kila mtu alipaswa kulipa kodi kwa kila faida anayopata.
 

Ninakazia: Majaji wote akiwamo Jaji Kiongozi Siyani.

Staajabu ya Mussa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…