Pre GE2025 Haya mabango ya Mama Samia kila kona, nani anagharimia? Yanatusadia nini kama nchi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata yeye anajua hakubaliki ndio maana ametumia muda wote tangu ashike madalaka kujinadi kama mechi ya Simba na yanga, lakini upumbavu ni kwamba hiyo pesa wanayo itumia kuweka huo upumbavu ni pesa ambayo ingeweza kusaidia maisha ya Watanzania wengi wanao teseka maeneo mengi ya nchi
 
Lissu aliyalipua hayo mabango , Halafu walichokisahau ni kwamba , Mabango hayasaidii lolote , jiwe aliweka mabango hadi kwenye vyoo vya umma lakini mwisho akaiba kura
 
Haya mabango ya 🕔 mia yanakuza uchumi wa mifukoni mwa wapigaji waliofumania mgodi WA Kodi zetu TU.
Na hayana tija wala faida kwa taifa
 
Kama naye anayapenda basi Kuna shida mahali
 
Lissu aliyalipua hayo mabango , Halafu walichokisahau ni kwamba , Mabango hayasaidii lolote , jiwe aliweka mabango hadi kwenye vyoo vya umma lakini mwisho akaiba kura
Usimsingizie Jiwe!! Kazi za Jiwe zilikiwa zinajulikana na zinajitangaza zenyewe.

Nyie CHADEMA kumsema Jiwe ndo kimewapoteza kwenye siasa. Sijui kwanini hamjifunzi
 

Itakuwa pesa Mwarabu hiyo...
DPW.
 
Kitu kizito kichwani, ndio tukome mbele ya safari
 
Halafu Nchimbi anakuambia Mama yake kafanya makubwa na yupo kimya siyo kama wengine.

Hao wengine waliishia kujisifia tu majukwaani bure,yeye anatumia gharama pia kueleza anachofanya si bora angeandika kwenye miamba nchi nzima kama Bwana Nchemba.

Pale Kahama bango moja kubwa lipo pale kwenye lango la kuingilia stendi kuu ya mabasi, imagine.
 
Kibaya chajitembeza
 
Kuna mwalimu wangu wa psychology enzi hizo alikua ni raia wa Japan kupitia haya mabango nimekumbuka kauli yake moja.

Alisema "sehemu yoyote ukiona mtu anaibuka kujionesha kwa kutumia nguvu sana miongoni mwa wenye akili jua huyo ndio mjinga kuliko wote kwenye kundi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…