Hawataki kukubali ukweli kuwa Rais Samia anatuongoza vyema

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari wakuu sijawahi andika hapa kwenye hili jukwaa la siasa ila leo acha ni andike kidogo tu.

Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye raisi wetu ameonyesha muelekeo mzuri kwa kiasi kikubwa katika uongozi wake japo ni mapema kidogo.

Wapo watu bado sijui ni seme wana usingizi au bado giza limetanda machoni mwao kwa maana ya kutoona tofauti ya awamu hii ya 6 na ile ya 5.

Binafsi na furahishwa na utendaji wa rais wetu wa awamu iliyopo madarakani Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuangalia namna anavyo zingatia ushirikishwaji wa idara zote katika kutenda au kufanya jambo husika ndani ya uongozi wake.

Ndio yapo mapungufu machache hatuwezi sema yupo 100% ila kwenye hizo asilimia naimani amefikia 80% kupanda juu.

Aliipokea nchi kipindi kigumu hasa kufiwa na kiongozi mkuu wa nchi jambo ambalo ni geni.katika hili taifa letu. Yote alijitajidi na ameweza kutuunganisha kwa itikadi zetu tofauti tofauti, leo chadema na CCM wanacheka, CUF na Chedema wanakaa pamoja na CCM mtaani tunapiga story kadha wa kadha.

Mambo ya kukaa mwaka bila ajira kwa wahitimu yameanza kutatuka japo idadi ya waliopo mtaani ni kubwa mno. Miradi iliyo achwa inakamilishwa na ameongeza miradi mingine. Fikiria ujenzi wa madarasa kwa mamia kwa shule zetu ni jambo jema na la kupendeza. Mhe amejitahidi kushirikiana na wataalamu kwa kila idara inayohitaji utaalamu.

Ukiangalia kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi wa umma wataalamu wamekaa na kuja na ripoti nzuri ambayo imetumika kuwaongezea mshahara wafanyakazi wa umma.

Demokrasia ile tuliyo izoea imeanza kurudi mahala pake, mambo ya kufanya maamuzi gizani hayapo tena.

Nyakati zimebadilika ila wapo wanaosema hafanyi lolote kwa macho yao yaliyozibwa ambayo hayaoni mabadililo kadhaa basi hawa tuwaweke kundi lile linalo tajwa "SUKUMA_GANG" hawa watu wao hawataki kuamini tusemalo au kuona watu tunaishi kwa amani, furaha na ushirikiano ambayo ndiyo tamaduni yetu.

Kuishi kwa mashaka au kuishi bila kukosoana katika taifa matokeo yake sio mazuri kikubwa tukosoane kwa hekima na kwa manufaa ya hili taifa letu.

Walionyimwa stahili zao wanasema wenyewe kuwa wanalipwa sasa hivi ni jambo jema taifa letu lina rudi mahala pake pa utu kwa watu wake.

Waliosema hataweza kutuongoza sijui wanajisikiaje..? Au nyie mnaoponda sijui mna roho au mawe.??

Kaushauri kwangu kwa utawala wake. Mhe Raisi kile kikokoteo kipya cha mafao nashauri au naomba wastaafu wapewe hela zao kwa namna wanavyotaka wao. Anaetaka kupewa yote apewe akishastaafu, anaetaka % kadhaa apewe kwa namna anayoona inamfaa yeye. Pesa ni zao wastaafu wasipangiwe wajipangie. Kikubwa washauriwe na wapate muongozo utakao wasaidia.

Mwisho. Myonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Mama anaupiga mwingi saana. Ni ombi kwa Mungu wangu wa mbinguni baba mwenye enzi zidi kumlinda na kumpa hekima Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.
FB_IMG_16255040166269644.jpg

Weekend njema wakuu. Sabato ikawe njema na mzidi kumuombea raisi wetu
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Habari wakuu sijawahi andika hapa kwenye hili jukwaa la siasa ila leo acha ni andike kidogo tu.

Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye raisi wetu ameonyesha muelekeo mzuri kwa kiasi kikubwa katika uongozi wake japo ni mapema kidogo. Wapo watu bado sijui ni seme wana usingizi au bado giza limetanda machoni mwao kwa maana ya kutoona tofauti ya awamu hii ya 6 na ile ya 5. Binafsi na furahishwa na utendaji wa raisi wetu wa awamu iliyopo madarakani Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuangalia namna anavyo zingatia ushirikishwaji wa idara zote katika kutenda au kufanya jambo husika ndani ya uongozi wake. Ndio yapo mapungufu machache hatuwezi sema yupo 100% ila kwenye hizo asilimia naimani amefikia 80% kupanda juu.
Aliipokea nchi kipindi kigumu hasa kufiwa na kiongozi mkuu wa nchi jambo ambalo ni geni.katika hili taifa letu. Yote alijitajidi na ameweza kutuunganisha kwa itikadi zetu tofauti tofauti, leo chadema na CCM wanacheka, CUF na Chedema wanakaa pamoja na CCM mtaani tunapiga story kadha wa kadha. Mambo ya kukaa mwaka bila ajira kwa wahitimu yameanza kutatuka japo idadi ya waliopo mtaani ni kubwa mno. Miradi iliyo achwa inakamilishwa na ameongeza miradi mingine. Fikiria ujenzi wa madarasa kwa mamia kwa shule zetu ni jambo jema na la kupendeza. Mhe amejitahidi kushirikiana na wataalamu kwa kila idara inayohitaji utaalamu. Ukiangalia kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi wa umma wataalamu wamekaa na kuja na ripoti nzuri ambayo imetumika kuwaongezea mshahara wafanyakazi wa umma. Demokrasia ile tuliyo izoea imeanza kurudi mahala pake, mambo ya kufanya maamuzi gizani hayapo tena.

Nyakati zimebadilika ila wapo wanaosema hafanyi lolote kwa macho yao yaliyozibwa ambayo hayaoni mabadililo kadhaa basi hawa tuwaweke kundi lile linalo tajwa "SUKUMA_GANG" hawa watu wao hawataki kuamini tusemalo au kuona watu tunaishi kwa amani, furaha na ushirikiano ambayo ndiyo tamaduni yetu.

Kuishi kwa mashaka au kuishi bila kukosoana katika taifa matokeo yake sio mazuri kikubwa tukosoane kwa hekima na kwa manufaa ya hili taifa letu.

Walionyimwa stahili zao wanasema wenyewe kuwa wanalipwa sasa hivi ni jambo jema taifa letu lina rudi mahala pake pa utu kwa watu wake.

Waliosema hataweza kutuongoza sijui wanajisikiaje..? Au nyie mnaoponda sijui mna roho au mawe.??

Mwisho. Myonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Mama anaupiga mwingi saana. Ni ombi kwa Mungu wangu wa mbinguni baba mwenye enzi zidi kumlinda na kumpa hekima Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan. View attachment 2250175

Walete walete 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220604-082128.png
    Screenshot_20220604-082128.png
    51.7 KB · Views: 19
Awamu ya sita ina amani ya kweli mioyoni mwa watu.Kuongoza sio kushurutisha ni kushawishi unaowaongoza.
Labda amani kwako. Mi awamu zote huwa nina amani ilimradi naishi vzr na jamii, kama ulikuwa mkosefu sehemu lazima awamu flan uishi kwa tabu tu. Ila kwa sisi watiifu tuliishi hv hv enzi zote
 
👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220604-125902.png
    Screenshot_20220604-125902.png
    110.6 KB · Views: 15
Ila wapiga kura zaidi ya 50% wangekuwa humu ungewachota sana 😂
Wapiga kura wako huku wanafurahia matunda ya awamu ya 6 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220604-095319.png
    Screenshot_20220604-095319.png
    91.7 KB · Views: 10
  • Screenshot_20220603-220549.png
    Screenshot_20220603-220549.png
    110.4 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220603-163354.png
    Screenshot_20220603-163354.png
    261.1 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220603-104746.png
    Screenshot_20220603-104746.png
    142.8 KB · Views: 10
  • Screenshot_20220601-203006.png
    Screenshot_20220601-203006.png
    171.3 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220601-150915.png
    Screenshot_20220601-150915.png
    284.9 KB · Views: 9
  • Screenshot_20220531-165053.png
    Screenshot_20220531-165053.png
    192.3 KB · Views: 10
  • Screenshot_20220527-214104.png
    Screenshot_20220527-214104.png
    165.1 KB · Views: 10
  • Screenshot_20220526-125408.png
    Screenshot_20220526-125408.png
    178.1 KB · Views: 12
Habari wakuu sijawahi andika hapa kwenye hili jukwaa la siasa ila leo acha ni andike kidogo tu.

Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye raisi wetu ameonyesha muelekeo mzuri kwa kiasi kikubwa katika uongozi wake japo ni mapema kidogo. Wapo watu bado sijui ni seme wana usingizi au bado giza limetanda machoni mwao kwa maana ya kutoona tofauti ya awamu hii ya 6 na ile ya 5. Binafsi na furahishwa na utendaji wa raisi wetu wa awamu iliyopo madarakani Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuangalia namna anavyo zingatia ushirikishwaji wa idara zote katika kutenda au kufanya jambo husika ndani ya uongozi wake. Ndio yapo mapungufu machache hatuwezi sema yupo 100% ila kwenye hizo asilimia naimani amefikia 80% kupanda juu.
Aliipokea nchi kipindi kigumu hasa kufiwa na kiongozi mkuu wa nchi jambo ambalo ni geni.katika hili taifa letu. Yote alijitajidi na ameweza kutuunganisha kwa itikadi zetu tofauti tofauti, leo chadema na CCM wanacheka, CUF na Chedema wanakaa pamoja na CCM mtaani tunapiga story kadha wa kadha. Mambo ya kukaa mwaka bila ajira kwa wahitimu yameanza kutatuka japo idadi ya waliopo mtaani ni kubwa mno. Miradi iliyo achwa inakamilishwa na ameongeza miradi mingine. Fikiria ujenzi wa madarasa kwa mamia kwa shule zetu ni jambo jema na la kupendeza. Mhe amejitahidi kushirikiana na wataalamu kwa kila idara inayohitaji utaalamu. Ukiangalia kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi wa umma wataalamu wamekaa na kuja na ripoti nzuri ambayo imetumika kuwaongezea mshahara wafanyakazi wa umma. Demokrasia ile tuliyo izoea imeanza kurudi mahala pake, mambo ya kufanya maamuzi gizani hayapo tena.

Nyakati zimebadilika ila wapo wanaosema hafanyi lolote kwa macho yao yaliyozibwa ambayo hayaoni mabadililo kadhaa basi hawa tuwaweke kundi lile linalo tajwa "SUKUMA_GANG" hawa watu wao hawataki kuamini tusemalo au kuona watu tunaishi kwa amani, furaha na ushirikiano ambayo ndiyo tamaduni yetu.

Kuishi kwa mashaka au kuishi bila kukosoana katika taifa matokeo yake sio mazuri kikubwa tukosoane kwa hekima na kwa manufaa ya hili taifa letu.

Walionyimwa stahili zao wanasema wenyewe kuwa wanalipwa sasa hivi ni jambo jema taifa letu lina rudi mahala pake pa utu kwa watu wake.

Waliosema hataweza kutuongoza sijui wanajisikiaje..? Au nyie mnaoponda sijui mna roho au mawe.??

Mwisho. Myonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Mama anaupiga mwingi saana. Ni ombi kwa Mungu wangu wa mbinguni baba mwenye enzi zidi kumlinda na kumpa hekima Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan. View attachment 2250175

Weekend njema wakuu. Sabato ikawe njema na mzidi kumuombea raisi wetu
[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]

Makofiiiiiii
 
Back
Top Bottom