Hawataki kukubali ukweli kuwa Rais Samia anatuongoza vyema

Hawataki kukubali ukweli kuwa Rais Samia anatuongoza vyema

Habari wakuu sijawahi andika hapa kwenye hili jukwaa la siasa ila leo acha ni andike kidogo tu.

Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye raisi wetu ameonyesha muelekeo mzuri kwa kiasi kikubwa katika uongozi wake japo ni mapema kidogo. Wapo watu bado sijui ni seme wana usingizi au bado giza limetanda machoni mwao kwa maana ya kutoona tofauti ya awamu hii ya 6 na ile ya 5. Binafsi na furahishwa na utendaji wa raisi wetu wa awamu iliyopo madarakani Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuangalia namna anavyo zingatia ushirikishwaji wa idara zote katika kutenda au kufanya jambo husika ndani ya uongozi wake. Ndio yapo mapungufu machache hatuwezi sema yupo 100% ila kwenye hizo asilimia naimani amefikia 80% kupanda juu.
Aliipokea nchi kipindi kigumu hasa kufiwa na kiongozi mkuu wa nchi jambo ambalo ni geni.katika hili taifa letu. Yote alijitajidi na ameweza kutuunganisha kwa itikadi zetu tofauti tofauti, leo chadema na CCM wanacheka, CUF na Chedema wanakaa pamoja na CCM mtaani tunapiga story kadha wa kadha. Mambo ya kukaa mwaka bila ajira kwa wahitimu yameanza kutatuka japo idadi ya waliopo mtaani ni kubwa mno. Miradi iliyo achwa inakamilishwa na ameongeza miradi mingine. Fikiria ujenzi wa madarasa kwa mamia kwa shule zetu ni jambo jema na la kupendeza. Mhe amejitahidi kushirikiana na wataalamu kwa kila idara inayohitaji utaalamu. Ukiangalia kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi wa umma wataalamu wamekaa na kuja na ripoti nzuri ambayo imetumika kuwaongezea mshahara wafanyakazi wa umma. Demokrasia ile tuliyo izoea imeanza kurudi mahala pake, mambo ya kufanya maamuzi gizani hayapo tena.

Nyakati zimebadilika ila wapo wanaosema hafanyi lolote kwa macho yao yaliyozibwa ambayo hayaoni mabadililo kadhaa basi hawa tuwaweke kundi lile linalo tajwa "SUKUMA_GANG" hawa watu wao hawataki kuamini tusemalo au kuona watu tunaishi kwa amani, furaha na ushirikiano ambayo ndiyo tamaduni yetu.

Kuishi kwa mashaka au kuishi bila kukosoana katika taifa matokeo yake sio mazuri kikubwa tukosoane kwa hekima na kwa manufaa ya hili taifa letu.

Walionyimwa stahili zao wanasema wenyewe kuwa wanalipwa sasa hivi ni jambo jema taifa letu lina rudi mahala pake pa utu kwa watu wake.

Waliosema hataweza kutuongoza sijui wanajisikiaje..? Au nyie mnaoponda sijui mna roho au mawe.??

Kaushauri kwangu kwa utawala wake. Mhe Raisi kile kikokoteo kipya cha mafao nashauri au naomba wastaafu wapewe hela zao kwa namna wanavyotaka wao. Anaetaka kupewa yote apewe akishastaafu, anaetaka % kadhaa apewe kwa namna anayoona inamfaa yeye. Pesa ni zao wastaafu wasipangiwe wajipangie. Kikubwa washauriwe na wapate muongozo utakao wasaidia.

Mwisho. Myonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Mama anaupiga mwingi saana. Ni ombi kwa Mungu wangu wa mbinguni baba mwenye enzi zidi kumlinda na kumpa hekima Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan. View attachment 2250175

Weekend njema wakuu. Sabato ikawe njema na mzidi kumuombea raisi wetu
[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]
Hahahaha kumbe mna rais wenu hongereni
 
Sio tu kwamba ni chawa Bali ni kibwengo
Pole mkuu na acha roho za kichawi. Zama za kusujudi mtu ndio hivyo Mungu kaamua kutumalizia yale mateso.
 
Hahahaha kumbe mna rais wenu hongereni
Raosi wetu Watanzania. Wewe sio mtanzania. Hata matumizi ya maneno katika lugha hujui. Raisi wa taifa letu tunamuitaje.? Ukiwa na ujinga kwa kichwa chako usitake kila mtu ajaze huo ujinga wako kwenye kichwa chako. Tupo huru kuelezea furaha, kukosoa, kushauri na kupeana mawazo mema sio hizo chuki, hila, unyama, nk katika mabaya hatupo huko mkuu.
 
Acha kulitaja Jina la MUNGU Bure

Na Yesu kwenye siasa ameingiaje

Usilete mzaha , kwenye issue serious
Acha kumtishia mtu. Mungu ndiye aliye amua tu kutuvusha. Kama sio yeye hakika tungeteseka saana. Mungu huangamiza au huondoa utawala wowote wa kinyama. Kiongozi yoyote mwenye kuwatendea mabaya watu wake ni chukizo mbele za Mungu na Mungu humuondoa ili kunusuru watu wake. Usitutishe ukija kwa kutumia biblia tutakunyoosha pia.
 
Huyu jamaa ni mweupe kichwani , Kama Mama yake
Endelea kubet. Mweupe au mweusi kichwani ni wewe ambae unalazimisha watu wa seme utakavyo. Unayo haki ya kukataa mawazo ya mtu kwa hoja na sio kuruka ruka tu mara ooh mara eeh. Jitambue
 
Mungu yupi unayemsemea ww?

Kama Ni wa Mbinguni , hato-deal na Babel ( Id ya Mungu Babel )
Hizo ni ID tu mkuu. Sawa usijitoe ufahamu. Hapa tunatumia majina fake hivyo jitambue. Mungu ni mwema
 
We apo unamsudia nani ndo maana we kiroboto wa bi kiroboto
Sikujibu tena hii ya mwisho maana tutaonekana wote punguani. Huna hoja wala huna la kuelezea unaruka ruka hueleweki.
 
Safari mumemwagwa wengi humu. Kazi ya mwiguru hii
 
Raosi wetu Watanzania. Wewe sio mtanzania. Hata matumizi ya maneno katika lugha hujui. Raisi wa taifa letu tunamuitaje.? Ukiwa na ujinga kwa kichwa chako usitake kila mtu ajaze huo ujinga wako kwenye kichwa chako. Tupo huru kuelezea furaha, kukosoa, kushauri na kupeana mawazo mema sio hizo chuki, hila, unyama, nk katika mabaya hatupo huko mkuu.
Hahahaha hongera kwa kupata uyo raosi wenu
 
KWA akili iliyojaa matope nikuambie nn sasa we endelea kuimba pambio kibwengo master hahahaha
Mapambio ni yale yaliimbwa kumtukuza mungu mtu. Ila Mungu mkuu mwenye nguvu yupo makini zaidi
 
Acha kumtishia mtu. Mungu ndiye aliye amua tu kutuvusha. Kama sio yeye hakika tungeteseka saana. Mungu huangamiza au huondoa utawala wowote wa kinyama. Kiongozi yoyote mwenye kuwatendea mabaya watu wake ni chukizo mbele za Mungu na Mungu humuondoa ili kunusuru watu wake. Usitutishe ukija kwa kutumia biblia tutakunyoosha pia.
Labda Mungu wenu wa kuzimu maana MUNGU wa binguni hutenda kwa atakavyo sio kuwafurahisha vimbwengo kama wewe
 
Back
Top Bottom