Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Ina maana wananchi wameshindwa kuelewa nini Rais wetu anafanya hadi watangaziwe kwenye mabango?
Ina maana raia hawamjui rais wao hadi afanyiwe kampeni kwenye mabango ilihali yupo madarakani?
Haya mabango kila kona nchini yanaendelea kusimikwa kana kwamba tupo kwenye kampeni za uchaguzi aa urais yana sadifu nini haswa?
Kama yanalipiwa na wafanyabiashara, wao wanapata nini in collateral?
Kama serikali inatoa hela, mbona ripoti ya CAG ipo kimya.kwenye hili? Je hela inatoka kwenye vote gani ya bajeti?
Kama huu ndo ubunifu wa kitengo, basi tuna watumishi mafisadi huko ndani kuliko hata wanasiasa wetu.
Tunahitaji
- Huduma bora za afya
- Maji safi, salama ya uhakika
- Umeme usio katikakatika
- Miundombinu imara
- Katiba mpya
- Kushuka kwa mfumuko wa bei
- Kudhibiti rushwa